Je kiswahili kinajitosheleza?

IrDA

JF-Expert Member
Aug 26, 2010
743
350
Eti Kiswahili kinajitosheleza...nyoooo!!
Hakijitoshelezi hata kidogo
Jana nilikuwa na mjumbe mmoja mkongwe wa TATAKI(Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili).Bila aibu akashindwa kunipa tofauti ya maneno HEAT na TEMPERATURE katika kiswahili.Na akakubali kuwa kiswahili hakijitoshelezi.Nyie mwasemaje?
 
Heat: Joto
Temperature: Kiwango cha joto
Unauhakika huyo mtu hajakudanganya? mbona rahisi tu?
 
Temperature: Halijoto ni neno la kutaja hali ya kitu kama ni baridi au moto

Heat: Mvuke, Fukuto, Harara, Hamasa, Hari, Joto, Moto, Mwako, Uharara, Ujotojoto, Umoto, Umotomoto, Vukuto,
 
Bwana wamayanga ulijilidhisha kwamba huyu mtu aliyeshindwa kujua tofauyti kati ya heat na tempreture ni wa tasisi hiyo?
 
Eti Kiswahili kinajitosheleza...nyoooo!!
Hakijitoshelezi hata kidogo
Jana nilikuwa na mjumbe mmoja mkongwe wa TATAKI(Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili).Bila aibu akashindwa kunipa tofauti ya maneno HEAT na TEMPERATURE katika kiswahili.Na akakubali kuwa kiswahili hakijitoshelezi.Nyie mwasemaje?

Kuwa "Mjumbe mkongwe" wa taasisi ya kiswahili hakumaanishi kuwa yeye ni mfasiri "translator" wa lugha. Pengine hayo maneno ya Kiingereza uliyoyauliza hayajui maana yake. Ingawa ni kweli kiswahili hakijitoshelezi lakini hayo maneno yana kiswahili chake:

Heat = Joto
Temperature = Harara
 
Hakuna Lugha yenye kujitoshereza hapa duniani, kila Lugha kwa namna moja hama nyingine imekopa baadhi ya misamiati au baadhi ya maneno kutoka lugha nyingine.
 
we nae huwezi, HEAT-JOTO, TEMPERATURE-JOTORIDI.
Ninavyoelewa mm Temperature ni Halijoto. Hii JOTORIDI umeipata wapi mkuu?

Eti Kiswahili kinajitosheleza...nyoooo!!
Hakijitoshelezi hata kidogo
Jana nilikuwa na mjumbe mmoja mkongwe wa TATAKI(Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili).Bila aibu akashindwa kunipa tofauti ya maneno HEAT na TEMPERATURE katika kiswahili.Na akakubali kuwa kiswahili hakijitoshelezi.Nyie mwasemaje?
Kwanza, kwa mkongwe mmoja wa TATAKI kutoelewa tafsiri ya baadhi ya maneno, haina maana kuwa Kiswahili hakijitoshelezi.
Pili, kukosekana kwa tafsiri ya moja kwa moja ya maneno toka au kwenda lugha nyengine, haina maana kuwa lugha hiyo haijitoshelezi. Elewa kuwa, hasa maneno ya kisayansi na kiufundi kila siku yanaongezeka kutokana na uvumbuzi wa vitu vipya, na si lazima majina ya vitu hivyo kuwa na tafsiri katika lugha nyengine. Mfano, nani atatafsiri kwa lugha yoyote neno Ipad?
Lugha ni mawasiliano na hata tafsiri nzuri ni ile inayoakisi mawasiliano na sio maneno tu.
 
Kiswahili ni lugha inayojitosheleza. Ninavyofahamu mm hakuna lugha hata moja duniani inayoweza kusimama yenyewe ikajitosheleza ktk mahitaji yake yote.

Lugha yyt inayotumika kwa jamii ikakidhi lengo la mawasiliano ni bora.
 
Hakuna lugha ambayo haijakopa kutoka lugha nyingine, kwani lugha ni sawa na mahusiano ya watu au mataifa mbalimbali, kuchanganyika kwao ndio kunakopelekea baadhi ya maneno ambayo lugha moja kuazima kutoka lugha nyingine, hali hii uitwa kutohoa, na wakati mwingine neno kamili linashindikana kutoholewa na kubaki kama lilivyo au kutafuta msamiati mpya kwa ajili ya ilo neno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine.

Leo hii tunabishania maneno ya kiingereza kwenda kwenye kiswahili, na hali tunasahau kuwa kuna maneno ya kiswahili ambayo hayapo kwenye Kiingereza.

Waswahili wana maneno ambayo pia tumeyatoa kwenye lugha nyingine na kuyafanya kuwa yetu kama vile, Pilau, Biliani, chapati, (Kihindi), na kuyaweka kwenye msamiati wetu, vilevile kuna maneno kama Wali, Mchele, Ubwabwa, K/Vitumbua maneno ambayo kwa Kiingereza hayapo. Zaidi ya neno mchele (Rice) hawana tena neno lingine kutofautisha kati ya wali, ubwabwa, pilau na biriani. Kuna neno kama Ugali, mlenda, mchicha n.k

Vile vile tuna maneno kama Bwana shamba, lala unono, mwiko, upawa (vifaa vya kupikia), Chimpumu, dengerua, gongo (aina ya pombe), kuuza sura, kindumbwendumbwe, mchakamchaka, sadakarawe, Pole, Chanda, Askari, Hakuna matata, Jambo, K(V)ipusa, swahiba, Shoga, Basha, waubani na mengine meeeengi.
 
Back
Top Bottom