Fahamu Laptop zinazofaa kwa Designers na Content Creators kabla hujanunua

Renald Gasper

Member
May 6, 2012
12
22
Kabla hujafanya uwamuzi wa kununua laptop yako mpya kwa ajili ya matumizi yako ya Graphic designing, Architecture, au Content Creation yafahamu haya.

NI MUHIMU!
• Category hii ya watu wa aina hiyo, wanahitaji PC (Laptop) yenye uwezo wa kustahimili program zao zenye uwezo mkubwa, kama CAD, Adobe After Effects, etc.

ZINGATIA HAYA:
🔲 SCREEN SIZE
✓ Kwa designer yoyote yule au Content Creator, hakikisha PC yako iwe si chini ya inchi 14. Kwanini 😕? Kwasababu, program nyingi huwa ni kubwa na kadri ya ukubwa wa project yako ndivyo itakavyo kuwa na mambo mengi kwenye screen yako. PC kama ya inch 13 itakupa shida sana, utakuwa kama unachungulia, pili utahitajika kuscroll maranyingi mno ili ku access mafaili au vitu ambavyo havionekani kwenye screen. Pia hii si nzuri kwa macho kwani program italazimika kufanya vitu viwe vidogo, icons, tabs, fonts ili kuweza ku fit kwenye screen.

- 14 inches na kuendelea ni perfect size kwa matumizi.

🔲 SCREEN RESOLUTION
✓ Hapa kiukweli hakuna mjadala, ila kama wewe ni designer au Content Creator alafu unatumia laptop au screen yenye resolution HD (1080*720) na below, haupo serious na kazi yako, na hata quality ya kazi zako itajulikana.
- Optimum au resolution ya kuanzia hakikisha ni FHD (1080*1920) na kuendelea, kumbuka 4k au 8k kwenye screen ya inch 14 kushuka kwa upande wangu ni kupoteza hela kwani hauitumii kwa full potential, ni kama kuendesha sport car kwa gear no. 2 basi.
- Resolution ni muhimu sana kwani inasaidia quality ya vitu unavyo viona kwenye screen yako, ili hata ukipost viwe sharp na sio pixelated.

🔲 SCREEN COLOR ACCURACY
✓ Hapa jamani ni pamuhimu mmno kuliko mnavyo dhani, wabunifu wengi hapa bongo wanaotumia njia za kidigitali hawaelewi hili, LAPTOP au screen yako hataiwe nzuri au ya bei kiasi gani kama color accuracy yake ni mbovu, kazizako zitakuwa mbovu kwenye upande hasa wa rangi.
- Color accuracy, hii inakusaidia, kile unacho kiona kwenye screen yako ndicho kitakavyo onekana kiki printiwa au kiki postiwa, hasa kwa upande wa rangi. Ulisha wahi ona unaona kwenye screen yako rangi ya orange alafu una print, kinacho toka nichaajabu au picha yako inapendeza kwenye screen ila unapo post rangi nitofauti, mara imekooza kupita kiasi kiufupi ni mbaya. Na hapa maranyingi utasikia printa yako mbovu 😁
- Hakikisha screen yako iwe na color accuracy kuanzia 60% RGB nakuendelea 80% - 100% recommended. Hii itakusaidia sana hata katika macho yako hauta jisikia kuchoka kwa haraka au kichwa au kichefuchefu ukitazama screen mda mrefu.

