Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.
Ndugu zangu watanzania;
Je, haya mazoea ya miaka mingi ya baadhi ya watu kuogea sabuni za kufulia ni sahihi kweli? Kama si sahihi, yana madhara gani kwa afya za watanzania hapo baadae?
Nimeamua kuandika haya kwa maana kwamba, tangia nianze kutazama TV sasa ni mwaka karibia wa 20 na sijawahi kuona hizi sabubi za kufulia kama vile mbuni, jamaa, kodrai pamoja na mshindi zikitangazwa kama ni sabuni za kuogea. Matangazo ya sabuni hizi yamekuwa yakiwaonesha akina mama wakiwa wanafua tu nguo hususan zile za watoto wadogo.
Sijawahi kuona tangazo likionesha mtu anaoga kwa kutumia sabuni za kufulia nguo jambo ambalo linamaanisha kwamba ndani ya sabuni hizi kuna kemikali maalum (detergents) kwa ajili ya kutoa uchafu katika nguo tu na sio kwa ajili ya mwili wa mwanadamu. Sasa huu utaratibu wa kuogea sabuni za kufulia, hususan za vipande ulitokea wapi?
Kwa miaka ya nyuma kidogo, kama sikosei basi ni mwaka 2017 au 2018 nilikuwa nikisikia kupitia matangazo ya redio pamoja na television khusiana na tangazo linalohimiza watu kutotumia dawa hovyo pasipo kupata ushauri wa daktari.
Katika tangazo lile walikuwa wanasisitiza kwamba sio kila homa ni malaria ikiwa na maana kwamba serikali ilikwisha gundua kuwapo na mazoea mabaya ya watanzania kupenda kujinunulia dawa kiholela pasipo kuthibitisha kama anaumwa ama la.
Yaaani homa tu ikimshika mtu hata kama ni homa inayotokana na mafua, basi mtu anakimbilia dukani kununua dawa mseto kisha anameza. Mimi ninafikiri hili la watu kupenda kuoga kwa sabuni maalum kwa ajili ya kufulia limeshamiri sana maeneo waishio watu wa kipato cha chini (uswahilini) na serikali inapaswa kutazama hili kwa jicho la pili.
OMBI LANGU: Wizara ya afya inapaswa kukemea kupitia matangazo ya kwenye media (Radio, Television, online platforms) watu kuogea sabuni za kufulia kama ambavyo walikuwa wanakemea matumizi holela ya dawa (sio kila homa ni malaria) pasipo kupata ushauri wa daktari.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.