Je, Kikwete ni mdini?



Unapopinga kwamba TZ hakuna Udini ni kubisha ukweli halisi uliokuwepo TZ. Udini/Mdini ni yule mtu anaeajiri watu, anawabagua watu, anawatukana watu, kwa sababu ya dini zao nk, (Biases). Sasa tuangalie statistic za hizi biases kama kweli zipo TZ.
Tuangalie ktk serikali yetu je ina diversity yoyote? Mfano nchi kama Marekani ina Affirmative action ili kuwapa na nafasi minority ktk serikali, mashuleni.
Sasa ukiangalia vitu kama hivyo basi utaona kwamba serikali yetu haina diversity yoyote ktk serikali; kwa sababu kuna watu wanapeana kazi kwa kujuana na nk. Njia ambayo itaweza kuisadia TZ ktk balaa la vita vya kidini ni kuandaa sheria maalum ya kuwapa watu ruhusa ya kuangalia mfumo mzima wa diversity za kidini ktk kazi serikalini, biashara nk.

Wewe angalia hii Jamii Forum, wanasema kwamba inaendeshwa as secular, lakini inapromote Injili- sasa ni kweli hii JF inaendeshwa as secular? Sasa kama secular mbona kuna Injili tu peke yake? Hivyo ndivyo vitu ambavyo vipo ktk serikali yetu. Serikali inasema haina Udini, lakini action inazofanya zipo ktk biases za kidini.
 
kuna watu wana akili finyu sana kiakili kidogo alichonacho ndo kinaishia habari za dini. JK ni mwelewa mwacheni msimweke kwenye vitu vya kijinga.
hivi mtu ukikaaa na dini yako mwenyewe na mwingine akae nayo ya kwake bila kutafuta hoja za kijinga kwani naamini hakuna dini inafundisha muumini afanye dharau kwa dini nyingine, abague dini nyingine n.k ila watu wachache wa mawazo finyu na inferiority ndiyo huanzisha UDINI
 

Mkuu udni ni kuangalia katika kila nafasi kawekwa mtu wa dini gani. Hauwezi kuprove sehemu fulani kuna udini kwa kuangalia wangapi wa dini fulani wameajiriwa. You must go deeper than that. Kama ukiangalia tu nani ana dini gani kwenye ofisi fulani basi wewe una taka mfumo wa kuajiri unaozingatia dini kwa maana mwajiri aweke kupao mbele uwiano wa dini na siyo sifa. Toa ushahidi kwa sehemu fulani mtu wa dini fulani alikuwa na vigezo zaidi ya mtu wa dini fulani lakini bado haku chaguliwa. You can't just say ofisi kumejaa watu wa dini fulani then ukasema kuna udini no way.

Marekani unayo itolea mfano wa affirmative action una changanya watu. Affirmative action haipo tena lakini hiyo ilipo kuwepo ni kwa ajili ya minorities kama ulivyo sema. Je Waislamu ni minority Tanzania? Je Wakristo ni minorty Tanzania? Kumbuka affirmative action iliwekwa kwa sababu ya weusi ambao kwa population ya Marekani walikua less than 12%. ya total population. Waislamu wako wangapi? Wakristo wako wangapi? Je katika hizo ofisi mbona Wapagani, Wahindu, Singa Singa etc hawa hoji? Mbona hao hamuwatetea? Na kwa taarifa yako sasa hivi Marekani hamna affirmative action kuna equal opportunity kwa hiyo una weza kwenda sehemu kumejaa weupe tupu au sehemu kumejaa weusi tupu. Hawaangalii rangi gani ina watu wangapi sehemu fulani.

Kuhusu diversity nawe sasa inaonyesha upeo mdogo wa kufikiria. Tuna taka a merit based system wewe una taka proportionality system which is what diversity is. Sasa kwa hiyo mkuu una taka kwenye ofisi waangalia Waislamu/Wakristo wapo wangapi. Kisha waangalia makabila mangapi yame wakilishwa seti? Mbona wanawake ni more than 50% Tanzania ila hakuna anaye hoji kwamba kwenye ofisi nyingi wanawake wana kuwa less than 30% kuanzia Bungeni, baraza la mawaziri, ofisi za umma mpaka ofisi binafis. Kwa hiyo wanawake nao wadai "diveristy"?


Haya njoo kivingine tuendeleze mjadala. Tutaenda hatua kwa hatua.
 


