Je, huu ni ukweli uliofichwa kwa miaka mingi?

Hili halihitaji tafakuri yoyote mkuu
Ukitafakari sana utaangukia kwenye falsafa tu za kibinadamu.
Adam naye alikula tunda
Naleta maandiko kuhusu hao wana wa Mungu na wana wa Ibilisi
 
Hili halihitaji tafakuri yoyote mkuu
Ukitafakari sana utaangukia kwenye falsafa tu za kibinadamu.
Adam naye alikula tunda
Naleta maandiko kuhusu hao wana wa Mungu na wana wa Ibilisi
Mkuu hoja sio tunda pekee mzizi wa hoja ni kwamba Adam sio baba wa Cain..... Na kwamba Nyoka alipomdanganya Eve ilihusisha ngono kati ya nyoka na mwanamke na hayo sio maneno yangu bali nimenukuu hapo maandiko matakatifu ya Biblia na wayahudi ambayo yanaonyesha Adam akikiri kuwa mtoto hakuwa wake bali Seth.

Kuhusu Tunda pia ieleweke haikuwa tunda kama tunda la kawaida ila ni metaphor tu imetumika kwahiyo tunda laweza kumaanisha kitu chochote hivyo kama ikiwa ni ngono ndio tunda basi tuseme baada ya Hawa kunajisiwa na nyoka naye akaenda kulala na mmewe and the rest is history.

Hivyo sijatoa falsafa za duniani bali nimenukuu maandiko matakatifu labda tuanzie hapo je ina maana Biblia ya kikristo ya NJT imepotosha??

Tuanzie hapo
 
Kabla haijafikabali hii habari, mkuu check maandiko ya mwanamke anaedaiwa mke wa Adam wa kwanza- "Lilith" kabla ya Hawa. Inasadikika kabla ya Hawa, huyu alionekana kumzidi Adam na akaomba awe sehemu ya Adam. Kwa utukufu wa Adam, Mungu Mwenyezi akaamua kumleta mwanamke mpole Hawa.

Binafsi madam hii itanipeleka kumuona mwanamke mkaidi kwa mumewe kuwa wa uzao huu, Lucifer kwa wasiojua inanguvu ulimwenguni, inanifanya niamini kwamba uzao wa Adam una mixer na mashetani ambayo yanaishi, na kutufanya tuamini Mungu anatukinda Sana kea sabab huo uzao unanguvu za kimalaika- sheitwaini
 
Mkuu acha kufikiria kwa uwezo mdogo kiasi hichi, Mungu mnamuweka wapi unapowaza uwezo wa dunia? Mungu anashindwa kufanya nini
Mkuu biblia ni pana sana! Mtiririko wa biblia unaeleza tu kwa wale wanao hitajika mfano Musa anaelezewa yeye tu au Daud pia Yesu mwenyewe hakuna story kuwahusu ndugu zake. Biblia yenyewe inasema kama vyote vingeandikwa dunia isinge weza kubeba.
 
Mkuu zitto junior asante kwa kunikaribisha katika uzi wako mwingine tena. Lakini nitaandika kwa kifupi tu, ni hivi; hoja hiyo ya kusema eti lile halikuwa "tunda la mtini" bali lilikuwa ni tendo la ndoa mimi binafsi nakataa hasa kutokana na NENO la MUNGU halidanganyi. WARUMI 3:4 "MUNGU ajulikane kuwa mkweli na wanadamu wote waongo"..... Pia soma ZABURI 116:11

Kwa kuwa MUNGU siyo muongo na Musa alikiandika kitabu cha MWANZO kwa kuambiwa na MUNGU mambo yote yaliyotukia, hivyo yote yaliyoandikwa kwenye BIBLIA ni KWELI tupu pasipo shaka yoyote ile!

Ili tujue kwamba lile lilikuwa ni tunda la mti kweli na siyo vinginevyo hebu soma MWANZO 3:6 .."mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho nao ni mti wa kutamaniwa kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala".

