Ni nani anaweza acha pesa akafuata passion?

Mgumu04

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
1,934
1,043
Nimeanza na kichwa cha habari kwa kuuliza je katika huu ulimwengu wa sasa kuna mtu anaweza acha kweli pesa au kazi inayo muingizia pesa na kufuata passion?

Katika miaka ya 2007s kipindi nipo A level kuna jamaa yangu alishakuwa na ABC za computer application weekend tukawa tuna drop(watu wa minaki na pugu hapa mnanisoma) jamaa akawa ananifundisha basic applications nikazidi kupenda mambo ya technlogy sana.

Nikiwa first year sasa mimi class ndio nikawa programmer wako teacher akitoa kazi tu jamaa hao wanakuja room nachapa codes(nafanya for fun) basi ziku zikawa zinasonga na nikawa na vimba kuitwa programmer. Nikiwa mwaka wa pili kukawa na short kozi za oracle(database), pc repair and maintenance na data analysis(Spss).

Mimi nikaanza kupiga pc repair and maintenance ndani ya wiki moja nikapata deal la kurepair pc za taasisi moja hivi DODOMA aise ile siku nimerudi na kibunda kikubwa sana(pesa) mambo ya programming tena yakaanza kupungua nimeonjeshwa asali sasa nikaanza kuchinga mizinga yangu.

Jamaa yangu yeye akawa anafurahia ku create data base anajisifu ku delete, drop tables na mambo mengine mengi sana mimi ikawa naendeleza kozi na kutafuta deals ziko wapi ,kipindi hicho nime sign up kozi za programming web development katika site ya coursera kwani nazisoma sasa.

Hatimaye mwaka wa mwisho huo hapo tumemaliza nikapata muda mwingi wa kuzama kwenye programming nikaaza kusoma kwa bidii sana msuli mpaka saa 7 usiku shemeji yenu akawa anamind kwanini natenga muda mwingi kwenye pc kuliko yeye, kiwaka vizuri sana kwenye programming nikaanza kutafuta kazi sasa za progrmming(kimbembe) unaongea na clients vizuri mnapatana umtengenezee system siku ya siku sound nyingi mteja anaingia mitini(kila ukiingia mitandaoni watu wanalalamika programming bongo miyeyusho), kipindi hicho nafanya biashara zangu maisho supa sana nafanya programming for passion suddenly corona hiyo ooh mambo yakaharibu business yangu totally ikafika wakati nakosa hata 1000 ya kufanya familia yangu ile aise maisha ya kufirisika yasikie tu bongo movies ilikuwa inapita hata wiki 3 sijala ndunda la shemeji yenu nguvu zinatoka wapi?

Jamaa zanguni nikiwacheki hawapokei simu , bahati nzuri kuna dogo wangu moja hii yeye alishakuwa na skills za mobile phone repair akaniambia bro msaada wangu kwako ni kukufundisha skills nilizo nazo za mobile phone repair nikasema poa within a week nikawa poa akaniambia sasa kanunue NCKDONGLE (Device ya ku flash simu) na vikorokoro vingine budget ikafika kama 900,000 nikanunua vyote.

Changamoto ikawa fremu sasa nazunguka mara huku mara kule wapi(pesa imekwisha hapa natafuta mtu anibebe kwenye fremu yake lakini hola). Hivi mtu akifirisika huwa ananuka? yaani kila mdau ninayemcheki ananikatalia. Kuna jamaa akanisaidia fremu(muda wangu wa kunyanyuka ulishafika tena) mambo yakaanza kunoga mambo ya software nikawa nayabuluza hatari(mafundi wengi software hawapendi kwa sababu ni ghalama sana imagine nckdongle inafika 370000).

Kiroho safi tu baadaya ya mambo yangu kusimama vizuri(hapa siwazi tena programming ni mwendo wa ufundi simu tu) nikamuomba nipange sehemu yangu na jamaa bila hiyana akakubaili nisimame peke yangu(Allah amuongezee utu huyu jamaa) basi nikapanga nikanunua spear za kutosha mambo sasa hivi ni more fire pesa inaingia vizuri tena sana na programming nimeanza kuipiga chini sifanyi tena vitu for fun.

Funzo;
1.usifanye vitu kisa tu ni passion utapoteza mkuu.
2. ukiwa na pesa jitahidi isipotee kufirisika ni kubaya sana.
3. usifanye vitu kuwafurahisha ndugu au marafiki ukikata ringi ndio wakwanza kukukimbia.
 
maelezo mengi mazuri but naona kama hayaeleweki vizuri! hongera
 
Mkubwa mbona kama hauko serious yaani unajiita programmer halafu ukanunua NCK dongle kwa laki 9
Nioneshe sehemu nilipoandika nimenunua nckdongle kwa 900k, soma taratibu mkuu hukimbizwi.
 
Kufanya kitu kwa passion tu wanafanya Sana wazungu, wenyewe wanaweza ishi miaka yote anafanya Jambo flani for passion na halimuingizii pesa,
Unakuta anategemea watu wadonate kwa kazi anayofanya tuu yaani ukipenda anachofanya unamchangia. Na wazungu wanachangia Sana wakiona mtu amefanya kitu kusaidia jamii kusolve tatizo flani.

Kwa bongo ukisema ufanye kitu kwa passion yaani utumie mda wako wote kukifanya utakufa njaa kwa sababu hata Kama unatengeneza solutions zinazotatua changamoto flani katika jamii hayupo atakayekupa pesa Kama donation kwa kile unachofanya.

Kitu pekee Cha kufanya nikuibadilisha passion kuwa business yako bila hivo utakwama Sana.
 
Siku zote wanaofanya Kwa passion ndo huwa wanaenda kutajirika mwishoni...

Nakushauri usiache hiyo passion
Itakuja opportunity hutaamini..


Bado Una safari ndefu
Ufundi simu soon utapata competition kubwa
Watu wengi wanajaa huko
 
Kma unapata hela ya kula unaweza fata passion yako kwakua mwsho wa siku italulrtea hela pia
 
Back
Top Bottom