Je Kipoozeo ni tiba ya kero katika ndoa au mahusiano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Kipoozeo ni tiba ya kero katika ndoa au mahusiano?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Jan 24, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Katika kujadili misukosuko na dhoruba zinazokabili ndoa na mahusiano ya kimapenzi, watu wamekuwa na mikakati mbalimbali ya kustahimili na kuhimili ( coping mechanisms). Ndoa nyingi zipo katika vita baridi bila ya wanaume kujua kinachoendelea vichwani mwa wake zao. Kuna hili moja nimeliona katika mjadala hapa JF -  Suali langu ni hili:
  1.Je, hiki ni kitu kilichopo katika yale mambo yanayofundwa kimila au kwenye kitchen party au ni suala la mtu akili-kichwani mwake?

  2.Hivi wanaume wanapowakosea akina mama na kuona wamesamehewa hudhani imeisha kweli au nao huwa na wasiwasi?

  3. Akina mama mnadhani kuna njia mbadala ya kumaliza maumivu ya kero zinazowapata kwenye ndoa ( haswa suala la kuendewa kinyume - kukosekana uaminifu kunakofanywa na waume mara kwa mara) badala ya kipoozeo?

  Naomba michango yenu.
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...WoS umeninukuu vibaya, swali langu liliishia hapa;
  ...aliyeyaandika haya;
  ...sie mie!!!:)...ni mwanachama mwingine wa JF!

  hata mimi ningependa kujua kwanini watu wanaona short cut ya kutatua kero za ndani ni kuwa na mapozeo nje...
  Tuendelee...
  ...We dare talk Openly here!
   
 3. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2009
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kipozeo ndio nini?
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  kuwa na mwanamke au mwanaume nje ya ndoa.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nakiri kuwa sehemu ya pili ya nukuu si yako mkuu..ni ya mchangiaji mwingine kwenye thread ya " nani mvumilivu zaidi katika ya mwanaume na mwanamke"...
  samahani kwa usumbufu.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,616
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kipoozeo ni tiba ya muda ya maumivu ya penzi ila sio dawa wala sio suluhisho la kudumu. Suluhisho la kudumu ni kufikia stage inayoitwa spritual union ambayo lazima kazi ifanyike kufikia hapo.

  Mapozeo ni suluhisho la muda kwa kupata faraja ya sex kupooza aumivu ya roho kutokana na kutendwa na mwenzi wako. Dawa ya kudumu ni kujua chanzo kilichopelekea kutendwa.

  Wapenzi wowote ambao hawajafikia spritual union kwenye sex, wanachance ya kuwatenda wenzi wao. Na ni kawaida mtenda akitendewa hujihisi kaonewa.

  Formular ya kufikia spritual union, inapatikana katika kitabu cha 'Kama Sutra' nikiielza hapa ni mambo ya kikubwa, ila nitawapa matokeo ya spritual union.

  Spiritual union hufikiwa pale ambapo wapenzi mnafanya juhudi za kufikia simultenous orgasm kwa msaada wa love meditation, hiyo simultenous orgasm inageuka kuwa multiple orgasm ambapo kila mmoja wenu anajihisi hana mwili tena kwa tendo hilo linawablend mnakuwa mwili mmoja na mnaishia usingizini.

  Hiyo ndiyo the highest level ya love bonding, na baada ya hapo, huwezi tena kupata hamu na mtu mwingine yoyote ila yule wako tuu. Mwingine, hata akuvulie na kukupanulia, hakuna kitu kwa sababu ile spiritual bonding, inaseal mambo yote ya kimwili na ni spirit inatake control. Imekuwa mwili mmoja.
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kuna rafiki yangu ameanza mapenzi na mke wa mtu..tena moto moto hata anamfuata Dodoma sasa ni 7 years..na wameshibana sana ..hata wanajiiba wanaennda Zenj kwa kificho! Huyu mwanamke ana kazi nzuri sana na pesa nzuri..sema mme wake yuko dar amemfrastrate kwa kuchukua dem nje ya ndoa!

  Je kulipiza kisasi ni jawabu?
   
 8. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Pichaz .. peleka kwenye ze*****
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...bado sijaona raha ya kulipiza kisasi iwapo ni kwa kujiiba, na kujificha ficha.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,874
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Mimi kwa maoni yangu binadamu kama wanyama hatukuumbwa na tabia ya kuwa na mwanamke mmoja au mwanaume mmoja. Hili limeletwa zaidi na dini na ustaarabu. Angalia hata wale waislamu walioa wake wanne bado wanaangaza huku na kule pamoja na kuwa wana wake wanne.

  Kwa hiyo hiki kipozeo ni namna tu ya kuficha ukweli halisi na kupretend kwamba kipozeo ni muhimu kuwa nacho hasa kama kumetokea ugomvi nyumbani basi mwanaume au mwanamke anakuwa na kippozeo chake kinachomsahaulisha yale matatizo ya nyumbani.

