The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,606
- 47,079
Jiulize ni kwanini unajisikia kufanya hivyo, wakati mwingine inaweza ikawa ni tabia yako uliyojifunza nyumbani kwenu au unafanya hivyo ili uwapendeze watu unaotoka nao out! ila kama unafanya kwa sababu unapenda moyoni kufanya hivyo ni jambo zuri lakini liwe na kiasi, hasa kwa jinsia tofauti na yako.
Anachokisema Quruxbadan huenda wengine wakafikiria anatania, nadhani hii inakua ni tabia ya mtu kama ulivyoelezea hapa mkuu.
Hata mimi nina hiyo kitu sana, yaani tukiwa sehem napenda nigharimie mimi hata kama tuko na wanaume wenzangu. Nakumbuka kuna siku tumeenda kula na bosi wangu tena sio mara moja, na yeye ni wa kiume ikija bili nataka nilipe mimi, akilipa yeye next time akisema tukale naona vibaya na siwi huru kabisa.
Kuna siku akanipa darasa, kwamba tunafanya kazi ili tupate pesa na akasema bado unasafari ndefu sana, sikukatazi kuwa na roho nzuri na ya ukarimu ila jitahidi kuwa mwangalifu vinginevyo watu watatumia huoukarimu wako vibaya.
Nikahama kampuni nyingine kuna mzungu yeye wakike, tukienda kula nataka nilipe. Siku hiyo akaniambia kuanzia leo kila mtu analipa bili yake. Mwingine nililipa bili, akasema tangu nije TZ wewe ndio mtu wa kwanza kunilipia bili. Nikaanza kulichukulia hilo suala kwa mtazamo tofauti na kujitahidi kuwa na kiasi.
Nilikaa nikawaza nikaona ni ujinga, mda mwingine unalipa hadi unabaki bila pesa na unaona ni heri kuliko mtu akulipie bili...it sounds senseless ila ndio hivyo.
Quruxbadan, jaribu kuwa na kiasi.