Je, hii ni sawa?

feysher

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
2,656
2,762
Wakuu nisaidieni kunishauri nahitaji kujitegemea kutoka nyumbani na kwenda kupanga ila tangu niwashirikishe nyumbani kuhusu mpango wangu kila mtu amelichukulia kwa mtazamo negative kwamba ni mapema kwenda kupanga kwa mtoto wa kike,natakiwa niondoke mpaka niolewe,najiona nimekua,nimepata bwana/danga ndoananichanganya,nitakua siheshimiki katika jamii.

Je kama Ke siruhusiwi kuendesha maisha yangu kwakua sijaolewa bado?

Hii ni sawa kweli?
 
Unafanya kazi???? Hii ndio nafasi ya pekee ya wewe kutoka hapo kwenu ila kama ni kula kulala sahau kuruhusiwa kwenda kupanga subiria mwewe aje akunyakue mkaanze maisha huko

Nafanya kazi ila hawanielewi kwa kigezo cha kwamba me ni Ke natokaje nyumbani sijaolewa nakimbilia maisha
 
Kwa uzoefu wangu mtoto wa kike kwenda kupanga anajipunguzia nafasi ya kupata husband material wanaume wengi wanakasumba yakuona binti akipanga basi amepangishwa na shugadady nawao wanakua wanachapa wanasepa wanajua unakibabu chako.
 
Kwaiyo nizeekee kwetu sababu nitaonekana nimepangishia nyumba kweli
 
Kama unajitegemea,kupanga ndio kukua kwenyewe,lakini kwa msichana kunaihitaji nidhamu sana,kwako kusiwe gheto kwa wadada wasioeleweka....kila la kheri.
 
Nionavyo mimi kuhama nyumbani inahitaji very strong reasons otherwise hawatakurelease.
Kama una dada zako wakubwa ama kama mama mnaelewana waambie vizuri.
Kua wewe ni binti umekua haupo comfortable sana kukaa nyumbani unahitaji kujitegemea na kujijenga
na kujifunza kufanya maamuzi yako.
Ila kama umepata mtu seious waambie tu wajue ili wakupe uhuru naohitaji labda hutahama ila ukichelewa hutaulizwa
 
Nimekwelewa sana tu na asante kwakuchangia ila sijapata mtu na nadhani naumia zaidi napoona nakuwa denied kuendesha maisha kwa maamuzi yangu mwenyewe just becouse sijaolewa...inamaana nisipopata mtu ntaishiaga kukaa kwetu
 
Mkuu hebu njoo pm nikushauri vizuri maana hapa ya wengi yatakuchanganya. Upatapo ujumbe huu usiufanye moyo wako kua mgumu. Awaiting for you

Mkuu moyo wangu mgumu kuja huko nishauri hapa hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom