Je, Kikwete ni mdini?


kwa ukweli watu kama wewe wananikera sana,tunajua umetumwa lakini wewe na waliokutuma iko siku mambo haya yatawatokea puwani.upuuzi mtupu jamani hivi ninyi watu flani mnaotaka kumsafisha JK mtafanya hivyo mpaka mbinguni?mbona mengine hamyasemi?au mnataka tuanze kumwaga kila kitu hapa itakuwa haibu.

BUT FRIEND TIME IS KNOCKING ON THE DOOR..........
 
Tuache udini watanzania tuna ishi kwa raha lakini kwa nini suala hili liibuke wakati huu kwani 2005-2010 JK si yulyule
 
Mbona huongei chuo cha Tanesco MORO KUWA CHUO CHA WAISLAM, Hujagusia shule kama SONGEA BOYS, SANGU secondary, Tabora Boys kama zilikuwa za catholic, na kwa taarifa yako NHC nyingi ni za wahindi nenda uendako miji mingi mikubwa ya tanzania ilijengwa na wahindi na ndio wengi walionyan'anywa nyumba wala sio waislam, Old Moshi ilikuwa ya wahindi leo ya serikali hausemi, Makamba mwislam aliwahi kusema wakati wenzetu wakristo wanakwenda shuleni kupata elimu dunia sisi waslam tulikuwa tunakwenda madrasa.

Idadi ya mawaziri wakristo inatakiwa hivyo au ilitakiwa kuwa kubwa zaidi ya hapo nafikiri wajua idadi ya wakristo na waislam ipo tofauti ukibisha hamnazo,

Mimi nimekuwa nikifuatilia hoja za waislam kuhusu udini na mengineyo nimeona mara nyingi sio tatizo lao bali wanamatatizo ya inferiority complex ambayo inasababishwa na maustaaadh wasokuwa na data bali kupandikiza chuki na mifarakano katika jamii kama wewe. Na uende uendako JF haitafungiwa kama sababu ni dini
 

umesahau Pugu secondary -catholic, minaki sec-anglica, muhimbili hosp-anglican
 
Zanzibar vipi?unasema mnaweza mbona wasionyeshe mfano kuwa hiyo dini unayosema huku imekandamizwa???????????Naomba masuala ya dini tuwaachie hao wanaofaidi kwa kutujaza ujinga wa dini.Tuongelee maendeleo yetu na mustakabali wa Taifa.Je wao walipeleka hoja kwa serikali wakanyimwa hiyo ruzuku???Kanisa lina hospitali KCMC,Bugando,vyuo St.August,Tumaini etc ambavyo hakuna ubaguzi wa huduma.Ni kwa nini basi watumie sadaka za wakristo tu?Ndio maana wanaiomba serikali na yenyewe ichangie au basi leteni sadaka za msikitini nazo zitumike kwenye maendeleo ya jamii,na sio kulalamika kuwa wakristo wanapendelewa.Lete data na hoja,tusipeane nafasi kutokana na dini.Namkumbuka jamaa mmoja tukiwa A Level alijikita sana kwenye dini akapata 0,wenzake waliojikita kwenye masomo wakafaulu Je ikitokea nafsi ya uongozi tumpe aliyesoma akapata div.1 au anayekuja na hoja ya udini huku alishindwa akapata 0.Amua mwenyewe sokomoko.
 

Ushahidi wa malengo haya unaonekana wazi kwenye vitabu vya Jan P van Bergen Development and Religion in Tanzania: Sociological soundings on Christian participation in rural transformation, John C. Sivalon Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, Frieder Ludwig Church & State in Tanzania: Aspects of a Changing Relationship, 1961–1994. Uchunguzi wa vitabu hivyo pamoja na vya Bwana Mohamed Said na Dkt. Hamza Njozi unaonyesha vipi Kanisa lilivyoitumiya Dola ya Tanganyika na baadaye ya Tanzania kujiimarisha ndani ya nchi kwa kuwazuwiya Waislam wasipige hatua za kimaendeleo zitakazoweza


Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru! 299
kuwapita Wakristo.
Tafauti na Waislam, wakala za kujitoleya na taasisi za Kikristo zinatowa mchango mkubwa katika huduma za kiafya na za kiilimu Tanzania. Huduma nyingi za kiafya katika sehemu za vijijini huwa zinatolewa na taasisi hizo ambazo zinapata misaada kutoka kwa wafadhili wa taasisi za kimataifa. Inakuwa ni vigumu kwa Waislam kupata misaada kutoka nchi za Kiislam na taasisi za kimataifa. Upande mmoja wameelemewa na vita vya kipropaganda dhidi ya Waarabu Waislam na utumwa wa Waislam ambavyo vinawaghadhibisha na kuwakimbiza wafadhili Waislam na taasisi za Kiislam. Au zitatafutwa taasisi za Waislam ambazo zimejaa ufisadi na kuwafanya wafadhili Waislam na taasisi za Kiislam zikataye kuwasaidiya Waislam kwa kupitiya taasisi hizo. Baina ya mifarakano yote hiyo Wakristo wanaongeza na wanaongezewa nguvu na waumini wenzao kutoka nchi za Magharibi.
Tarehe 21 Februari mwaka 1992, Baraza la Kikristo Tanzania na Baraza la Maaskofu Katoliki walitiya saini Mkataba wa Maridhiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliyoandaliwa na Profesa, Dokta, C. R. Mahalu wa Kitengo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kutiwa saini na Edward Ngoyai Lowassa kwa niaba ya Serikali, Elinaza Sendoro kwa niaba ya Baraza la Kikristo Tanzania, na Josephat Lebulu, kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki.
Mkataba wa Maridhiano una lengo zuri la kuendeleza huduma za afya na ilimu katika jamii na unaikalifisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania:
…itajitahidi kujumuisha misaada ya kifedha kwa ajili ya huduma za jamii zinazomilikiwa na ‘Makanisa' itakapokuwa katika mazungumzo ya kuomba misaada husuusan mazungumzo yake na Jamhuri ya Kifedirali ya Ujerumani. Uwezekano kama huo uangaliwe pia itakapokuwa na mazungumzo na wafadhili wengine.22
Wakati Zanzibar ilipotaka kujiunga na shirika la Kiislam la Organization of Islamic Conference (OIC), Askofu E. Sendoro wa Mkataba wa Maridhiano alitahadharisha juu ya uamuzi wa kitendo hicho kwa kusema: "Zanzibar ikiwa ni Dola ya Kiislamu, itaendeleya kuwa sehemu ya Muungano? Bunge la Muungano litakuwa na dhamana juu ya Zanzibar au lipo kwa ajili ya Tanzania Bara?"23
Askofu Sendoro kalikozesha suala la Zanzibar kutaka kujiunga na OIC na kulifanya ni suala la Zanzibar kutaka kuwa Dola ya Kiislam. Kwani Mkataba wa Maridhiano ambao lengo lake kubwa ni kuendeleza huduma za kijamii za Kanisa katika sekta za ilimu na afya ulikuwa na lengo la kuifanya Tanzania kuwa Dola ya Kikristo? Kwa vile Mkataba wa Maridhiano ni mkataba baina ya Taasisi zisizo za kiserikali na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jee, ulipata baraka za Baraza la Wawakilishi la nchi ya Zanzibar na Bunge la Jamhuri ya Muungano au ilionekana kuwa hakuna haja ya kufanya hivyo?

From the book Kwaheri Ukolonin Karibu Uhuru page number 209 - 300
 

Kitafute kitabu Cha Haridh Ghasany kwakuwa upo nje itakuwa rahisi kukipata kisha soma kuanzia ukurasa wa 299 - 300 utaona mikakati ya ukristo kuukandamiza uslam na hata mapinduzi ya zanznibar ni kuogopa dola ya kiislam mwandishi ameelezea kwa kina na kunukuu vitabu kadha wa kadha vilivyo andikwa na wazawa pamoja na wazungu. Dont miss nadhani ukikisoma utachangia hoja kwa upeo mkubwa na hutakuwa mnafiki.

Shukran
 
hakuna anayesema kikwete ni mdini,...kikwete ni fisadi..acheni kujadili mada isiyo na faida kwa taifa,mtu yoyote asiye na uwezo wa kujenga hoja anakuja na hoja ya udini kama kikwete sasa hivi na huyo mfuasi wake:embarrassed:
 
Washindwe kabisa wote wanaotaka kutugawa kwa misingi ya dini zetu wakati kuwa Kiongozi si sababu ya kuanzishwa dini.

Najua ni njama za mafisadi kutaka kuendelea kukaa madarakani huku wakiendelea kuitafuna nchi yetu.

Mimi najua kati yangu mimi na wewe hakuna udini ila watu wachache wakiwemo mafisadi ndo wanaitumia udini ili kutufunga macho na kutugawa,
Amkeni muwe macho..............
 
Kikwete mdini sana tu...baraza lake limejaa waislamu 33 na wakristo 17..damn! isitoshe sipendi kuona hao 17 kwanza hawana uwezo, hawajasoma, hawafai kabisa...wakristo wanachapa kazi bana sio mchezo...angalia ngeleja..umeme hakuna mgao, angalia sophia simba..hana mchezo, angalia mkuchika hana utani...JK ondoa hao 17 weka watu waliosoma achana na madrasasultul...hawana elimu...

JK anawaogopa wakristo period!
 
kigezo cha baraza la mawaziri nadhani si jibu sahihi la hili swali/hoja ni kwamba anakandamiza dini au thebu gani na kupendelea lipi lakini nadhani serikali haina dini
 
 
 

tatizo swala la udini kalianzisha rais(kama kweli ni rais halali),should anything destructive happen to this country as far as religion is concerned,JK must be held responsible,he has planted a very bad seed,its sad but i must admit i begin to hate him for that:redfaces:
 

Ulitakiwa kumpongeza ..wewe mwenyewe mdini
 
This post from Sokomoko is one of the post that need to be discussed and im very happy for bringing this matter here coz majority of us here in JF tunaeneza propaganda za ajabuajabu kuhusu Kikwete na Uislam.

Big up sokomoko
 
 
 
Kwa hiyo hata kama hao waislam wamefeli utawapa tu nafasi ya kusoma na walopass unawaacha??u would be the worst president since the creation of the planet earth
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…