  Ukweli ni kwamba nimewaona wanaume na wanawake ambao hawana matatizo yoyote ndani ya ndoa zao lakini wana hivyo vipozeo vyao na wakati mwingine unamuona mwanaume ana mke mzuri kama malaika lakini kachukua mwanamke wa hovyo hovyo tu na wakati mwingine wengine hutembea hata na wafanyakazi wao wa ndani.

  Sasa hivi katika ndoa nchi za magharibi wazungu wengi wanakubali wake zao na waume zao wawe na boyfriend na girlfriend ambaye akisikia kukutana naye basi humtaarifu mwenziye na anaweza hata kulala nje na huyo rafiki yake. Weusi katika nchi hizo nao taratibu wanaanza kuiga tabia hii. Kikubwa kinachowafanya wanandoa waruhusu tabia hii ni kwamba wengi wao wanaona haiwezekani ukafanya mapenzi na mwanaume/mwanamke mmoja kwa miaka chungu nzima ambayo upo kwenye ndoa hivyo badala ya mtu kujificha ili kutembea nje wao wameona umuhimu wa kuliruhusu ndani ya ndoa zao.

  Hivyo vipozeo ni hadithi tu, lakini ukweli ni kwamba kama wanyama binadamu tunapenda kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja. Wapo wanaojizuia na matamanio hayo ya kuwa na mwanaume au mwanamke nje ya ndoa lakini ni wachache sana.
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Pasco,
  Umesema kipoozeo siyo suluhisho.Kwako wewe suluhu ya kudumu itapatikana through spiritual union ( ambayo nadhani hujafafanua vya kutosha na labda hapa si mahali pake kujadili)
  Umesema hata hivyo kuwa dawa ya kudumu ni kujua chanzo kilichozaa kutendwa.Unadhani watu wanatendana kwa vile hawajui chanzo au kwa vile wanabaki na jeraha linalopwita ha hivyo kuhitaji tiba?
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hivi? Unadhani mapenzi ya hawa wawili ni kulipiza kisasi au ni hali iliyoachiwa itokee kwa vile sasa kuna sababu? Ninachotaka kusema ni kuwa pengine kama huyo mwanamke hakuwa frustrated pengine asingemkubali huyo bwana.Sijui lakini...
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  BAK,
  Ulichoonyesha hapa ni kuwa binadamu wana unafiki sana inapofikia mahusiano.Kila mtu anataka kuonekana malaika mbele za macho ya watu lakini deep down in their souls wana udhaifu na mapungufu mengi na laiti kama wangekuwa wakweli!
  Kweli kimaadili na kiimani watu wanategemewa ku behave in a certain manner ( to be monogamous or stick to those that one is legally married to kama ni recognised polygamy)
  Sasa unadhani hali hii ya unafiki inasaidia kushikilia jamii/wanandoa pamoja?
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,874
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Jamani kwenye huu mjadala tusizungumzie tu wale wanaotembea nje kwa kisingizio cha matatizo nyumbani bali pia tujadili wale ambao hutembea nje pamoja na kuwa ndani ya ndoa zao kila kitu ni shwari kabisa. Je, kulikoni hawa ambao ndoa zao hazina kasoro yoyote bado wanatembea nje?
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,874
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Haisadii kushikilia jamii/wanandoa pamoja lakini kumbuka kuna ile methali inayosema ukimchunguza kuku sana hutamla. Hivyo mambo ya kupekuanapekuana ndani ya ndoa yakizidi basi mwisho wake huwa si mzuri. Nimeshawahi kuwaona ndigu wa mwanamke wa Baba mmoja na Mama mmoja kuwajia juu marafiki wa dada yao waliotaka kumwambia kwamba njemba ina 'kipozeo' nje na kunapata huduma nzuri sana toka kwa njemba yule. Maana hata nguo na viatu alikuwa ananunua sare sare tofauti ilikuwa ni rangi tu. Na ndani ya ndoa ile kulikuwa hakuna matatizo yoyote na yule mama kwenye ndoa alikuwa kajaliwa katika dept ya uzuri.

  Na wale ndugu hawakutaka kumweka kiti moto shemeji yao kwa kumanga manga nje ya ndoa. Kwa maana nyingine waliruhusu Shemeji yao kupuyanga nje ya ndoa kwa sababu tu alikuwa anamtunza vizuri dada yao.
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nadhani hapa BAK umegusia another dimension... "mambo ya kuambiwa"..kuna watu wanadhani ni vema kumtonya mtu pale Wanapojua habari za mhusika( nadhani mmenielewa hapa).
  Je, ni vizuri wewe kuwa chanzo cha habari katika ndoa za watu? na je, wewe kama mwana ndoa utapenda kuletwa habari kumhusu mwenzi wako?
  Binafsi sitapenda kuwa chanzo cha habari maana sitakuwa nawasaidia wana ndoa bali kuwafarakanisha.Vile vile sitapenda kuambiwa maana nisichokijua hakitanidhuru!
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hao "wamepitikiwa tu" wanafaa kusamehewa kwa udhaifu walokuwa nao...
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,874
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Ya ngoswe mwachie ngoswe! Si vizuri hata kidogo kupeleka habari kwa rafiki yako kwamba mume/mke wake anatembea nje. Wengine watasema urafiki wako ni wa unafiki maana humtakii mema rafiki yako pamoja na kuwa unajua fika mke/mume wake anatembea nje.

