Je, Kikwete ni mdini?

Je, Kikwete ni mdini?

Mods, na wana JF,

Haitakuwa busara kwa thread hii kuipeleka sehemu ya dini, inajulikana sehemu hiyo haifikiwi na watu wengi hapa JF ikiwa mimi mmoja wapo.

Ni matumaini yangu kuweza kuiaccess hii thread na kuona mijadala ikichangiwa ili kuweza kujua ukweli.

Sitegemei kuwa JF/Mods wapo kwa ajili ya kuchochea chuki dhidi ya Serikali iliyopo madarakani kwani kama itakuwa ni hivyo basi wanafanya jambo la hatari sana linaloweza kutugharimu. Tumeona ile thread ya OIC ikiachiwa kuchangiwa na kila mtu na mwenye kila tusi dhidi ya dini ya kiisamu na kejeli akiachiwa kwa marefu na mapana. Kwahiyo sioni sababu ya hii thread ya kisiasa zaidi kutupiwa huko kusikojulikana.

Mwisho napenda kutoa angalizo:

Sio haki kuhamisha thread ya mtu na kuipeleka sehemu asiyokuwa na access nayo. Hapa JF ni sehemu ya kutoa mawazo na kila mmoja aheshimiwe mawazo yake na sio kufungwa na kutupwa kapuni.

Kuna tetesi Zimeenea mtaani kuwa baada ya JK kuingia madarakani aligomea ruzuku iliyokuwa ikitolewa na Serikali kuendesha makanisa pamoja na taasisi zinazoendeshwa na makanisa katoliki nchini kama shule, hospitali na vyuo. "The Government shall provide financial assistance to Church institutions and shall seek financial assistance to Church run social services in its bilateral negotiations with foreign governments"

source
:The Memorandum of Understanding between the Government of the United Republic of Tanzania and the Tanzania Episcopal Council (TEC) and the Christian Council of Tanzania-page 3 (attached herewith)

Nasikia JK aliwaambia kuwa nchi hii haina dini na itakuwa ubaguzi kuwapa ruzuku watu wa dini moja na kuwaacha wa dini nyinginezo akatolea mfano kuna waislam, wabudda, masingasinga, wahindu na wasiokuwa na dini je hao hawana haki ya kupewa ruzuku? na serikali ikitoa ruzuku kwa hawa wote itawezaje kujiendesha? Basi bora mkose wote. Hapo naona JK aliona mbali sana ila hakujua kama anajiharibia yeye na chama chake. Na ndio maana kwa kutumia mlango wa nyuma kuna chama kikasimamisha watumishi wa Mungu kwa wingi na kufanikiwa kupenya kila pembe ya Tanzania. Inasemekana Kanisa liliplay part kubwa kwa mafanikio ya chama fulani. Na hizo zilikuwa ni hasira za watumishi wa kanisa.

KUNA TETESI KUWA WAFUATILIAJI WA MAMBO WAMEITHIBITISHIA SERIKALI UBADHIRIFU MKUBWA WA RUZUKU ILIYOKUWA INATOLEWA NA SERIKALI SAMBAMBA NA MISAMAHA YA KODI. MISAMAHA HII YA KODI NI ILE YA UAGIZWAJI MAGARI NA VITU MBALIMBALI KUPITIA TRUSTEES ZA MAKANISA. NA TANGU KUANZA KUBANWA KUMEKUWA NA UAIGIZAJI WA VITU MDOGO TOFAUTI NA HAPO MWANZO, MAANA INASEMEKANA WAJANJA WALIKUWA WANATUMIA MWANYA HUO KUJINUFAISHA.

Ukiunganisha picha itaona hapo ndio chanzo hasa cha timbwili hili mnaloliona leo lililo vikwa ngozi ya vyama vya siasa ( upinzani ). Hapo awali Wakristo na CCM walikuwa chanda na pete. Ilikuwa ni kosa la jinai kwa mkristo mwenye imani kuwa upinzani ndio maana hata viongozi wao wengi mwaka 2005 walisema JK "chaguo la Mungu"

Leo hii ukitia pua tu JF na maeneo mengi kwenye mitandao na mitaani utakutana na shutuma kuwa JK ni Mdini, lakini hawatoi facts za udini wake.

Je, JK ni mdini?