Nimekutolea mifano yote ili uelewe jinsi serikali inavyotakiwa iendeshwe. By the way, Affirmative action bado inaendelea Marekani.
Vigezo vya kuwa na elimu ya juu peke yake, visiwe chanzo cha kumchagua mtu awe kiongozi peke yake. TZ inamchanganyiko wa dini tofauti, lakini kuna majority ambayo ni Wakristo na Waislamu, na kuna ethnicities kama Singa Singa, Hindu, Wapagani ni minority ktk nchi yetu ambao kama tungekuwa na diversity ktk nchi yetu basi hizi minority zingebenefit zaidi. Suala la Wanawake TZ lipo zaidi kwenye our traditional aspects.

Kwenye suala la dini.TZ inaweza kuanzisha mfumo maalum serikalini ambao kila mtu akiajiriwa inabidi aeleze dini yake ili kuweka equal opportunity kwa kila dini. Nchi kama Marekani wanatumia mfumo wa race kumuuliza mtu anapotaka kazi, immigration process, nk.
 
Lakini kwenye hili hapa kuanzia mwanzo swali gumu ni Je Kikwete anaweza kuwa ni Mdini kwa kuangalia tu wateuliwa wake walivyo? Je tunaweza kumhumu Kikwete kuwa ni mdini kwa kuangalia kilia akiteua waislamu watatu bila kuweka jina la Mkristu basi tupige kelele ni udini? (of course watakaofanya ni wakristu) na pale atakapoteua watu wenye majina ya kikristu tu basi waislamu waanze kulia "udini"? Huu ni udini gani wa kijinga namna hii?
 

Ndiyo maana ni muhimu kwa viongozi wetu kuliangalia suala la udini kuwa ni muhimu kama tunataka nchi yetu isiwe kama Lebanon, Sudan, India-Pakistan, Rwanda, Congo nk. Moja ya matatizo makubwa yanoyoikumba dunia ni vita vya wenyewe kwa wenyewe, na vita vyote vinavyotokea ni kwa sababu ya biases fulani au ignorance fulani inayotolewa na viongozi.
 

Mkuu Marekani weusi ni asilimia ngapi ya population na Tanzania Waislamu ni asilimia ngapi ya population? Na unajua historia ya affirmative action? Ilikua kuwapa opprotunity blacks wacatch up kutokana na utumwa. Waislamu walikua watumwa Tanzania? Na pia sasa hivi Marekani it is illegal to employ somebody based on their age, gender, religion or race/ethnicity.

Pili, kwa nini tuangalia dini, jinsi na ukabila wa mtu kama unavyo suggest. Je hauoni hapo tuta kuwa tuna kosa merit? Je hauoni kwamba kuna watu wata kosa kazi kwa sababu nafasi za watu wa dini yake imesha jazwa. Sasa huo kama si udini ni nini? Haujioni mwenyewe kwamba hapa una advocate udini kwa kusema tuwe na mfumo unao angalia dini ya mtu kwenye ajira?



Sasa huo ndiyo udini. Ukitaka mtu aeleze dini yake ina maanisha una ajiri watu based on their religion. Kwa hiyo wewe una advocate udini. Au muda wote huu ulikua una pinga udini bila kujua mwenyewe udini ni nini?
Kuhusu wanawake ubaguzi ni ubaguzi tu hauwezi kusingizia mila. Kama uta singizia mila basi kuna wengine wata kuambia wao ni wadini kwa sababu ya mila.

Kuhusu Marekani nisha kuambia blacks are 12%. Waislamu wala Wakristo siyo wachache hivyo Tanzania. Kwa nini hao wengine ambao ni minorities hawa tetewi? Unacompare vitu halafu una jichanganya mwenyewe. Je Waislamu Tanzania ni minorities mpaka utake kitu kama affrimative action Tanzania?


Sasa nikuulize nani mdini? Si yule anaye taka watu waajiriwe kutokana na dini zao?
 

So to make it short and simple. Una taka ajira iangalie dini ya mtu, yes or no?
 
So to make it short and simple. Una taka ajira iangalie dini ya mtu, yes or no?