Nime-highlight hayo maneno hapo juu kwa rangi nyekundu ili tuyajadili na kupata majibu...."ule mti wafaa kwa chakula"... sentensi hii inatosha kabisa kutonesha kuwa ule ulikuwa ni mti wa matunda kama miti mingine ndiyo maana Eva aliona unafaa kwa chakula. Kama tunda lingekuwa ni "uchi" wa Eva au "uchi" wa Nyoka, Je! uchi unafaa kwa chakula? Au tendo la ngono linafaa kwa chakula?

...."basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe naye akala"...hapa tunaona wazi kabisa ni kitu alikula kwa kutumia mdomo wake, maana baada ya kula alimpatia na mumewe naye akala. Je! kama tunda lingekuwa ngono angewezaje kula "uchi" wake na kumpa mumewe naye ale?


Kuna watu watabisha na kusema; "oooh, hiyo ni lugha tu ilitumika kuficha ukweli". Mimi nasema hapana, kama kitendo cha ngono kingefanyika basi BWANA MUNGU angesema kuwa ni ngono ilifanyika wala asingeficha ukweli. Ngono ilipofanyika kati ya malaika waasi na wanadamu BWANA MUNGU hakuficha bali alisema wazi;

Baadhi ya Malaika walipoacha viti vyao Mbinguni na kuja duniani kufanya ngono na binti za wanadamu, BWANA MUNGU alisema bila kificho, MWANZO 6:1-2 ..".........Wana wa MUNGU waliwaona hao binti za Wanadamu ya kuwa ni wazuri, wakajitwalia wake wowote waliowachagua". Tukubali tu kuwa MUNGU haufichi UKWELI.

Sasa hebu ona ushahidi mwingine kutoka kwenye Biblia kuwa lile lilikuwa ni tunda la mti na siyo tendo la ngono. Soma MWANZO 3:22-24 ... "BWANA MUNGU akasema basi huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya, na sasa asije akanyoosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akala akaishi milele................akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka huko na huko kuilinda njia ya mti wa uzima".

Baada ya Adamu na Eva kula matunda ya mema na mabaya, kulikuwa na mti mwingine wenye matunda ya Uzima, ambao sasa ikabidi BWANA MUNGU auwekee ulinzi ili Adamu na Eva wasije wakaenda na kunyoosha mikono yao na kuchuma matunda yake na kula. Kwa mistari hii tunaona UKWELI ni upi na uongo ni upi. MUNGU hasemi UONGO hata siku moja, wala Biblia haijadanganya wala kuuficha UKWELI.

Shetani ni mjanja sana na anatumia ujanja wake kuwadanganya na kuwarubuni Wanadamu ili waone kuwa MUUMBA wao ni muongo. Lengo la Shetani ni kutuaminisha kuwa MUNGU ni muongo na alitumia ujanja huo huo kumfanya Eva amuone MUNGU ni muongo. Shetani amewasaidia Wanadamu kuandika vitabu vingi sana vyenye maudhui ya kupingana na Biblia ili tu kuwafanya wanadamu wamuone MUNGU ni muongo.

Vitabu hivi vyenye maudhui ya kudanganya vipo vingi sana na viliandikwa miaka mingi sana nyuma, enzi za mfalme Nimrodi wa Babeli ya kwanza kabisa. Hapa ndipo palipokuwa chimbuko la dini zote za KIPAGANI na maandiko yenye kupotosha.
MWANZO 3:22-24 ... "BWANA MUNGU akasema basi huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya, na sasa asije akanyoosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akala akaishi milele................ mkuu kwa hii kauli hapo inaonesha Mungu alikua surprised hao walivokula hilo tunda ina maana hakujua mbeleni kuwa itakuja kutokea hivo? na je alikua hana uhakika kuwa tunda la uzima litaliwa mbeleni mpaka akawafukuza kwa kuogopa isije ikatokea hivo?
 