Orodha ya Baraza la Mawaziri na Manaibu wa Wizara 26 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2010 - 2015

  1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora - Mathias Chikawe (Mkristo)
  2. Waziri wa Nchi, Oisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu - Steven Wassira (Mkristo)
  3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma - Hawa Ghasia
  4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Muungano - Samia Suluhu Hassan
  5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Mazingira - Dk. Terezya Luoga-Hovisa (Mkristo)
  6. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge - William Lukuvi (Mkristo)
  7. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji - Mary Nagu (Mkristo)
  8. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - George Mkuchika (Mkristo)
  9. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (i) - Aggrey Mwanri (Mkristo)
  10. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ii)Kassim Majaliwa -
  11. Waziri Wizara ya Fedha - Mustapha Mkullo
  12. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (i) - Gregory Teu (Mkristo)
  13. Naibu Waziri Wizara ya Fedha (ii) - Pereira Ame Silima
  14. Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Shamsi Vuai Nahodha
  15. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Balozi Khamis Suedi Kagasheki
  16. Waziri wa Katiba na Sheria - Selina Kombani (Mkristo)
  17. Waziri Wizara ya Mambo ya Nje - Bernard Membe (Mkristo)
  18. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje - Mahadhi Juma Mahadhi
  19. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi
  20. Waziri Wizara yaMaendeleo ya Mifungo - Dk. Mathayo David Mathayo (Mkristo)
  21. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Mifungo - Benedict Ole Nangoro (Mkristo)
  22. Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia - Profesa Makame Mnyaa M'barawa
  23. Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi ya Teknolojia - Charles Kitwanga(almaaruf Mawe Matatu) (Mkristo)
  24. Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Profesa Anna Kajumulo-Tibaijuka (Mkristo)
  25. Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Goodluck Ole Medeye (Mkristo)
  26. Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii - Ezekiel Maige (Mkristo)
  27. Waziri Wizara ya Nishati na Madini - William Mghanga Ngeleja (Mkristo)
  28. Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini - Adam Kighoma Ali Malima
  29. Waziri Wizara ya wa Ujenzi (Barabara na Viwanja vya Ndege) - Dk. John Pombe Magufuli (Mkristo)
  30. Naibu Waziri Waziri Wizara ya wa Ujenzi - Dk. Harrison Mwakyembe (Mkristo)
  31. Waziri Wizara ya Uchukuzi - (Reli, Bandari, Usafiri wa Majini) - Omary Nundu
  32. Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi - Athuman Mfutakamba
  33. Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara -Dk. Cyril Chami (Mkristo)
  34. Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara - Lazaro Nyalandu (Mkristo)
  35. Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Dk. Shukuru Kawambwa (Mkristo)
  36. Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi - Philipo Mulugo (Mkristo)
  37. Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dk. Haji Hussein Mpanda
  38. Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Dk. Lucy Nkya (Mkristo)
  39. Waziri Wizara ya Kazi na Ajira - Gaudensia Kabaka (Mkristo)
  40. Naibu Waziri Wizara ya Kazi na Ajira - Dk. Makongoro Mahanga (Mkristo)
  41. Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Sophia Simba
  42. Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto - Umi Ali Mwalimu
  43. Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - Emmanuel John Nchimbi (Mkristo)
  44. Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - Dk. Fenela Mukangala (Mkristo)
  45. Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki - Samuel John Sitta (Mkristo)
  46. Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki - Abdallah Juma Abdallah
  47. Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Profesa Jumanne Maghembe
  48. Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika - Christopher Chizza (Mkristo)
  49. Waziri Wizara ya Maji - Profesa Mark James Mwandosya (Mkristo)
  50. Naibu Waziri Wizara ya Maji - Gerson Lwinge (Mkristo)
Jumla yote ni 50 kati yao wakristo 32 na waislam 18.

Wakristo 64%
Waislam 36%

Ukiangalia wakuu wa mikoa na wilaya utaona wakristo ni wengi zaidi ya waislam sasa sijui na sifahamu huo udini wa JK upo wapi???

Mwenye data tafadhali azilete jamvini.

Kuna habari za hivi punde ni kuwa kuna makampuni zaidi ya 80 ya clearing and forwarding yamefungiwa kwa sababu mbalimbali kubwa hasa ubabu mashi. Inajulikana kwenye sekta hii watu wa kutoka mkoa fulani wameishikilia kwa asilimia zaidi ya 80. Inasemekana sifa ya watu wanaotoka huko ni ujanja mwingi na ni wakwepaji wakubwa wa kodi na walitumia vizuri sana nafasi ya kuwa na udugu kuanzia uwaziri mpaka kamishna wakati wa Che Nkapa.

