Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,498
- 113,595
Nakuunga mkono 100% kuwa na principle ya kutosikia la mtu. Ndoa nyingi zimevunjwa kwa maneno ya pembeni haswa mnapokuwa ni wanandoa mnoishi mbali mbali.Nadhani hapa BAK umegusia another dimension... "mambo ya kuambiwa"..kuna watu wanadhani ni vema kumtonya mtu pale Wanapojua habari za mhusika( nadhani mmenielewa hapa).
Je, ni vizuri wewe kuwa chanzo cha habari katika ndoa za watu? na je, wewe kama mwana ndoa utapenda kuletwa habari kumhusu mwenzi wako?
Binafsi sitapenda kuwa chanzo cha habari maana sitakuwa nawasaidia wana ndoa bali kuwafarakanisha.Vile vile sitapenda kuambiwa maana nisichokijua hakitanidhuru!
Nilipoanza maisha ya ndoa, muda mfupi nikahamia London, then, DC, US, ambako wife alibaki mimi nikarejea Bongo.
Kila mwaka nilikuja DC for visit na mambo yalikuwa safi. Wakati fulani akaja mtu toka DC anatufahamu, akanieleza mambo ya wife huko DC na kusisitiza nisiulize kwenye simu maana wife atamhisi ni yeye maana ndio aliyekuja bongo. Japo nilinyamaza I was sudenly cold mpaka nilipokuja DC.
Ingawa wife alijitahidi kuwa as usual, mimi nilijikuta na kumuona cold mpaka nilipokuja kuuliza. Aliruka hatua mia na kudai huo ni umbeya wa wabongo wa DC. Naye akasema amesikia mengi juu yangu Bongo ila ameyapuuza. Japo hatimaye tuli compromise, life has never been the same.
Jamaa aliyeniletea habari akatangaza, 'nimetengenezwa'.
From there tukakubaliana hakuna kusikiliza lolote, hata akitokea msamaria mwema wa kuleta habari za bure, dawa ni kumwambia 'ishia hapo hapo' tuendelee na habari nyingine.