Habari za jioni wana JF mada ya leo ni sensitive kidogo hivyo ningependa tuisome kwa umakini,tujifikirishe na tujadiliane kwa mapana bila kashfa za kidini,kejeli,matusi,hasira n.k maana mada hii ni kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana mawazo,maarifa,elimu n.k sio uwanja wa vita
View attachment 828516
Mada ya leo ni kuhusu ukweli wa mzazi halisi wa Cain ama tuseme kizazi cha nyoka na kizazi cha Adam. Ikumbukwe nyoka anyeongelewa hapa sio nyoka huyu wa sasa anayetambaa naongelea yule wa kabla ya tunda kuliwa.

Reference yangu itakuwa vitabu vya dini kadhaa kuanzia uyahudini,biblia,apocrypha,pseudipigraphi, maandishi ya wanatheolojia na vitabu vya kihistoria.

UTANGULIZI
Kupitia nadharia hii, yote yanaanzia kwenye bustani ya Eden ambapo tunaona shetani kupitia nyoka akimshawishi Hawa "kula tunda" na katika tunda hilo inaaminika linahusianisha ngono ambapo nyoka alimlala Hawa na kumpachika mimba ambayo baadae alikuja kuzaliwa Mtoto wa uzao huo yaani kizazi cha nyoka yaani Cain ili shetani aweze kuharibu uumbaji wa Mungu.

KWANINI NADHARIA HII?
Ili tuamini Nyoka alilala na mwanamke tunaweza tumia vigezo vifuatavyo

1. Adhabu kubwa ya Mungu kwa mwanamke ilikuwa ni kwenye sekta ya ngono sababu ndipo alipoanguka ndio maana Mungu akamhukumu sababu ya tendo la ndoa na mimba aliyobeba pia.

Mwanzo 3:
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala

Pia shetani tukisoma kwenye kitabu cha biblia (madhehebu kadhaa hukitumia) cha Apocalypse of moses 26:1-4 tunaona hukumu ya Mungu kwa shetani kuwa atamtoa masikio,mabawa na UUME!!!!

Hivyo nadharia hii kuwa ngono ilihusika inapatiwa nguvu kupitia mistari hii

NANI BABA WA CAIN?
Biblia ya kiswahili inasema

Mwanzo 4:1
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA

Lakini tafsiri iliyofanyiwa uhakiki kupitia New jerusalem Translation inasema hivi kwa kiswahili

...... Nimepata mtoto kutoka kwa malaika wa Bwana

Hivyo kama tafsiri hii ya NJT ina maanisha Adam alikiri kuwa mtoto sio wake ila wa MALAIKA ambaye kwa muktadha huu ni lucifer.

Kwenye biblia ya kiebrania neno lililotumika kwa KUMJUA ni Yada na Eth ambapo Yada baada ya kufanyiwa utafiti mpya limeonekana haimaanishi tu ni kumlala mwanamke bali inamaanisha KUTAMBUA KITU na Eth ina maanisha ALAMA FULANI(mabadiliko) hivyo tukiuandika mstari huu upya kutumia tafsiri ya maneno haya itakuwa hivi;

Adamu akatambua alama/ishara ya mabadiliko juu ya Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kutoka kwa malaika wa BWANA

Kwahiyo mpaka hapa tumeshapata maana tofauti kabisa ya mstari huu si ndio wakuu??

