Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 28,409
- 81,899
Ninaomba tu kufahamau kama hiki kitendo kinachofanywa na hii Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), kama ni sahihi au la. Binafsi naona kama ni kitendo cha kihuni.
Maana mwezi uliopita kuna kundi kubwa la wahitimu wa vyuo vikuu walioko kwenye utumishi wa umma, na ambao kimsingi walishakatwa kwa miaka mingi deni la hii Bodi na kumaliza; wameanza tena kukatwa na hii upya kwa kisingizio cha retention fees, na bla bla nyingine!
Yaani watu wamebambikiwa madeni kwa sababu tu hawakuchukua cheti cha kumaliza hayo makato!
Hivi inawezekana kweli taasisi ikukopeshe pesa, baadaye ikuwekee deni kwenye salary slip na kuanza kukukata mpaka deni linaisha! Halafu baada ya miaka 5, taasisi hiyo hiyo inaanza kukukata tena deni lile lile, huku kukiwa hakuna maelezo ya kujitosheleza!
Natoa rai kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia Waziri mwenye dhamana waingilie kati jambo hili. Maana wanachofanyiwa wafanyakazi wa nchi hii na hii Bodi ya Mikopo, kwa mtazamo wangu ni uonevu. Na kitachangia sana kuendelea kurudisha nyuma morali ya kufanya kazi.
Watu wa sheria pia wangeingilia kati jambo hili! Usawa huu mfanyakazi ana majukumu lukuki ya kifamilia, halafu unakuja kumkata tena makato upya, na wakati ulishamkata huko nyuma kwa miaka mingi, mpaka deni lake likaisha.
Moderator, naomba uniandikie hapo mwishoni kwenye kichwa cha hii mada yangu, haya maneno matatu; yao, ni sahihi?