Je, hili linawezakana vipi? Katibu Tawala Wilaya ya Mbarali azitaka CHADEMA, CUF na ACT kuwasilisha taarifa za vyanzo vya fedha na namba za akaunti

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Katibu Tawala Wilaya ya Mbarali, Michael J. Semindu ameviandikia barua Vyama Vya ACT Wazalendo, CUF na CHADEMA barua kuvitaka kuwasilisha taarifa zao katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.

Barua hiyo ambayo nakala imeenda kwa Mkuu wa Wilaya inavitaka vyama hivyo kuwasilisha;
  1. Muundo wa Uongozi wa Chama/Viongozi waliopo sasa katika Ngazi ya Wilaya
  2. Taarifa za vyanzo vya fedha na namba za akaunti za vyama hivyo pamoja na namba zao za simu
  3. Majengo ya Ofisi
  4. Miradi ya Chama
474CD080-84D5-4535-9AF1-E85284FA97F2.jpeg


UPDATE
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga amesema “Wao hawawezi kutoa taarifa hizo kwani zipo chini ya Baraza la Wadhamini hivyo waimbia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuwa waandike barua kwenda kwa Katibu wa Baraza la Wadhamini kupata taarifa hizo”
 
Back
Top Bottom