Je, kukataliwa au kutothaminiwa au kuonekana ni wa Ajabu na Kero ni Kurogwa au una Jini ndani yako?

Cognizant

JF-Expert Member
Aug 13, 2022
491
1,056
Unakuta kuanzia Wazazi wako, Ndugu na hata Marafiki bila sababu yoyote au Kosa lolote lile Wanakudharau, Hawakuthamini na Wanskuona ni Kero, Mzigo na hata Takataka Kwao. Na hali hii inaweza kukuta ukiwa una Ajira yako na hata Pesa au huna Ajira na Pesa vile vile.

Na kama haitoshi pia hata ukiwa unamsimamisha Mdada ili umsalimie tu au mjuane au hata Umtongoze ukiongea nae tu hachukui hata Sekunde 10 anaondoka na hakupi Umuhimu wowote sana sana anakuwa kama vile anakudharau na anakushangaa.

Na unaweza kukuta hali hii imekutokea tu miaka ya karibuni kama 10 hivi iliyopita ila miaka ya nyuma zaidi hukuwahi kutokewa nayo na ulikuwa unapata Ushirikiano mkubwa sana kutoka kwa Makundi tajwa ya Watu.

Je, hali hii husababishwa na nini hasa? Kurogwa au Kutupiwa Kitu kibaya na Maadui zako kuanzia Wazazi, Ndugu na Jamaa au huwa unakuwa na Jini ndani yako linalokutesa hivyo Maishani? Na je, Dawa yake au Suluhisho lake huwa ni nini ili uwe vizuri?
 
Swali la msingi, wewe mwenyewe unajichukuliaje/kujiwekaje?

Maana sio unajiweka kama jitu la ovyo ovyo, tabia za kijinga jinga halafu unataka watu wakuheshimu.

Jitu kama li Mwijaku hata likichukuliwa la ovyo atamlaumu nani ikiwa mwenyewe anajifanya hamnazo.
 
huwa ni hali tu inatokea....na huwa haidumu, ila kama unaishi kanda ya ziwa hali hiyo ni ya kawaida na inatakiwa uwe bize zaidi na mambo yako......pwani na sehemu nyingine ambazo mwanamke hujitambua kama mwanamke ni nadra sana hali hiyo kukutokea labda kama umechezewa
 
Oga maji ya chumvi rafiki yangu,oga ukinuiza ya kwamba natoa mabaya yote katika mwili wangu,navunja roho ya kukataliwa,na vuta kibali mbele za watu na ninavuta roho ya upendeleo kwangu,watu wote wanithamini na niheshimike kwa watu wote,Laana na mikosi yote iondoke

Some time watu tunapata mikodi pasipo kujua,au kutupiwa vitu vibaya,mwonekano wa kinyonge nk.

Chumvi ina nguvu ya kuvunja mabaya,oga kwa imani kwa siku saba mfululizo,iwe asubui au mchana hata usiku,chumvi ya mawe,chota kiganja kimoja tia kwa maji yako oga.
 
Kabla hujawaza kuwa umelogwa au kutupiwa jini jaribu kuangalia jinsi unavyo amiliana na watu, Angalia ongea yako, uvaaji wako na mahusiano yako na jamii kwa ujumla ukiona mahusiano yako na jamii ni mabovu basi badili tabia na mwenendo wako.
Tuje upande wa pili kama mwenendo wako ni mzuri basi huenda ikawa umetupiwa nuksi au umefanyiwa hasadi hivi vitu vipo sana tu kwa kifupi umefanyiwa uchawi wa nuksi sasa unawezakuwa umefanywa kwa kutupiwa jini la nuksi na kukataliwa au umefanyiwa bila kutupiwa jini yote yanawezekana.
Hayo uliyoyataja ni dalili za mtu mwenye nuksi dalili zingine zinaweza kuwa kama kujihisi uvivu sana, kuchukia kazi , kujichukia mwenyewe na kuota ndoto za mambo mabaya kama vile upo jalalani, umezungukwa na nzi, ndoto za nyoka n.k kwa kifupi ndoto mbaya.
Nikupe tiba rahisi sana ya kuondoa nuksi mwilini, Chukua chumvi ya mawe changanya kwenye maji ya kuoga kisha oga fanya hivyo kwa siku tatu mfululizo.
Njia nyingine chukua majani ya mti wa mbaazi yatwange upate unga wake kisha changanya kwenye maji ogea kwa nia ya kuondoa nuksi na mabalaa hii njia ni nzuri sana na kama kweli umefanyiwa uchawi unaweza tetemeka au kuishiwa nguvu hapo jua dawa inapambana na uchawi .
Kumbuka: Mtangulizi Mungu kwa kila jambo kwani yeye ndiye muweza wa kila kitu miti hii na dawa nyingine ni sababu tu na Mungu mwenyewe ndio anajua siri zilizopo kwenye miti na dawa kwa ujumla hivyo fanya hayo ukimtegemea Mungu.
Mungu akusaidie
 
Linaitwa Gundu bob,hulioni Kwa macho ila lipo,wewe unajiona sawa ila wenzako wanaona kama umejinyea.Naskia wanasema ukioga baharini linaondokaga.
 
Back
Top Bottom