JE KWANINI NASEMA CAIN SIO MWANA WA ADAM
1. Biblia huko mbele inamtaja Cain kama alitokana na ''yule mwovu'' yaani shetani

1 Yohana 3:12
12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
View attachment 828519


2. Biblia inamtambua seth kama mtoto pekee wa Adam maana inadai Henoko alikuwa mtu wa 7 baada ya Adam na ukihesabu utagundua imetaja uzao wa seth peke yake na imemuacha Cain peke yake hivyo ikimaanisha Cain hakutambuliwa kma mwana wa Adam

Yuda 1:14
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao
View attachment 828520


3. Tunaona hata seth ndio biblia inaonyesha alizaliwa kwa mfano wa sura na mfano wa adam

Mwanzo 5
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi

Hii yote ikimaanisha Cain hakuwa uzao wa Adam ndio maana hakufanana naye Adam kwa lolote hivyo muandishi hakuona sababu ya kujumuisha jambo hilo alipozaliwa cain.

4. vitabu vinavyotambuliwa na dini ya kiyahudi kama Zohar Pekudei 21:5 kinakubali hoja hii.

Baada ya adam na mke wake kufanya dhambi, na shetani kumjua Hawa na kumnajisi, Hawa alimzaa Cain. Alikuwa na umbo la duniani na kuzimu. Hivyo,alikuwa wa kwanza kuleta kifo duniani,iliyosababishwa na upande wake wa kuzimu,sababu alitokana na uchafu wa najisi ya nyoka (kwa hawa). Asili ya nyoka(shetani) ni udanganyifu,mauaji,na Cain,alijifunza nyendo zake. (Utafsiri binafsi)

HITIMISHO
Kupitia hayo maandiko machache nlioweza kupata ninaweza kufikia hitimisho kuwa kuna uwezekano tumefichwa kwa muda mrefu kuhusu uhalisia wa kilichotokea Eden nikaona nilete nadharia hii JF ili tuweze kufikiri pamoja na kupata ukweli wa jambo hili.

NB: Naomba Moderator msiunganishe nyuzi hii na zingine juu ya bustani ya edeni maana hii imejikita zaidi kwa Cain na sio maisha ya bustanini

Naomba kuwasilisha
Bwana Zitto ipo hivi. Hayo matunda yaliyoliwa yalikuwa matunda halisi na mti wa matunda halisi na siyo ngono. Kwani biblia inasema pia kulikuwa na mti mwingine wa matunda ya uzima(mwingine ni wa ujuzi wa mema na mabaya). Aliruhusiwa kula matunda mengine yote

Mwanzo2:16-17'' And the Lord God commanded the man, “You are free to eat from any tree in the garden; 17 but you must not eat from the tree of the knowledge of good and evil, for when you eat from it you will certainly die.”
 
Kama tuliumbwa tuishi milele ipi mantiki ya mti wa uzima? Halafu pia huenda adam na hawa hawakujua katazo ipasavyo maana ilikua ukila mti wa uzima ndio huwezi kufa ndio maana wakafukuzwa edeni na bustani kulindwa na malaika na mapanga ili wasije kula katika mti wa uzima wakaishi milele.
ANGUKO LA MWANADAMU

MATUNDA YA MTI WA UJUZI' USILE , SIKU UTAKAPO KULA UTAKUFA HAKIKA.
Fungu la tafakari:
“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamafanya dhambi.” Warumi 5:12.
Makusudi ya somo hili:Kuonyesha kuwa mwanadamu aliumbwa vyema ili aishi millele, na kwamba kifo ni matokeo ya kutokutii amri za Mungu.
UTANGULIZI..
Kazi ya uumbaji kwa siku sita, ilimalizika kwa kuumbwa kwa mwanadamu. Ulikuwa mpango wa Mungu, mwanadamu aweze kuufurahia ulimwengu milele. Lakini ilitegemea utii wake na kuwa na dini ya uongozi wa Mungu.
Mungu aliwaumba wanyama wengine wote – Samaki, ndege, mijusi, wadudu, n.k “kwa jinsi yake” Kila jamii ya viumbe ilikuwa na mwonekano wa namna yake.
Lakini mwanadamu aliumbwa kwa namna ya Mungu, na si ya wanyama. Kwa viumbe wengine Mungu alitamka na vikatokea, lakini kwa mwanadamu, Mungu alienda chini, akafinyanga udongo, na “kumfanya” mtu kwa sura yake. Mwanadamu alikuwa ni kilele cha ubora wa kazi ya uumbaji ya Mungu.
“Pumzi ya Mungu” iliyoleta uhai kwa umbo lililofinyangwa la “mtu” ni zaidi ya pumzi tunazozijua. Hii ni kanuni ya uhai inayoweza kufananishwa na umeme unaoleta tofauti unapounganishwa kwenye gropu. Ni nguvu inayoanzisha uhai na kuendeleza (Matendo 17:28). Nguvu hii inapoondolewa, uhai wamtu hukoma.
Kuanguka kwa mwanadamu katika dhambi:

Mwanadamu alipoumbwa aliwekwa katika bustani ya Edeni. Mwanzo 2:8.
“Mungu alimweka mwanadamu chini ya sheria, kama sharti lisilokwepeka la kuishi kwake”
Bwana Mungu akachipisha katika ardhi kila mti wa matunda unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mwanzo 2:9.
Bwana Mungu akawapa agizo kuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile; kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Mwanzo 2:17.
“Wazazi wetu wa kwanza, ijapokuwa waliumbwa bila dhambi, hawakuwa kwenye mazingira yasiyofikiwa na dhambi. Mungu aliwaumba wawe na uhuru wa kimaadili, wanye uwezo kuchagua kutii au kutotii. ... Mti wa ujuzi, ambao ulikuwa jirani na mti wa uzima katikati ya bustani uliwekwa kuwa mtihani wa utii, imani na upendo wa wazazi wetu wa kwanza.
Dhambi iliingiaje?
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanzo 3:1
Majibu ya mwanamke;
Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Mwanzo 3:2,3;
Nyoka akasema nini baadaye?
Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanzo 3:4,5.
Shetani aliwaonyesha “Adamu na Hawa” kwamba wangenufaika kwa kuvunja sheria ya Mungu. Je, siku hizi hatusikii hoja zinazofanana na hizo? Watu wengine wanashutumu wale wanaozitii amri za Mungu, wanasema wanamawazo mafinyu, huku wakidai wenyewe kuwa wanamawazo mapana na wanafurahia uhuru mkubwa zaidi. Hiki ni nini, kama si mwangwi wa sauti ya Shetani toka Edeni inayosema , ‘siku mtakayokula matunda ya mti huo’ (vunjeni matakwa ya Mungu) ‘Mtakuwa kama Mungu’’’’?
Ona madhara ya dhambi:
Baada ya Shetani kufanikiwa kuwadanganya wazazi wetu wa kwanza, madhara yakaanza kujitokeza. Wakafumbuliwa macho yao wakajiona wako uchi, (yaani wakavuliwa mavazi ya utukufu aliyo wavika Bwana) wakatengeneza mavazi ya mtini wakajivika (yaani wakajivika mavazi bandia) Wakajificha yaani wakakimbia mbali na uso wa Bwana. Mwanzo 3:6,7,16,17-19.

Laana ikawa juu yao. Kuzaa kwa uchungu, kula kwa jasho, na kifo kikawakabili, sasa ukweli wa Shetani ni upi? Alisema “hamtakufa bali mtafanana na yeye” je, leo hatufi? Hata wazazi wetu wa kwanza nao walikufa.
“Kwa mtu mmoja dhambi ikaingia ulimwenguni” na sote tumeshuhudi vifo, ajali, majanga ya kila namna. ...”Mauti ikwafikia wote kwa sababu wote wamefanya dhambi. Warumi 5:12. haya yote ni ushuhuda kuonyesha kuwa dunia inasumbuka na iko katika maumivu.


Kauli ya Mungu imebaki palepale “Hakika mtakufa” na ni kweli ndivyo ilivyo, hakuna anaye bisha sote tunajua kuwa siku moja tutakufa.
 