Ushauri kwa JK, Mkuu wee endelea kukaza buti watu walipe kodi kwa manufaa ya nchi usijali tunakusapoti kwa maana hawana shukrani Serikali imewaachia wamekula sana kodi kupitia ukwepaji na misamaha hewa lakini wamekuwa mbele kunyea kambi.

Have you ever read Plato's allegory of the cave? You are one of the prisoners in the cave!
 
A:Yes, iwapo CCM itamsimamisha Muislamu mwaka 2015 basi kuna hatari ya nchi kuvurugika, kwa sababu watu wataamini kwamba CCM ni chama cha dini fulani. Unajua mwaka 2000 CUF ilikuwa na wafuasi wengi kwa sababu Waislamu wengi waliamini kwamba CCM haiwatendei haki. Waislamu wengi waliamini ni bora kumpigia kura Lipumba (Muslim) kuliko Mkapa (Mkristo). Same issue kwa Chadema mwaka huu, ukiangalia kura nyingi walizopata Chadema ni sehemu ambazo inasemekana kuna Wakristo wengi.

kwa hiyo waliofanya hivyo walikuwa ni wadini?

B: Source nyingi ziliripoti hii issue ktk view tofauti. Lakini kuna inside source ambazo zilisema issue ilikuwa zaidi kwamba, Nyerere alisema ni fair kwa Wakristo iwapo rais atakaekuja atakuwa mkiristo. Haimake sense, watu wampigie kura mtu ambaye hana uzoefu wa kundesha nchi. Kwa nini walimpigia kura mtu ambaye hajui kuongoza nchi?

Nipe mfano wa credible source moja tu. Vinginevyo hizo ni tetesi tu kama za yule mtu aliyesema ati Kikwete alipelekewa cheki na viongozi wa kanisa na wapo wanaoamini hilo.
 
A:Yes, iwapo CCM itamsimamisha Muislamu mwaka 2015 basi kuna hatari ya nchi kuvurugika, kwa sababu watu wataamini kwamba CCM ni chama cha dini fulani.

kwa hiyo hata kama hakuna mkristu anayekubalika au kufaa, muislamu akataliwe na CCM kwa sababu ya dini yake ili kumsimamisha Mkristu hata kama Muislamu huyo anakubalika na kufaa zaidi? Una maana hata vyama vingine vya upinzani navyo visimamishe wakristu tu - CUF isimamishe mkristu vile vile?

Lakini itakuwaje kama wataamua kumsimamisha mtu asiyeamini Mungu kabisa lakini anayekubali au mganga wa kienyeji mpagani lakini anayekubalika?
 
si uliona aliyevaa kibandiko mahakamani alivyoleta sokomoko! Sasa wewe ingia na viatu msikitini kama utasalimika.
nazani utakuwa umesahua-1999 polisi waliingia na viatu mwembachai-waliolalamika walilalamika kama ilivo kawaida yao
 
kwa hiyo hata kama hakuna mkristu anayekubalika au kufaa, muislamu akataliwe na CCM kwa sababu ya dini yake ili kumsimamisha Mkristu hata kama Muislamu huyo anakubalika na kufaa zaidi? Una maana hata vyama vingine vya upinzani navyo visimamishe wakristu tu - CUF isimamishe mkristu vile vile?

Lakini itakuwaje kama wataamua kumsimamisha mtu asiyeamini Mungu kabisa lakini anayekubali au mganga wa kienyeji mpagani lakini anayekubalika?

Kama CCM itaamua kumsimamisha mtu ambaye si Mkiristo, basi utaona chuki za kidini zinazidi, na malalamiko yatazidi kuhusu Udini. Baadaye itakuwa Cancer, ambayo matokeo yake utaona matatizo kama Rwanda, Sudan, Congo, nk.

Vyama vya upinzani vipo ktk stage ya Udini, fulani,. Ukiangalia statistic za Chadema, utaona kwamba Chadema ni chama chenye Wakristo wengi, na ukiangalia statistic za CUF utaona CUF ni chama chenye Waislam wengi zaidi.

Simply, hivi vyama vya Upinzani bado havina sura ya national demographic. Bado vinashinwa kuatract WTZ tofauti tofauti.

