Je, kuna maisha mengine baada ya hapa duniani?

Unataka facts au blahblah blah kulingana na msimuliaji ?
 
Wakuu bishanenii, mwisho mje na majibu ya kueleweka hapa. Nataka kusoma mistari miwili na kuelewa sio maelezo mareefuu, mara kasome wakorinto
 
Hivi wakuu tukiacha hizi nadharia na dhana zingine za kufikirika kuhusu hatima yetu baada ya kifo.

Nataka tuongee kiume sasa.

Hivi ni kweli tukifa kuna mahali tunaenda au ni siasa na kufarijiana tu ilmradi maisha yasonge?
Ndiyo.
 
Ulishawaza inawezekanaje au ni mtumwa wa fikira na hisia za watu.
 
Jibu ni kwamba "the truth sits upon the lips of dying man" hayo mengine ni kufarijiana tu.we subili siku ufe ndio utajua.maana hakuna aliyewahi kufa na kurudi kuleta mrejesho.
 
Wewe una kitu ungetusaidia hapa. Ila shida yenu mnaongea vitu nusunusu, mnafumba fumba, na hapo ndio tunapata mashaka na kuto waamini. Wekeni mambo wazi. Fikiria uwazi wa jambo hili ulilo limega nusu na kutuambia kuhusu koo ungeliweka wazi ungeponya wangapi? Kama kweli kuna thawabu, ugehesabiwa tjawabu kiasi gani kupotia kupona kwao?

Hapo ndipo mnapotupa mashaka
 
Reactions: A43
Hivi wakuu tukiacha hizi nadharia na dhana zingine za kufikirika kuhusu hatima yetu baada ya kifo.

Nataka tuongee kiume sasa.

Hivi ni kweli tukifa kuna mahali tunaenda au ni siasa na kufarijiana tu ilmradi maisha yasonge?

Kwani wewe kabla ya kuja huku duniani ulikuwa unaishi wapi?
Ndivyo utakavyoenda kuishi ukitoka hapa duniani.
 
Wakuu mnaotaka ku prove kwa maandiko mbinu hii sio inayohitajika hapa. Ingekua ku prove kwa biblia na quraan (sijui kuoandika) inakubalika kwenye hili, basi hakuna kiumbe kingebisha. Shida ni kwamba hizo prof za kwenye vitabu ni nadharia na sio practical, watu hawataki mistari wanata practical
 
Hivi wakuu tukiacha hizi nadharia na dhana zingine za kufikirika kuhusu hatima yetu baada ya kifo.

Nataka tuongee kiume sasa.

Hivi ni kweli tukifa kuna mahali tunaenda au ni siasa na kufarijiana tu ilmradi maisha yasonge?

Utakwenda kuishi huko huko ambako ulikuweko kabla ya kuja hapa duniani. Jaribu kujiuliza babu na babu na babu hadi babu yako wa kwanza walikuwa wanaishi wapi!
 
Point of agreement. Uzi umeisha.
 
Scientifically (Practically) you can’t prove life after death na hii ni kwasababu Sayansi haitoi majibu ya kila kitu. Sayansi ina ukomo wake. Sasa kama mnaanzisha mijadala ambayo mnalimit watu ku-refer to the appropriate references, basi ni heri ufunge mjadala wako.

Life after death is a spritual thing (science doesn’t go into spiritual life). A good way to deal with spiritual matters ni through Holy Books ambazo wewe hutaki kusikia. Huwezi kuuliza swali la Civics halafu utegemee majibu kutoka kwenye kitabu cha Chemistry.
 
Nakubaliana na wewe kwa kuwa dini ni biashara, so nguvu hutumika ili pesa ipigwe. Sasa mkuu, kuna wale wahindi wanaoabudu ng'ombe, vipi kule injili itafika lini?
 
Yan mungu alete Dini, watu Fulani Tu [emoji23], alafu wengine wabaki kupokea mapokeo Tu,
Huyo mungu ni mchoyo Sana wa elimu, halafu ni mbaguzi
Eti, yaani uifuatilia hizi dini tunzotamba nazo ni za wazungu tu, hakuna dini imetokea kwa weusi. Hizi dini ni biashara za wazungu, kwa sasa na weusi wameshtuka wameanza piga pesa tu
 
Nakubaliana na wewe kwa kuwa dini ni biashara, so nguvu hutumika ili pesa ipigwe. Sasa mkuu, kuna wale wahindi wanaoabudu ng'ombe, vipi kule injili itafika lini?

Wapo wanaotumia Dini kama Biashara yes hatukatai na wananufaika kimaslahi. Lakini tukirudi kwenye sole purpose ya kuanzishwa kwa Dini, hilo sio lengo lake. Ni kama ambavyo silaha zimeundwa kwaajili ya protection lakini hilo halizuii wenye nia ovu kuzitumia kujipatia mali. Soma zaidi kuhusu falsafa ya Dini.

Hakuna mahali Injili haijafika. Kila mtu ataisikia, ila kuguswa ni Neema. Huko India kuna watumishi wengi tu wa Mungu wanamtumikia Bwana Yesu. Hata China wapo budhist waliobadili maisha yao na kumfuata Kristo.
 
Kama ni hivyo mkuu kwamba hakuna ushahidi wa kuthibisha pasi na shaka isipokua kwa kutumia vitabu (theoretically) tu, basi niungane na mjumbe aliyesema jibu la swahili hili kama huamini basi liwe 'sijui' kama ilivyokua sijui kama kuna maisha kabla nizaliwe basi sijui pia kama kuna maisha baada nife. Ila kwenu mnao amoni mnayo majibu mkuu
 
Ooh hallelujah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…