🔲 RAM
✓ RAM ni kigezo kingine cha muhimu sana, kwani hapa ndipo uchawi wakufanya PC yako iwe nyepesi au na speed inategemea hapa pia. Haijalishi uwe na processor yenye nguvu kiasi gani, Core i9, 11th generation (with 8 cores) kama ramu yako haina speed au huna ya kutosha, speed yako haitatofautiana sana na mwenye core i3.
- Kwa watu wa category hii hakikisha RAM yako sii chini ya 8GB na kama unampango wa kufanya VFX au heavy rendering hakikisha una RAM si chini ya 16GB - 32GB.
- Lamsingi sana, ukitaka kuichosha PC yako nahata kuuwa RAM zako ni kuto kubalanci yaani unajidai mjanja unaweka RAM moja 4GB na nyingine 6GB eti una 10GB hapo unaleta matatizo, PC sio binadamu unapo badilisha RAM au Ku upgrade hakikisha una balance kama ni 4GB zote ziwe 4GB na zote ziwe na speed moja kama ni 3200hz zote ziwe hivo tena ukiweza zote ziwe kampuni moja, unapo changanya RAM ni kama kuchanganya pilau na ugani, afu utegemee utamu uwe sawa.

🔲 GRAPHIC CARD
✓ Hapa sasa, watu ndo hawaelewi, kama wewe upo au unategemea kuwa mtu wa category hii (Graphic Designers au Content Creators) lazima uwe na Graphic Card. Hii itasaidia color nzuri kwenye screen, pia itaisaidia RAM mzigo kwani kama hauna Graphic card, sehemu ya RAM itatumika kama Graphic card, na performance ya huwa ni ovyo, kwasababu hiyp siyo kazi yake.
- Kwa watu ambao hawana mpango wa kufanya rendering, VFX, 3D au 4D design sana, hakikisha uwe na Graphic card 2GB (Dedicated)
- Na kwa wale wenzangu ambao wana taka kufanya VFX, RENDERING, ANIMATION NA LOTS OF 3D AU 4D HATA WA ARCHITECT, hakikisha usiwe na chini ya 4GB, 8 GB na kuendelea ni recommended.

🚨 Kuwa makini hapa, kuna Graphic RAM mbili kwenye PC, HUWA kuna Internal VRAM na DEDICATED VRAM ninayo ongelea hapa ni DEDICATED hiyo nyingine haina umuhimu wowote wa msingi hata kama ukute PC ina internal VRAM 16GB ni takataka, hiyo PC itakuwa na RAM 32GB na sehemu yake ndiyo hiyo 16GB.

💰 Vingine vilivyo baki, ni wewe Storage, 360x capability, touch screen, long battery life, etc.

Like, na share watu wapate kujua, comment na utajibiwa, follow for more mafunzo soon.
 

the_legend

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
1,550
6,679
Asus swift 4, Apple Macbook air, Lenovo flex 5, na some HP. Sijazitaja kwani PC nyingi zina version zake ambazo unakuta version moja ni bora wakati nyingine ni mbovu, hovyo fwatilia na soma specs uifahamu vizuri kabla huja nunua.
Uzi mzuri. Mkuu bei ya Asus swift 4 na Lenovo flex 5 ipoje?
 

privacy

JF-Expert Member
Apr 20, 2014
1,431
1,227
Asus swift 4, Apple Macbook air, Lenovo flex 5, na some HP. Sijazitaja kwani PC nyingi zina version zake ambazo unakuta version moja ni bora wakati nyingine ni mbovu, hovyo fwatilia na soma specs uifahamu vizuri kabla huja nunua.

MacBook air ipi ina graphics nzuri boss kwa ishu za graphics? Nlidhani ungetaja PRO as ndio toleo powerful compared na hiyo uliyo andika
 

Andrew Tate

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
3,324
5,000
Hiyo computer lazima iwe ni high end So hapo itabidi uwe na pesa sio chini ya 5 million.

Kitu ambacho kwa uchumi wa watanzania wengi ni ndoto.
 

Renald Gasper

Member
May 6, 2012
12
22
Hiyo computer lazima iwe ni high end So hapo itabidi uwe na pesa sio chini ya 5 million.

Kitu ambacho kwa uchumi wa watanzania wengi ni ndoto.
Hapana, 3 Million kushuka unapata mpya, USED ukiwa vizuri chini ya 1 Million unapata. 3 Million kupanda hizo ni kwa Ma professional, wanajua nini wanakihitaji specific.
 
10 Reactions
Reply
Top Bottom