Unajua tatizo tupo katika Development, na ukiangalia historia utaona kila nchi imepitia hii stage kabla ya kuwa Secular 100%. Nchi nyingi za Africa zinasuffer hii stage kwa sababu kila group, kabila, dini linaona linaonewa na serikali kwa sababu bado tupo na umaskini.
Hii stage tutaipita kwa amani iwapo kama society itakuwa inapata mahitaji ya muhimu kama uchumi mzuri kwa kila mkoa, elimu ya haki kwa wote, na serikali kutoa kipaumbele kwa mikoa ambayo ipo nyuma kimaendeleo.
 
Kama CCM itaamua kumsimamisha mtu ambaye si Mkiristo, basi utaona chuki za kidini zinazidi, na malalamiko yatazidi kuhusu Udini. Baadaye itakuwa Cancer, ambayo matokeo yake utaona matatizo kama Rwanda, Sudan, Congo, nk.

CCM watajuaje mtu fulani ni Mkristu ili wamsimamishe?

Je akiwepo Muislamu anayefaa na kukubalika akataliwe kwa sababu ya dini yake ili kumpa nafasi Mkristu hata kama hakubali na hana uwezo?
 
CCM watajuaje mtu fulani ni Mkristu ili wamsimamishe?

Je akiwepo Muislamu anayefaa na kukubalika akataliwe kwa sababu ya dini yake ili kumpa nafasi Mkristu hata kama hakubali na hana uwezo?

I think ni logic kumjua MTZ yupo ktk dini gani. WTZ wangi wanajua kwamba Mwinyi ni muislamu, Nyerere mkristo, Mkapa Mkiristo, JK ni muislamu, ni common sense.

Hiyo ndiyo issue niliyosema mwanzo kwamba JK aliposhinda Dodoma, inasemekana aliambiwa asubiri baadaye kwa sababu itakuwa siyo fair kwa Wakristo iwapo JK(muislamu) awe rais baada ya Mwinyi (muislamu).

Study CCM utaona kuna viongozi wanachaguliwa ili kuwa na balance ya power ktk dini. Kwa mfano, kwa nini Waziri Mkuu lazima awe Mkiristo? au IGP awe muislamu, mkuu wa majeshi wa Mkrisito? CCM wanajua issue ya Udini, ndiyo maana wanafanya hivi ili wawe na balance ya power.
 
I think ni logic kumjua MTZ yupo ktk dini gani. WTZ wangi wanajua kwamba Mwinyi ni muislamu, Nyerere mkristo, Mkapa Mkiristo, JK ni muislamu, ni common sense.

Common sense siyo common kihivyo; kwa mfano Mwinyi watu wanajua ni Muislamu kwa sababu wameona akienda kuswali, akijitambulisha hivyo n.k Nyerere watu wanajua ni Mkristu kwa sababu walimuona anaenda kanisani n.k vivyo hivyo kwa JK na Mkapa. Sasa kwa hawa Watanzania wengine tutawajuaje kuwa ni wakristu au waislamu?

a. Wakati wanaomba kazi tuwaulize kama ni Wakristu/Waislamu?

b. Tuwafuate msikitini au kanisani japo kwa mwezi mmoja?

c. Tuwaulize wakiri kanuni ya imani au shahda ili tujue wanachokiamini?

Tuweke utaratibu gani wa kumjua mtu ni muislamu au mkristu ili tuweze kufikia lile lengo la 50/50 uliloliashiria?
Hiyo ndiyo issue niliyosema mwanzo kwamba JK aliposhinda Dodoma, inasemekana aliambiwa asubiri baadaye kwa sababu itakuwa siyo fair kwa Wakristo iwapo JK(muislamu) awe rais baada ya Mwinyi (muislamu).

Study CCM utaona kuna viongozi wanachaguliwa ili kuwa na balance ya power ktk dini. Kwa mfano, kwa nini Waziri Mkuu lazima awe Mkiristo? au IGP awe muislamu, mkuu wa majeshi wa Mkrisito? CCM wanajua issue ya Udini, ndiyo maana wanafanya hivi ili wawe na balance ya power.[/QUOTE]
 
Hiyo ndiyo issue niliyosema mwanzo kwamba JK aliposhinda Dodoma, inasemekana aliambiwa asubiri baadaye kwa sababu itakuwa siyo fair kwa Wakristo iwapo JK(muislamu) awe rais baada ya Mwinyi (muislamu).

