Tusijenge majumba makubwa tukistaafu yanachangia upweke

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
Habari zenu wadau.

Napenda wote tujifunze kitu hapa kwa maisha halisi niliyojionea.

Nilikua naalikwa na Mzee mmoja jirani mstaafu ambaye atakua na miaka 73 au zaidi. Siku zote tukikutana amekua akinialika nakosa muda.

Jana roho ikaniambia, huyu Mzee kila siku anakualika kwake hembu nenda na sikua na shughuli ya maana ya kufanya na ni zaidi ya miaka 4 amekua akinialika kwake.

Basi jana na hii sikukuu nikasema haya ngoja niende bila kumuarifu ili nisimtese maandalizi na pia nisikae sana.

Mida ya saa tano nikawa getini kwake nikapiga honi mlinzi akafungua nikaingia ndani. Ukweli nilikua napita tu nje na jua pale ni kwake lakini sikuwahi kuingia ndani.

Nikakutana na mazingira ya kihoteli na jumba la fahari. Basi nikakaribishwa nje sehemu nzuri sana ya kupumzika akaenda kumuita.

Na hapo parking kuna gari zake 2 zote anatumiaga. Mzee akaja na tabasabu akasema leo umepata nafasi karibu ndani tukaingia sebleni then tukaelekea Library matata kabisa.

Usijidanganye, kuna wabondo wanaishi maisha ya kwenye movies aisee na ni hapa hapa Tanzania. Nikamsifia Mzee kwa nyumba nzuri ya kifahari jibu likanishangaza 'haina hata maana sana, ningependa kuwa kwenye nyumba ndogo zaidi'.

Ndio tukaanzia hapo story nikamwambia kwanini wakati mimi naona ameyapatia maisha sana. Akasema 'nani kakuambia nina familia hiyo inayohitaji ili jumba?.

Mimi na watoto wawili wote wako UK na mke wangu amewafuata huko.

Anapenda maisha ya huko kuliko ya hapa ingawa huko wanakaa kwenye viapartment tu sio nyumba nzuri kama hii'.

Akasema huku akicheka. Ndio akanipa na ushauri kabisa 'kijana wangu ukiwa unajenga nyumba yako ya kustaafia usifikirie sana watoto labda kama unawatoto viwete unauhakika utakaa nao milele.

Lakini hawa wanaojitambua hawawezi kuja kuishi na wewe.

Wao watakua na maisha yao na familia zao. Mimi ningelijua hili mapema wala nisingepoteza hela yangu kujenga hili jumba.

Ningejenga nyumba yangu ndogo au ninunue apartment kipindi hiki cha uzee ningeishi huko. Kutunza nyumba hii ni kazi na gharama isiyo ya lazima.

Hapa lazima niwe na walinzi wawili , lazima niwe na house gardener na lazima niwe na house keepers wawili. Na bado na dreva.

Na ukweli wanaofurahia hapa ni dreva anaishi hapa na mke na watoto wake na housekeeper mmoja yeye hajapenda kuolewa hata kuwa na mtoto na nimekaa nae zaidi ya miaka kumi na tano toka akiwa msichana wa miaka 25 sasa hivi ana arobaini.

Hapa yeye ndio nyumbani kwake kabisa kuliko hata watoto wangu'. Nikamuuliza Mzee watoto na mke si wanakujaga Tanzania.

Akasema mke wake anakuja mara moja moja sana ila watoto wao hawapapendi Tanzania, mimi ndio naendaga kuwasalimia na Kila nikienda wanajaribu kunishawishi nisirudi Tanzania.

Lakini mimi ndio sipendi maisha ya nje na huko sio nyumbani kwangu. Nikamuuliza Mzee huna ndugu uje uishi nao hapa?

Akacheka sana akasema kwenye ukoo wetu kila mtu anajiweza na kila mtu anakaa kwake.

Tinakutana kwenye sherehe na matukio tu ambayo pia ni mara moja moja. Mdogo wangu anaenifuata anaumri wa miaka 64 na yeye hatuchekani anakaa Arusha mwenyewe kama mimi na watoto wote wako nje.

Akipata nafasi huja hapa Dar kunisalimia na mimi huenda kwake kumsalimia Arusha. Maisha yamebadilika sana sisi sio kama wazee wetu walikua hawakosi ndugu au watoto au wajukuu wakuishi nao.

Ukiwa unalelea vizuri ujue kabisa gharama ya mafanikio ya wanao ndio hii ya kuishi mwenyewe baadae.

Nashauri watu wengi na vijana kama nyie, mkiwa mnawaza kustaafu cha muhimu ni uwe na uwezo wa kujitegemea, uwe na hela zako ili usianze kutoa laana kwa watoto hawakutunzi au hawaji kukusalimia au ukalazimishwa kuishi pahala usipopataka.

Kuishi kwa watoto ni kupoteza uhuru na utu uzima wako. Kwa mtoto uishi umeshazeeka sana hujiwezi na ukiweza kujitunza mwenyewe mpaka mwisho wako ni heri zaidi.

