Kama una uwezo wa kifedha gen ya 11 ama Amd ryzen 5000 series ndio nzuri zaidi.
Sema budget zetu hizi za kitanzania ngumu mtu kutoa mamilioni ya Hela kununua laptop, wengi wetu tu nanunua laki 6 kushuka
Gen ya 2 mpaka ya 7 haitofautiani sana uwezo wa cpu, ila gpu za ndani kuna utofauti mkubwa, ndio maana unaona tuna recommend generation kubwa.
Ila kama Unapata Gen ya 2 ama ya 3 ina gpu ya Nvidia nzuri si mbaya unachukua, sababu ile weakness ya Gpu ya ndani inakuwa imeondoka.
Kama unanunua yenye gpu ya ndani ndio unaangalia na budget. Budget yoyote ya laki 3 kupanda angalau gen ya 4 Tafuta.
Ikifika budget laki 4 kupanda i3 Gen ya 6 ama ya 7, mpaka laki 6 Angalia i5 Gen ya 6/7
Budget Ikifika laki 8 unaanza kuangalia laptop mpya sasa.