Mremaaa
JF-Expert Member
- Jul 1, 2015
- 293
- 325
Habari wanaJamvi, nawasalimu sana.
Hongereni na poleni kwa majukumu ya siku ya kujipatia riziki. Naomba kuwashirikisha mkasa huu wa mke wangu wa ndoa, mnishauri kwa busara za ki utu uzima.
Mimi na mke wangu wote watumishi wa umma, yeye anafanya kazi DSM na mimi Mwanza, hii ilitokea baada ya yeye kupata uhamisho mwaka jana kutoka huku kwenda DSM. Kimsingi sikufurahishwa na huo uhamisho lakini ilibidi aende tu sababu wakati anapata uhamisho mimi nilikuwa masomoni DSM, hivyo ilikuwa kama kigezo cha yeye kuwa karibu ingawa wakati anahamishwa nilikuwa nimebakiwa kama miezi 7 ili nimalize safari hiyo ya masomo.
Baada ya kumaliza masomo nikarejea kazini hapo yeye kabaki DSM, mtoto tumejaliwa kupata mmoja wa kiume. Nimekuwa nikiitembelea familia yangu ninapopata nafasi, mara nyingine hata kutoroka ili kuwaona. Nimekuwa nikitoa taarifa mara chache kuwa nakwenda huko, wakati mwingine nimekuwa sitoi taarifa.
Sasa mkasa wenyewe ni hivi, mwishoni mwa mwezi jana nilisafiri bila kutoa taarifa hahati mbaya tulipata hitilafu ya gari hivyo tuliingia DSM saa 9 usiku. Nikachukua bolt mpaka nyumbani tunapoishi na mzigo yangu kama baba wa familia, tunapoishi ni chumba self na sebule, jiko, na choo cha nje.
Nilipofika kwa mshangao nikamkuta baba mkwe kalala sebleni, mke wangu kalala chini chumbani na binti wa kazi kitandani na mtoto. Baba Mkwe anaishi DSM (familia yao wazazi walitengana ila binti anamsikiliza zaidi mama kuliko baba sababu inaonekana kakulia sana umamani), kwa mazingira hayo ndoa kuliwa ikawa ngumu, pili baba mkwe akawa anarudi pale kana kwamba anaishi pale kwa zaidi ya siku 3, unaweza kutafakari kidogo hali niliyokuwa nayo.
Siku ya nne baba mkwe hakurudi na nilikuwa nimebakiza siku moja kuondoka. Baada ya kuondoka mke alihama bila kuniambia kama ana hama hapo, nilimwachia hela kwa ajili ya kodi sababu ilikuwa inaisha. Nimekuja kufahamu kuwa kahama zaidi ya wiki mbili mbele baada ya kupenyezewa na waliyokuwa majirani zake.
Kuuliza vipi mbona mmehama hamjasema kwanini? Akakataa kuwa hawajahama, kumbana sana akakubali kuwa wamehama, mlihamaje bila kusema? Ohoo ungejua! Nisaidieni, hili liko Sawa great thinkers?
Sababu anazotoa ni kuwa mimi namvamia sisemi kama nakwenda, hivi mwanaume ukitaka kwenda nyumbani kwako lazima useme? Labda nimelelewa vibaya mwenzenu? Kimsingi kwangu huwa naingia muda ninaotaka hata bila taarifa. Je, hii imekaaje?
Uamuzi wangu niliompa ni kuwa nikienda DSM sitatafuta alipohamia bali nitashukia hotelini aniletee mtoto nimuone halafu niondoke zangu, sababu kuhama bila kusema kuna lililojificha. Kwa upande mwingine nimeweka intelligence yangu kufuatilia na kubaini alipohamia.
Naombeni ushauri juu mkasa huu.
Asante sana nitashukuru kwa maoni na ushauri wenu.