Kama hapa mimi najigharamia kila kitu mwenyewe ikitokea nikilazwa sasa hapo ndio tutajua ila gharama za matibabu naziweza.

Mimi nilibahatika kufanya kazi nje ya nchi kwahiyo maisha haya yakujitegemea na kuishi mwenyewe katika umri huu hayanishtui sana kwasababu ndio maisha ya wenzentu huko.

Wao system zinawaandaa mapema kwasababu mtoto akishamaliza college hatakiwi kuishi na wazazi tena kwahiyo wanajua kabisa after some years kama wewe ni single parent utabaki mwenyewe kama ni couple mtabaki wenyewe.

Ila mimi nilikosea sehemu moja tu naregret kuandaa nyumba ya kustaafu kubwa na ukweli yalikua mawazo ya mama ambae sasa yeye ndio hapataki huku Tanzania'.

Tukaongea mambo mengine mengi ya maisha ya kazi, siasa za Tanzania na kadhalika lakini nikagundua nilichojifunza kupitia maisha ya huyu Mzee ni kikubwa sana hata kukitafakari.

Nikajikuta naondoka kwa Mzee saa mbili usiku na nimeamka najiuliza maswali magumu sana sijawahi kujiuliza.

"Je baada ya miaka kumi nitakua naishi na nani na mazingira gani?
Hawa naoishi nao watakuwepo hapa?
Je nitaweza kuishi mwenyewe ikibidi?
Nikiumwa nitajihudumiaje?
Nitakua na Bima ya afya?

Je nitapata wapi fedha za kunihudumia bila kumtegemea mke au mtoto au mtu mwingine?"

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa, wengi wako hivyo upweke wa nguvu. Watoto walisha anza kivyao. Wazee wa ulaya wana marafiki wa kupotezea muda kama vile kuimba kwaya, wale walevi kushinda bar. Na wapenda kusafiri kuishia trip kusafiri kwenye meli za utalii. Uzee ni baraka na bahati ya wachache. Hongera kwake. Huyo mke wake sasa hivi anashinda ndani kama mfungwa kwa baridi la UK.
 
Kuna ndugu yangu anamshangaa kaka yetu kwa nini amejenga jumba kubwa huku wamebaki wawili tu yeye na mke wake tu hata house girl hawana, wajukuu wapo kwa watoto wao, watoto nao wote ni watu wazima wana maisha yao. Mzee amestaafu anakula pensheni wawili tu kwenye jumba kubwa. Bora mtu ukajenga nyumba nzuri ndogo ya kuishi baada ya kustaafu. Nyumba isiyo na upweke
 
Sa we unafikir lifestyle ya huyo mzee ambae watoto wote wapo nje pamoja na mkewe ni sawa na sisi eti na uka amua utupe na ushauri kama huo au sio.mimi nina wake 3 na watoto 11 siwez kukosa kukaa na wajukuu swaini!
 
Hii hali ya upweke huwa inawakuta sana wanaume hasa wa kina baba wa kiafrika.

Kina baba tujitahidi sana kuweza kumingle na watoto wetu kucheza nao, utani kidogo, stories, n.k., haya mambo ya kuwa serious sana na watoto kuna siku nao watakuwa wakubwa wakianza kujitegemea wanakusahau kabisa sababu hawana memories na wewe.

Kuna mzee kastaafu namjua alipokuwa na mke wake nyumba ilikuwa inaapata sana ugeni wa watoto ila baada ya mke kufariki kabaki mzee peke yake, watoto wanakuja mara chache sana muda mwingi yupo mzee pekeyake.
 
Habari zenu wadau.

Napenda wote tujifunze kitu hapa kwa maisha halisi niliyojionea.

Nilikua naalikwa na Mzee mmoja jirani mstaafu ambaye atakua na miaka 73 au zaidi. Siku zote tukikutana amekua bila kumtegemea mke au mtoto au mtu mwingine?"

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Kwenye umri wangu huu wa 46, nimejigundu mimi ni bonge ya Fala. Airbnb inalipa sana kuliko nyumba yangu ya kuishi
 
Maskini mnatiana moyo, eti jumba kubwa la kifahari ukistaafu halifai, eti inaleta upweke, story ya kutunga hii na uongo mtupu, ukiwa maskini, hasa wa akili basi dunia hii utapata taabu sana, maana utakuwa bendera fuata upepo tu, nyumbu plus yaani, nyoko kabisa

Jumba kubwa la kifahari ndio huondoa upweke kuliko kijumba kidogo cha kubana kila kitu, of course upweke mkubwa huanzia akilini mwa mtu, sio jengo kubwa, but ukiwa na jengo dogo sana ndio tatizo na huleta upweke kwani hata parking ya gari shida au swimming pool hakuna, so mawazo ya kimaskini ndio tatizo hapa sio jengo kubwa la kifahari.
 
Back
Top Bottom