Dini isiwe kigezo cha kwanza bali iwepo katika moja ya sababu ya kumuajiri mtu. Sababu kubwa ni kuondoa mvutano wa kidini. Unajua TZ haiwezi kupinga kila siku kwamba TZ haina udini wakati wananchi wake, na serikali imecomfirm kupitia JK kwamba TZ kuna udini. Source hotuba ya JK.
Nimetoa mfano katika nchi nyingi ambazo zinapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe ni kwa sababu ya ignorance ya viongozi wake.
 

Kwa hiyo vigezo vingapi una taka vizingatiwe zaidi ya elimu na experience? Una taka dini izingatiwe. Kuna watakao taka jinsi izingatiwe. Kuna watakao taka Ubara na Uzenji. Kuna watakao taka mikoa izingatiwe. Kisha kuna watakao tana makabila ya zingatiwe. Sasa kwa mtazamo wake kweli kwa mfumo huo tuna weza tuka pata mtu anaye faa au tutaishia kuweka people based on who they are (religion, gender, tribe etc) instead of what they know and what they can do? Kwa sababu ukitaka dini izingatiwe haitaishia hapo. The division (or diversity as you call it) ita ongezeka tu.

In short mkuu unacho pendekeza ni kwamba udini uwe moja ya vigezo vinavyo zingatiwa. Na ndiyo maana nika sema labda haujui definition ya udini. Udini ni upendeleo au ubaguzi wowote unao tokana na dini ya mtu. Kwa hiyo mtu akipewa kazi na dini ikawa moja ya vigezo basi huo ni udini. Call it what you want to call it.
 
yes mdini

angalia viti vitatu vya upendeleo mwaka huu vya ubunge
angalia timu ya juu ya chama wala hastuki, yes mdini
 


Pamoja ni kwamba ilikuwa na racism, sasa je unataka kusema race wanayouliza ktk form zao ni kwa sababu USA bado wanaendelea na racism?
TZ ipo ktk tatizo kubwa la udini kuliko watu wanavyofikiria. TZ hatuna statistic zozote zinazoonyesha population kati ya Waislamu na Wakristo. Halafu nchi yetu imegawanyika zaidi katika misingi ya kidini kuliko makabila. The Only way to solve these issues through dialogue, and fairness..
 
Pamoja ni kwamba ilikuwa na racism, sasa je unataka kusema race wanayouliza ktk form zao ni kwa sababu USA bado wanaendelea na racism?

O.k. so ume kubali ni racism meaning huo siyo mfano wa kuiga. Kwa sababu you are contradicting yourself. On the one hand you say tuige mfano wa Marekani but one the other hand you are calling it racism which ni form ya ubaguzi. Sasa kama you can advocate for that what makes me think you can't advocate for udini Tanzania?


Mkuu you are full of contradictions. Kwanza hapa tena una taja Waislamu na Wakristo tu kana kwamba hamna dini zingine which shows you are not advocating for equality. Pili unasema Tanzania hamna statistics za Waislamu na Wakristo. Kama hakuna statistics za Waislamu na Wakristo unajua sehemu mbali mbali watu hawapo in proportionality to their religion? Kama haujui idadi ya Waislamu na Wakristo utasemaje ni udini sehemu kukiwa na Wakristo kumi na Waislamu watatu? Si haujui idadi? What makes you sure hao watatu hawa represent proportionality ya dini hizi mbili?
 
Ukiwapa ukweli wanakimbilia propaganda za kusema kuwa Waislam hawajasoma... Wakati mwingine utasikia ooh nendeni shule kwanza! Propanda zimewachukuwa kiasi wanajiona kuwa wao ndio wasomi peke yao...!

Wamesoma nini? Hawana taaluma. Hata wasome wapindukie, kama hawana taaluma ni bure.
 


Dini/Udini ni solution ya kusolve our problems. Tanzania ni moja kati ya nchi chache duniani zenye two strong religion. Kwa hiyo issue ya TZ ipo tofauti kabisa na nchi nyingi sana. Tuchukulie mfano wa Rwanda, Clinton aliwaambia waoane between wahutu na watutsi ili kuondoa ukabila.
Lakini moja ya solution iliyofikiwa ni kushare madaraka, nk.
Sasa kwa mfano, wewe ndiye mkuu fulani, halafu unatakiwa uajiri watu kwa vigezo vya elimu na uzoefu. Lets say wasomi wengi unaowajua wewe ni Wakristo halafu ukawapa kazi kwa vigezo vya elimu yao na uzoefu. Lets say kulikuwepo na Wasomi wengi wa Kiislamu ambao ulikuwa huwajui. Lets say baada ya kuwaajiri wewe ulikuwa unawaajiri kwa sababu ya vigezo vyao na si dini zao. Baada ya muda, public ikaanza kuquestion decision yako kwamba ulikuwa mdini kwa kupendelea Wakristo tu, ktk kazi za public.

