Saalam!
Wahenga walisema mficha maradhi kifo humuumbua, nami leo nimeona niweke wazi mambo yangu ili niweze kusaidiwa kupitia jukwaa hili ambalo kwangu limejipambanua kuwa suluhisho la matatizo mbalimbali katika jamii.
Nisiwachoshe ndg wasomaji niende moja kwa moja kwenye lengo mahususi. Mimi ni mtoto wa kwanza kwa mke wa kwanza (ambaye alishatangulia mbele za haki) wa mzee wangu. Baada ya mama yangu kufariki mzee alikaa miaka Kama mitatu hivi akaamua kuoa mke mwingine ambaye wamedumu nae kwa miaka kumi na minne, lakini hajazaa nae.
Na mamamdogo huyu kipindi anakuja kuishi na mzee alikuja na watoto wake wawili ambao mzee aliamua kuwalea Kama watoto wake kabisa.
Na mamamdogo kwa kuona mzee anavyowajari watoto wake, nae ametulea sisi vizuri hata Kama kulikuwa na vichangamoto vidogo ambayo ni Kama 5% tu ambayo kwangu niliona ni kawaida sana ukilinganisha na taabu wanazopitia watoto wengine kwa mama zao wakambo.
Ni miaka miwili nilikuwa masomoni mkoa mwingine ambapo ndipo asili yetu huko, kipindi hicho sikuwahi kurudi huku anakofanyia kazi mzee.
Sasa baada ya kurudi nimekuta mambo yanavyoenda sivyo, kumbe mzee kupitia influence ya mamdogo aliamua kujenga nyumba huko nyumbani kwa kina mamdogo (ukweni) na baadhi ya miradi mbalimbali ameanzisha huko na wameshahamia huko kabisa.
Sasa baada ya kufika na Mimi huko naona nikama vile mzee kadhamiria kukaa hukohuko maana naona anazidi kuongeza ujenzi huko.
Baba yangu huyu amekuwa na Imani kubwa kwangu na Mimi vilevile kwake, Sasa kwa haya yanayoendelea nashindwa kumwelewa.
Ijapokuwa na sisi ipo nyumba ambayo tulikuwa tunaishi awali, lakini sasa bado mambo yanayonitatiza ni Kama haya
Kwanini ajenge nyumba huko ukweni ilihali hana hata mtoto na huyo mwanamke?
Kwanini baadhi ya samani nyingi za ndani ya nyumba zihamishiwe huko?
Huku kujengajenga na kuanzisha miradi huko ni kwa ajili gani?
Je, ndugu wakitutembelea ndo wafikie huko kweli?
Naombeni ushauri wenu na neno kidogo juu ya hili wandugu.