Unachosema ni kuwa muislamu mwenye uwezo na anayekubalika akataliwe kwa sababu ya dini yake ili apewe mkristu asiyekubalika na asiye na uwezo mwaka 2015? Kwamba dini ndiyo iwe sababu kuu ya kuamua nani asimamishwe na nani asisimamishwe. Nimekuelewa.

Study CCM utaona kuna viongozi wanachaguliwa ili kuwa na balance ya power ktk dini. Kwa mfano, kwa nini Waziri Mkuu lazima awe Mkiristo? au IGP awe muislamu, mkuu wa majeshi wa Mkrisito? CCM wanajua issue ya Udini, ndiyo maana wanafanya hivi ili wawe na balance ya power.

Sijui kama umesoma nafasi zote ulizozisema zote zimewahi kushikwa na wakristu na waislamu;

Lakini vipi kuhusu Wahindu na wapagani wao hawana haki ya kuongoza nchi yao?
 
Unachosema ni kuwa muislamu mwenye uwezo na anayekubalika akataliwe kwa sababu ya dini yake ili apewe mkristu asiyekubalika na asiye na uwezo mwaka 2015? Kwamba dini ndiyo iwe sababu kuu ya kuamua nani asimamishwe na nani asisimamishwe. Nimekuelewa.

Sijui kama umesoma nafasi zote ulizozisema zote zimewahi kushikwa na wakristu na waislamu;

Lakini vipi kuhusu Wahindu na wapagani wao hawana haki ya kuongoza nchi yao?

Dini ambazo ni majority ni Waislamu na Wakristo, Wahindi na Wapagani ni minority. Kwa hiyo wapewe nafasi chache kutokana na population yao.
Hile ya common sense nilifupisha kwa sababu nilijua utanielewa.

Kazi za serikali zitolewe kwa kuzingatia vigezo vyote, elimu, uzoefu, na dini yako. Huwezi kuwapa kazi watu wa dini moja halafu ukasema, kwamba watu wa dini fulani hawana mtu anaequalify. Kwa mfano nchi zilizoendelea wanauliza una Race gani wakati unaapply form yoyote ili wacontroll haki kwa kila race.
Hata Marekani wana vigezo ambavyo wanatumia kucontroll visa za watu wanaokwenda Marekani kwa misingi ya haki kwa kila nchi, race nk. Sasa kama wangekuwa wanaangalia vigezo vya kualification tu peke yake basi kuna watu wa nchi nyingine ambazo zipo nyuma kimaendeleo wangeisikia Marekani kwenye bomba tu.

Sasa kama wenzetu wanatumia hivi vigezo kwa kutaka kuleta haki, kwanini TZ, na Africa hatufanyi? Vita vya kila siku kwa sababu hatuwapi haki watu fulani, kwa kuogopa kuitwa Wadini, Wabaguzi, nk. Angalia vita vya Sudan, Rwanda, na Congo, utaona ni lazima tubadilike kabla ya Cancer kubwa zaidi TZ.
 
Sokomoko umesahau na sofia simba nae ni mkristo...the percentage goes to???????
 
Mnaifanya hii forum kuwa forum ya chedema kumbe unafiki mtupu, mnatak iwe forum ya kikrosto shiiiiiit gadem...kama kweli manaakili na hoja mjibuni sokomoko
 
Mnaifanya hii forum kuwa forum ya chadema kumbe unafiki mtupu, mnataka iwe forum ya wakristo shiiiiiit gadem...kama kweli mnaakili na hoja mjibuni sokomoko

UPPUZI MTUPU
 
Dini ambazo ni majority ni Waislamu na Wakristo, Wahindi na Wapagani ni minority. Kwa hiyo wapewe nafasi chache kutokana na population yao.
Hile ya common sense nilifupisha kwa sababu nilijua utanielewa.

Kazi za serikali zitolewe kwa kuzingatia vigezo vyote, elimu, uzoefu, na dini yako. Huwezi kuwapa kazi watu wa dini moja halafu ukasema, kwamba watu wa dini fulani hawana mtu anaequalify. Kwa mfano nchi zilizoendelea wanauliza una Race gani wakati unaapply form yoyote ili wacontroll haki kwa kila race.
Hata Marekani wana vigezo ambavyo wanatumia kucontroll visa za watu wanaokwenda Marekani kwa misingi ya haki kwa kila nchi, race nk. Sasa kama wangekuwa wanaangalia vigezo vya kualification tu peke yake basi kuna watu wa nchi nyingine ambazo zipo nyuma kimaendeleo wangeisikia Marekani kwenye bomba tu.