Niulize kitu mkuu, unachukuliaje statement ya Bwana pale eden kua wanadamu washakua kama Mungu/malaika (kama wao) baada ya kula tunda la mti wa ujuzi kitu kilichopelekea wafukuzwe haraka kabla hawajala mti wa uzima ili wasiwe/tusiwe kama wao? Je, hii inamaanisha ukitoa uzima wa milele wanadamu tunasifa kama za Wao?
Mkuu hoja sio tunda pekee mzizi wa hoja ni kwamba Adam sio baba wa Cain..... Na kwamba Nyoka alipomdanganya Eve ilihusisha ngono kati ya nyoka na mwanamke na hayo sio maneno yangu bali nimenukuu hapo maandiko matakatifu ya Biblia na wayahudi ambayo yanaonyesha Adam akikiri kuwa mtoto hakuwa wake bali Seth.

Kuhusu Tunda pia ieleweke haikuwa tunda kama tunda la kawaida ila ni metaphor tu imetumika kwahiyo tunda laweza kumaanisha kitu chochote hivyo kama ikiwa ni ngono ndio tunda basi tuseme baada ya Hawa kunajisiwa na nyoka naye akaenda kulala na mmewe and the rest is history.

Hivyo sijatoa falsafa za duniani bali nimenukuu maandiko matakatifu labda tuanzie hapo je ina maana Biblia ya kikristo ya NJT imepotosha??

Tuanzie hapo
 
Bwana Zitto ipo hivi. Hayo matunda yaliyoliwa yalikuwa matunda halisi na mti wa matunda halisi na siyo ngono. Kwani biblia inasema pia kulikuwa na mti mwingine wa matunda ya uzima(mwingine ni wa ujuzi wa mema na mabaya). Aliruhusiwa kula matunda mengine yote

Mwanzo2:16-17'' And the Lord God commanded the man, “You are free to eat from any tree in the garden; 17 but you must not eat from the tree of the knowledge of good and evil, for when you eat from it you will certainly die.”
Mkuu Biblia imeandikwa kwa codes sio kila neno unalitafsiri as it is n ndio maana unatakiwa ujiulize kama tunda ni hili apple kivp Adam akiri Cain sio mtoto wake?? Kwanini Hawa alipigwa laana kwenye mambo ya ngono mfano kuzaa na tamaa ya ngono itakuwa kwa mmewe n.k??

Wanatheolojia kote duniani wanakubali kuwa tunda halikumaanisha matunda tunayojua sisi ili ilikuwa ni fumbo tu...kaulize theologian yeyote atakueleza hili hivyo hapo tuelewane.

Mie nimeweka sources naomba unieleweshe je hiyo Biblia ya NJT imepotosha?? Vipi Biblia haijamhesabu Cain kwenye agano jipya kama part ya kizazi cha Adam?? Tuanzje hapo
 
Mkuu hao watu wapo, amini usiamini hao watu wapo hai mpaka leo. Wewe kutowajua haina maana kuwa hawapo. Nitakuja na uzi humu JF na kuelezea kwa kirefu hao watu ni akina nani na hapo ndipo mtatambua UWEZA wa MUNGU. NENO la MUNGU halisemi uongo hata siku moja!

Nikiweka huo "uzi" nitaku-tag mkuu.
Mkuu huo uzi ulishaweka?kama upo naomba uweke link hapa ili niusome hili swali huwa najiuliza sijawahi kupata majibu
 
...Dah!...kama Cain alikuwa uzao wa nyoka vipi wale 'wana wa Mungu' waliowajua wanadamu kipindi cha Nuhu walikuwa kina nani? Na walitoka wapi?

Je inawezekana kizazi cha Cain kiliangamia pia wakati wa gharika?
 
...Dah!...kama Cain alikuwa uzao wa nyoka vipi wale 'wana wa Mungu' waliowajua wanadamu kipindi cha Nuhu walikuwa kina nani? Na walitoka wapi?

