Je, huu ndio ulikuwa mwisho wa Hananja?

Je, huu ndio ulikuwa mwisho wa Hananja?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,704
Reaction score
861,039
Alipendwa sana mitandaoni kutokana na maudhui yake na namna alivyowasilisha hoja zake.. Ni mwerevu na tajiri wa maneno ya Kiswahili... Akijua vema kuyachagiza anapofanya uwasilishaji.. Hakukauka mitandaoni
Waswahel wanasema ngoma ikivuma sana hupasuka!

Aidha kwa kujua ama kutojua.. Ama kwa utashi wake au ushawishi wa shekeli bila kuzingatia mahitaji ya nyakati na pengine kwa namna fulani kulazimishwa akajiingiza mzima mzima kwenye sakata la Gwajima na serikali

Ni sahihi kutoa maoni yake kama Mtanganyika lakini alikosea sana kwa nafasi yake na kule kuanza kutaja vyeo vyake vingi na taasisi anazosimamia ikiwemo mojawapo ya rais

Akatoa maoni yake kwa namna ya kumkandia vibaya sana Gwajima, waumini wake na kanisa lao... Ni maoni ambayo yalivuka mipaka na kuonekana alitumwa kumshambulia direct Gwajima na waumini wake!

Hata hivyo kwa body language take kwa siku ile ni kama kuna kitu hakikuwa sawa.. Maana kwanza alitanguliza kujisifu kwingi na mashambulizi yake yakajaa kujihami kwingi sana!

Sijui kwanini alishindwa kusoma alama za nyakati.. Sijui alipatwa na upofu gani mpaka kushindwa kuona kuwa kile kilichofanyika kwa Gwajima, waumini na kanisa lao kilikuwa na kasoro kubwa!

Anyway lakini baada ya ile Press conference yake umaarufu wake ukapotea ghafla.. Ni muda sasa sijamsikia wala kumuona na mbwembwe zake mitandaoni...
Anaweza kuvaa ujasiri mkuu na kuomba radhi.. Muungwana ni kitendo.. Akiweza hili ataona matunda yake!


View: https://youtu.be/UPp-jCBqkTM?si=26z8TPTw5S5unhI0
 
Huyu mzee Namfahamu mno Tangu akiwa Muinjilist wa Babu yangu Mchungaji.......

Kabla hajawa Mchungaji alikuwa Muinjilisti wa Babu, vimbwanga vyake vyote Navijua.

Ana kundi la Mateja na kwaya ya mateja , zaidi ya watu 50 wanakwenda kwake kila siku kula Ugali wa Bure.
 
Back
Top Bottom