Sasa kama wenzetu wanatumia hivi vigezo kwa kutaka kuleta haki, kwanini TZ, na Africa hatufanyi? Vita vya kila siku kwa sababu hatuwapi haki watu fulani, kwa kuogopa kuitwa Wadini, Wabaguzi, nk. Angalia vita vya Sudan, Rwanda, na Congo, utaona ni lazima tubadilike kabla ya Cancer kubwa zaidi TZ.

nimekupata vizuri sasa tukija kwenye hili la dini ni lazima tuangalie madhehebu ya dini ili kuyawakilisha vizuri au mtu akiwa ni mkristu basi ni mkristu tu; kwa mfano, tuhakikishe Wakatoliki, Walutheri na Wapentekoste nao wanakuwa represented vizuri kama vile Sunni, Shia, Answar?
 
Will see ikiwa OIC imewekwa kina mtu analijadili na nisuala linalohusu uislam aliepost hakufungiwa basi siku za JF zinahesabika mjue kuna watu wengi wanaifatilia na kujua ukweli na sitatofautisha JF na Ze utamu.

ukweli ni kuwa anapendelea wakiristo.
kwani muhula wake wa kwanza wakiristo walilalamika sana wapewe nafasi serikalini na alimteua mkiristo mmoja kwenye nafasi ya ubunge.
na huyo aliyeteuliwa alisema kuwa nafasi yake bungeni ni ya jamii sawasawa na kuwawakilisha wakiristo. kwani dini lake hilo pia ni la jamii na wakaomba nafasi nyingi zaidi.

mbona hakuchagua mbunge muislam. lakini viongozi hao hao wa kiislam wana walazimisha viongozi wa dini ya kuislam wawatangazie waislam kuwa wao wasijishuhulishe na siasa.
wakati hakuna muislam anayejishuhulisha na siasa ikiwa kuna waislam ambao jk anawachagua basi hao ni waislam majina tu lakini hawana imani na dini ispokuwa na matumbo yao.
na pia waislam hao kutoa rushwa kwa viongozi wa dini kufumbia maovu yoyote na kunyamaza kimya.
uislam uaneleza wazi kama kutakuwa kuna ubaya basi ukatazwe na uondolewe na kama hauwezekani basi na uchukiwe.
kutokana na maneno hayo ni kuonyesha wazi kuwa mambo mabaya wanayofanya viongozi wa serekali na ccm yake ni machukizo ya kuchikiwa na waislam na viongozi wake walio waislam.
kikwete udini wake upo kwa ukiristo kwani yeye ni mwenye kauli ya mwisho hakuna hata moja alilolifanya la upendeleo kwa waislam ila kwa wakiristo na wakiristo kuwa na kauli ndani ya bunge na serikali wao ni watu waliowekwa kwa maslahi yao si ya uislam wala ya waislam

nafikiria wenye macho wanaona.
wanapokwenda misikitini viongozi hao wa serikali au wa ccm huwaamrisha viongozi wa dini za kiislam kuwa wasijitie kwenye siasa yaani wayafungie macho mambo yanayofanywa na wanasiasa na serikali yake hata kama watafanya mabaya. na viongozi wa kiislam hawaombi vyeo kwenye ccm wala serikali isipokuwa wao hukataza mabaya tu, na kuwaonya waislam.
hii inakuja sawasawa na historia ya yesu kwani misikitini kulikuwamo watu ambao wanafata viongozi wa nchi na kuwakufurushiwa waislam ndio ccm na serikali yake kwa sasa inawakufurushisha waislam na kuwakataza wasizungumzie mabaya wao waswali tu.

lakini wakiristo wao kila siku kelele tuongozeeni vyeo serikalini na kwenye ccm na mabungeni na hizi habari zipo wazi na jk anafanya hivyo.
udini wa jk na waislam wenzakee ni kwa wakiristo na kuwafumba waislam wasizungumzie mabaya ili wapotee wende njia mbaya ya kupotea
huu ndio ukweli.
tukumbukeni enzi za ali hasani mwinyi. alipokuwa anangia urais aliingia na imani zabiti ya kiislam lakini baadaye naye alielekea muelekeo wa rafiki zake na hatimayake tuliiona.
nafikiria umeridhika sasa jibu unalolitaka ni tofauti hili ndio sahihi
 
Back
Top Bottom