Je, hii ni hali ya kawaida kwa wale wenye uzoefu?

Seniweba

Senior Member
Apr 14, 2021
179
412
Saalam!

Wahenga walisema mficha maradhi kifo humuumbua, nami leo nimeona niweke wazi mambo yangu ili niweze kusaidiwa kupitia jukwaa hili ambalo kwangu limejipambanua kuwa suluhisho la matatizo mbalimbali katika jamii.

Nisiwachoshe ndg wasomaji niende moja kwa moja kwenye lengo mahususi. Mimi ni mtoto wa kwanza kwa mke wa kwanza (ambaye alishatangulia mbele za haki) wa mzee wangu. Baada ya mama yangu kufariki mzee alikaa miaka Kama mitatu hivi akaamua kuoa mke mwingine ambaye wamedumu nae kwa miaka kumi na minne, lakini hajazaa nae.

Na mamamdogo huyu kipindi anakuja kuishi na mzee alikuja na watoto wake wawili ambao mzee aliamua kuwalea Kama watoto wake kabisa.

Na mamamdogo kwa kuona mzee anavyowajari watoto wake, nae ametulea sisi vizuri hata Kama kulikuwa na vichangamoto vidogo ambayo ni Kama 5% tu ambayo kwangu niliona ni kawaida sana ukilinganisha na taabu wanazopitia watoto wengine kwa mama zao wakambo.

Ni miaka miwili nilikuwa masomoni mkoa mwingine ambapo ndipo asili yetu huko, kipindi hicho sikuwahi kurudi huku anakofanyia kazi mzee.

Sasa baada ya kurudi nimekuta mambo yanavyoenda sivyo, kumbe mzee kupitia influence ya mamdogo aliamua kujenga nyumba huko nyumbani kwa kina mamdogo (ukweni) na baadhi ya miradi mbalimbali ameanzisha huko na wameshahamia huko kabisa.

Sasa baada ya kufika na Mimi huko naona nikama vile mzee kadhamiria kukaa hukohuko maana naona anazidi kuongeza ujenzi huko.

Baba yangu huyu amekuwa na Imani kubwa kwangu na Mimi vilevile kwake, Sasa kwa haya yanayoendelea nashindwa kumwelewa.

Ijapokuwa na sisi ipo nyumba ambayo tulikuwa tunaishi awali, lakini sasa bado mambo yanayonitatiza ni Kama haya

Kwanini ajenge nyumba huko ukweni ilihali hana hata mtoto na huyo mwanamke?

Kwanini baadhi ya samani nyingi za ndani ya nyumba zihamishiwe huko?

Huku kujengajenga na kuanzisha miradi huko ni kwa ajili gani?

Je, ndugu wakitutembelea ndo wafikie huko kweli?

Naombeni ushauri wenu na neno kidogo juu ya hili wandugu.
 
Komaa uandae future yako na ndugu zako, hizi mali za urithi huwa zinasababisha mambo ya ajabu sana.

Unawezajikuta unaanza kuandamwa na majanga, kumbe watu washakupiga kindole, baada ya kuanza kuhoji hoji vitu.
 
Jihadhari usipoteze uelekeo wa kuimarisha kwako kwa kuhangaika na kwa mzee. Yeye ana kwake kwa sasa jitihada kubwa weka nyumbani kwako.

Hata kama akijenga wapi, ilimradi ndio anaishi pale, hapo ndio kwake na nyie mtapaita kwenu.
 
Hizo ni zake, kama bado unamtegemea na ni katika umri na hali halali ya kumtegemea, basi hakikisha unamkubusha kukupa huduma hizo kwa mujibu wa ubaba wake.

Kinyume na hapo, pambana na wewe ukatumie vyako utakavyo, pengine nawe utashikwa tu masikio na ke, sio jambo la kubwata sana kama hujavuka hiyo stage.

Muhimu mkumbushe mzee kuwa, mali zake ndo zinapaswa kumlea wakati hana nguvu, kama anakowekeza anakuamini, aendelee, hutahusika na yeye kwakuwa na wewe utakuwa na wewe wako pia.
 
N

Nashukuru sana, nitaufanyia kazi ushauri wako mkuu
 
Hizo ni zake, kama bado unamtegemea na ni katika umri na hali halali ya kumtegemea, basi hakikisha unamkubusha kukupa huduma hizo kwa mujibu wa ubaba wake.

Kinyume na hapo, pambana na wewe ukatumie vyako utakavyo, pengine nawe utashikwa tu masikio na ke, sio jambo la kubwata sana kama hujavuka hiyo stage.

Muhimu mkumbushe mzee kuwa, mali zake ndo zinapaswa kumlea wakati hana nguvu, kama anakowekeza anakuamini, aendelee, hutahusika na yeye kwakuwa na wewe utakuwa na wewe wako pia.
Na Mimi siyo kwamba nazitegemea mali zake, lakini wasiwasi yangu huyu mama ambaye Hana mtoto nae atamtunza kweli siku za usoni!
 
komaa uandae future yako na ndugu zako,hizi mali za urithi huwa zinasababisha mambo ya ajabu sana.

unawezajikuta unaanza kuandamwa na majanga,kumbe watu washakupiga kindole,baada ya kuanza kuhoji hoji vitu.
Vitu vingine havihitaji ujuaji au siyo?@@@
 
Na Mimi siyo kwamba nazitegemea mali zake, lakini wasiwasi yangu huyu mama ambaye Hana mtoto nae atamtunza kweli siku za usoni!

Hilo mwachie Mungu ndugu yangu, anaweza asimtunze hata kama wanaishi kwenye nyumba aliyojenga mzee, tena bila kujali kama wana watoto.

Haujaona wanawake wanawatoto na bado wanawafanyia vitimbi na vituko waume zao?

Kikubwa, kama kuna maelewano, mambo mengine waachie wenyewe kiongozi.
 
Na Mimi siyo kwamba nazitegemea mali zake, lakini wasiwasi yangu huyu mama ambaye Hana mtoto nae atamtunza kweli siku za usoni!
Hakuna wa kumtunza ila wewe. Unachoweza kufanya ni kuongea nae kwa sauti ya chini jinsi gani anaweza kukusaidia usimame kwa miguu yako bila kugusia makando yake kwa sasa! Ukiona mambo hayaendi mara mbili tatu, unamuwashia moto mara moja, unatembea zako kuparanganyika kwa nguvu zako.

Atakusahau na hatajali kwa kipindi fulani, akija kukumbuka, hana nguvu ya kufanya lolote, ameshapoteza kila kitu na ndo unakuwa muda wa wewe kumtunza sasa, hapo sasa kama hukuparanganyika vizuri, mtabaki kulaumiana na yaliyotokea nyuma yasiyo na msaada kwa wakati huo.
 
Ukileta fyoko Mama mdogo anakufyeka!Mimi shida yangu ni hela.Nitatafuta hela hadi nakufa.Mapenzi hapana,sina shida nayo kabisa.
 
Back
Top Bottom