  Hili la wanandugu kukataa dada yao kuambiwa kuhusu extra activities za shemeji yao lilikuja baada ya marafiki wa dada zao ambao walikuwa wanajua fika kuhusu mambo ya shemeji yao. Marafiki waliwaweka kiti moto wana ndugu wale na kuwauliza kulikoni hawamwambii dada yenu kuhusu shughuli za shemeji yao pamoja na kuwa wanazijua? Wakasema wanazijua siku nyingi lakini shemeji yao ni provider mzuri kwa dada yao na wana 'maisha mazuri' hivyo kamwe marafiki wasiingilie ndoa ya dada yao. Kwa maana nyingine wao pamoja na kujua hali hiyo lakini kutokana na shemeji yao kuwa 'good provider' hawakuona umuhimu wa kutia neno ili 'kuitia dosari' ndoa hiyo.
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  nilikuwa sifikirii hata siku 1 kutoka nje ya ndoa yangu, ni binadamu kamili, mwanaume miezi kama 6 hivi hana time na mimi, kashapata hivyo vipoozeo, sasa mtu ufanyaje jamani, nilikuwa siwafikirii hao vipoozeo but hapo hapo mr akawa hanitendei haki, mimi alinifundisha yeye haya mambo, haaa wanaume haedache jamani.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,616
  Trophy Points: 280
  Mama WOS, its true kuifikia hiyo spiritual union, kazi kidogo lazima ifanyike na hapa si mahali pake. Inahusisha human dynamism, meditation na timing.
  Kutibu chanzo cha mapoozea ni kuzuia hitaji la mapoozeo lisitokee kwakutibu mapema dalili za penzi linalotaka kuchuja hivyo prevention is better than cure.
  Kuna wanaume aina 3.
  Ya kwanza ni wale genuine lovers, wenye mapenzi ya kweli na ya dhati, ukimpata huyu unauhakika you are the one and only. Huyu atakueleza kula anachotaka na uamuzi wa kukuchagua wewe ni kwa sababu ni wewe tuu.huyu hawezi kukutenda vinginevyo uyakoroge mwenyewe. Hawa ndio wale waonaosemwa na wakati mwingine hata kuchekwa eti mkewe kamshika kweli kweli.
  Aina ya pili ya waume ni wale ambao wapo wapo tuu. Hufikia uamuzi wa kuoa kwa sababu muda umefika. Hukuchagua wewe kwa sababu ni mwanamke ama kabila moja, ama mmotoka kijiji kimoja, ama mlisoma wote, ama mnaishi majirani ama mnafanya kazi ofisi moja. Ndoa hizi zinaitwa marriage of convenience.
  Yaani hakuna vitu vya moyoni. Ndoa hizi hudumu lakini not on the basis of love. Hivyo viissue vidogo vidogo tuu ugomvi mkubwa na hatimaye mmoja kwenda nje. Kutendwa.
  Aina ya tatu ni Mwanaume wa Kiafrika. Huyu ni type ambaye hata apendwe vipi, mke mmoja hatoshi. Huyu utamgundua hata kabla ya ndoa, alikuwa na msururu wa watangulizi ila akakuthibitishia wewe ndio wamwisho.
  Huyu lazima atakutenda tuu hata kama hakuna tatizo lolote ndani. Huyu ni tabia, wala hajiulizi mara mbilimbili na ukimgundua atakuomba msamaha wa mdomoni lakini moyoni hajuti na ataendelea na tabia hiyo baada ya muda mfupi. Hawa ndio wazee wa nyumba ndogo.na hata ukifikia mahali ukakubali tuko wawili, ujue kuna siku hayuko kwako wala kwake bali kwa mwingine kabisa maana hii ni tabia. Wanaume hawa ndio haswa wanahitaji kushikwa na ikibidi kuwaingiza kwenye huo muungano wa spiritual love.
  Wengine wetu wenye tabia hii msitulaumu bure, kama siye Wasukuma ni damu moto!. 'Rigwaride ra mara 3 kwa siku kama dozi, siku 7 kwa wiki utaweza'?. Badala ya kuwa starehe, inageuka karaha. Wale mama zetu zamani ni mke mwenyewe ndie anatafuta wasaidizi 'Rijamaa risije rikamuua'.
  Wasukuma wa siku hizi nguvu hizo hatuna bali tumebakiza hii tabia ya wanawake wengi, mind well, it has nothing to do with love. Kupenda tunapenda sana tuu tatizo huwezi kuwa peke yako. Dawa ni Spiritual Love only.
   
Loading...