Je, kuna maisha mengine baada ya hapa duniani?

 
Kim Jong Jr hapo juu uliponinukuu ungepaswa kutenganisha maoni yako, na yale ambayo mimi nimeandika.

Kitendo cha kufanya nisomeke kana kwamba nimeandika maoni yako, ambayo ni potofu, siyo cha kiungwana hata kidogo.

Naomba Moderator liangalieni hili maana ni kasoro ya App yenu.
 
Well huo ni mtazamo wa kibinadamu,
Lakini hata Sisi binadamu, hatukutokea tu, kuna master planner alituweka hapa.
Na yeye kupitia vitabu vyake(wengine hawaviamini) kasema kuna maisha baada ya kifo,
Ukiona mtu ana simu ya tekno au I phone, moja kwa moja unaamini imetoka china, au USA, na, samsung imetoka Korea, na unanunua unatumia,ukiamini kabisa ma designer wa USA wapo vzr kuliko china, na unaona ufahari kuwa na Iphone kuliko Tecno! Richa ya kwamba hujawahi, hata kuvuka chalinze achilia mbali kuona hiyo Iphone ikitengenezwa!
Ni logic ndogo tu, na wengi wa wale wanaodai hakuna maisha baada ya kifo, hata elimu ya dini kidogo hawana, hawawezi hata kukupa Historia ya vitabu vitakatifu, ka elimu kadogo, kasoma vijarida na kusikiliza upuuzi wa story book, anakuja hapa mishipa ya shingo imemsimama,
Kuna vitu vingi watu wa kawaida hawajuhi, chukua muda uwasome uwasikilize viongozi, wa dini(sio mwamposa, wale wenye PHD za theology), mapadre, Mashekh kama Dr Naik wa peace TV, Myles Munroe, TD Jakes, John hagee,na wasomi wengine kama Chris Mauki,Vusi Thembekwayo, Bagonza nk,
Sikiliza waliobobea kwenye maswala ya dini, kuna kitu utajifunza.
Sio una sikiliza story book, kutoka kwa form 4 leaver, then unajiona umebokuuuuuuaaaaaa!
 
Kwanini usimuombe mungu atenganishe nilichokichanganya kwenye andiko lako ?


Unakimbilia Kwa moderators , je wana nguvu kuliko mungu ?
 
kama binadamu alitokea Kwa master planner na huyo master planner alitokea wapi? Chanzo hakipaswi kuishia Kwa master planner lazima turudi nyuma tujue na huyo master planner alitokea wapi! By this logic Chenye chanzo kina chanzo.


Huyo mungu kwanini atumie watu wengine Ili yeye ajulikane ( hao uliowataja). Kwanini asiumbe binadamu awe anamjua mungu by default pale anapozaliwa ? Yeye mungu anaeijua kesho yetu kwanini aumbe binadamu anaemjua kesho atatenda matendo yasiyompendeza mungu na Kisha anamuhukumu huyo binadamu.

Hivi wewe unajua mtoto wako kesho atazini na nguvu za kumfanya asizini unazo ila unamuacha azini halafu unampa na adhabu! By the way hata hiyo dhambi ya kuzini muasisi wake sio yeye bali ameikuta!


Huyo mungu wenu ni muonezi na dictator! NDIO!

Hizi ni hadithi za uchwara
 
Bro kama Mungu anakuwa na chanzo huyo sio Mungu tena, Mungu hafungwi na muda,
Bro najua wewe una amini una akili, lakini bila Shaka, hujawahi kuziona akili, Ila unaamini unazo! Ni, logic ndogo tu, there is no way we just happened to be here! In our body, na mifumo yote ya kimwili, digestion system, nerve system nk, surely some baby designed it! He/she had to exist beyond matter, time, nk.
 
Yes najua kesho mtoto atazini,na nitamuadhibu, lakini good news ni kuwa, ana free will, anaweza akakataa kuzini vile vile, na akizini, toba IPO, anapata msamaa
 
hapa DUNIANI SIO KWETU MAKAZI YETU YAPO MBINGUNI.
Tumekuja tutapita..
Tutakwenda kuhukumiwa kutokana na mate ndo yetu.
Umedhulumu mtu utakwenda kumlipa,umemuua mtu utakwenda kumlipa,umempiga utakwenda kumlipa n.k
Haiwezi KUPITA HIVI HIVI.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Katika hayo kuna ya ukweli na uongo.
 
Hivi wakuu tukiacha hizi nadharia na dhana zingine za kufikirika kuhusu hatima yetu baada ya kifo.

Nataka tuongee kiume sasa.

Hivi ni kweli tukifa kuna mahali tunaenda au ni siasa na kufarijiana tu ilmradi maisha yasonge?
Subili wazungu waje wakupe ukweli sababu ndio unao waamini sidhani hapa kama kuna utakae muamini
 
Tahadhari tu kwamba hao wanaoharakisha kuwahakikishieni kwa ujasiri wote kwamba hakuna maisha baada ya mauti, hawajawahi kufa kamwe.
Kama ambayo hao wanaowaharakishieni kuwaambia kwamba Kuna maisha baada ya kifo hawajawahi kufa kamwe. The vice Versa is true chief.
 
umesema vema mkuu. lete proof tufunge huu uzi
 
Hivi wakuu tukiacha hizi nadharia na dhana zingine za kufikirika kuhusu hatima yetu baada ya kifo.

Nataka tuongee kiume sasa.

Hivi ni kweli tukifa kuna mahali tunaenda au ni siasa na kufarijiana tu ilmradi maisha yasonge?
Swali lako linaibua hisia za mimi kuuliza kama unaelewa maana ya kufa
 
Tahadhari tu kwamba hao wanaoharakisha kuwahakikishieni kwa ujasiri wote kwamba hakuna maisha baada ya mauti, hawajawahi kufa kamwe.
Hata wanaoeneza uongo huo kwamba kuna maisha Baada ya kifo nao hawajawahi kufa.

Uhakika kwamba hakuna maisha baada ya kifo unatokana na uelewa wa dhana yenyewe kama ilivyo.

Unaelewa maana ya kifo/kufa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…