Jibu; wewe si mdini bali ni kiongozi IGONORANT Kwa sababu umeignore reality ya TZ. Kama ikitokea tatizo katika nchi ni kwa sababu ya IGNORANT decision ambayo uliifanya.
Hili tatizo kubwa la viongozi wetu wa TZ, ni MAIGNORANT. Baadaye watakuja kujuta kwa action wanazozifanya sasa hivi.
 


Naelewa ninachosema. Mimi sikubaliani na suala la ubaguzi wowote kama ni la udini, au rangi. Ninachosema kwamba kuna watu ambao wanapinga kwamba TZ haina udini wakati wananchi wake na rais wake wameconfirm kwa nchi TZ kuna udini. Suala la population kati ya hizi dini ni kuonyesha jinsi gani TZ ipo ktk tatizo kubwa zaidi kwa sababu hatuna statistic zinazoonyesha population kati hizi dini mbili.

Kuzungumzia Dini/Udini haimaanishi kwamba mtu fulani ni biases wa dini fulani. Tupo kwenye progress ambayo kila nchi ktk development lazima ipitie.
 

Basi hao public wata kuwa wadini. Listen mfano wako inaenda both ways. Kama mimi wasomi wengi nanao wajua ni Wakristo basi kuna mtu mwingine wasomi wengi atakao wajua yeye ni Wasilamu. So ni the grand scheme of things it all equalizes. Kama tukiangalia elimu na uzoefu basi kuta kuwa na haki because kama fulani wengi anao wajua ni Wakristo basi mwingine wengi anao wajua ni Waislamu. As long as wana vigezo why not? Kwa sababu kuna sehemu kuna Wakristo wengi zaidi ya Waislamu na kuna sehemu kuna Waislamu wengi zaidi ya Wakristo. It all evens out. Kusema kuwa na uwiano wa kidini kwenye kile ofisi ya kila sehemu ni kuwa unrealistic.


Mkuu statement sahihi ni kiongozi ignorant siyo "kiongozi ignorance". I hope haumind kusahihishwa na Mkristo. Anyway kwa nini mnaforce tatizo? Mbona sija wahi kusikia nchini hapa Waislamu au Waktristo wakiandamana? Kwa nini huo udini mnauona nyie tu? Mimi nina marafiki wengi Waislamu sija wahi kusikia waki lalamika. Tena linapo kuja swala la kazi sija wahi kusikia anaye lalamika kukosa kazi kisa dini yake kwa maana mabosi Waktristo na Waislamu wote wapo kwenye jamii yetu. Sasa iweje leo nyie wachache mjifanye mna represent kila mtu wa imani yenu?
 

Sasa na wewe ndiyo unakuwa ignorant. Raisi kusema kuna udini ndiyo ina prove beyond a shadow of a doubt kwamba kuna udini? Kwa hiyo kesho akiingia raisi mwingine akisema hamna udini uta badilisha kauli na kusema hamna udini raisi kasibitisha? Where is your reasoning mkuu. Tambua yule ni mwanasiasa na politics and facts do not always go hand in hand. Kuna yule mwanasiasa katuambia zile kura milioni kumi ambazo hazi kupigwa zinge kuwa zake nae tumuamini?

Pili, hamna sehemu yoyote ambayo nime kuiya mdini kwa kuongelea dini. That is your own conclusion. Nilikuita mdini kwa kuadvocate ajira ziangalia among other things dini. Ina maana kwa utaratibu unaotaka wewe Athumani hata kama ana vigezo vyote ana weza kukosa kazi kwa sababu kwenye ofisi hiyo idadi ya watu wa dini yake wamesha timia!

Tatu, umesema JK kathibitisha kuna udini right? Haya JK kateua Wakristo hao 32 mnaodai dhidi ya Waislamu 18. Sasa je tumeenda full circle na sasa una jiunga na wanaodai JK ni mdini kwa sababu kateua baraza la mawaziri bila kuangalia uwiano wa dini? Si that's your point? Ama?
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…