Je inawezekana kizazi cha Cain kiliangamia pia wakati wa gharika?
Kwa nachofahamu.... Hao waliotokana na wana wa mungu tunawaita Wanefili ambao ni kikosi cha malaika kama Azazel,Semyaza n.k. waliotokea mbingu ya saba (Inadaiwa alipo Mungu yaani Yahweh)

ila Cain alikua purely seed ya Shamael (Lucifer) kutoka kuzimu.

Lakini cha muhimu ni kwamba Hawa wanefili wali target uzao wa Seth sababu ndio ulikua pure Seed according to mwanzo 5 (Uzao wa Yesu ulitokea hapa) na ndio maana Adam alimuona kama replacement ya Abel!! yaani mwanae wa kwanza na sio eti kijana wa pili baada ya Cain.

All in all walifanikiwa ku infiltrate kizazi cha seth na wenyewe wakawa kizazi cha nyoka kama Cain tu maana hawakuwa viumbe wa ''type'' ya Adam ila cross breed ya Malaika-Wanadamu.

But kupitia familia/ukoo wa Methuselah na Lamech ndio kinakua pure peke yake. Na ndio kupitia hao familia ya Nuhu ikaponea gharika meaning waliobaki wote Yaani familia ya Cain na Seth pamoja na wanefili waliteketea kwa maji.
 
...Dah!...kama Cain alikuwa uzao wa nyoka vipi wale 'wana wa Mungu' waliowajua wanadamu kipindi cha Nuhu walikuwa kina nani? Na walitoka wapi?

Je inawezekana kizazi cha Cain kiliangamia pia wakati wa gharika?
kama kizazi cha Cain & Sethi kiliangamia chote mfalme Ogu alitokea wapi?
 
Kwa nachofahamu.... Hao waliotokana na wana wa mungu tunawaita Wanefili ambao ni kikosi cha malaika kama Azazel,Semyaza n.k. waliotokea mbingu ya saba (Inadaiwa alipo Mungu yaani Yahweh)

ila Cain alikua purely seed ya Shamael (Lucifer) kutoka kuzimu.

Lakini cha muhimu ni kwamba Hawa wanefili wali target uzao wa Seth sababu ndio ulikua pure Seed according to mwanzo 5 (Uzao wa Yesu ulitokea hapa) na ndio maana Adam alimuona kama replacement ya Abel!! yaani mwanae wa kwanza na sio eti kijana wa pili baada ya Cain.

All in all walifanikiwa ku infiltrate kizazi cha seth na wenyewe wakawa kizazi cha nyoka kama Cain tu maana hawakuwa viumbe wa ''type'' ya Adam ila cross breed ya Malaika-Wanadamu.

But kupitia familia/ukoo wa Methuselah na Lamech ndio kinakua pure peke yake. Na ndio kupitia hao familia ya Nuhu ikaponea gharika meaning waliobaki wote Yaani familia ya Cain na Seth pamoja na wanefili waliteketea kwa maji.
kama kizazi cha Cain & Sethi kiliangamia chote mfalme Ogu alitokea wapi?
 
kama kizazi cha Cain & Sethi kiliangamia chote mfalme Ogu alitokea wapi?
Mkuu ukisoma vizuri bible Mwanzo 14:5 utaona warefai/wanefili wanatajwa kuwepo duniani.

Na hata kipindi wayahudi wameenda kuvamia canaan bado walikuwepo wanefili.

Sasa hapo kuna nadharia mbili

1. Mke wa Ham aliyeitwa Nei'tamuk alikua kutoka jamii zilizoingiliana na hao wanefili hivyo alikuja Kuendeleza kizazi cha hao wanefili tunaowasoma baada ya gharika.

2. Kma nlivyoeleza kwenyw uzi huu

Mfalme Ogu alipona gharika maana alikua pamoja na Nuhu wakati wote wa gharika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom