Je, haya mazoea ya miaka mingi ya kuogea sabuni za kufulia ni sahihi kweli? Kama si sahihi, yana madhara gani kwa afya za watanzania hapo baadae?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
12,178
2,000
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Je, haya mazoea ya miaka mingi ya baadhi ya watu kuogea sabuni za kufulia ni sahihi kweli? Kama si sahihi, yana madhara gani kwa afya za watanzania hapo baadae?

images (11).jpg

Nimeamua kuandika haya kwa maana kwamba, tangia nianze kutazama TV sasa ni mwaka karibia wa 20 na sijawahi kuona hizi sabubi za kufulia kama vile mbuni, jamaa, kodrai pamoja na mshindi zikitangazwa kama ni sabuni za kuogea. Matangazo ya sabuni hizi yamekuwa yakiwaonesha akina mama wakiwa wanafua tu nguo hususan zile za watoto wadogo.

Sijawahi kuona tangazo likionesha mtu anaoga kwa kutumia sabuni za kufulia nguo jambo ambalo linamaanisha kwamba ndani ya sabuni hizi kuna kemikali maalum (detergents) kwa ajili ya kutoa uchafu katika nguo tu na sio kwa ajili ya mwili wa mwanadamu. Sasa huu utaratibu wa kuogea sabuni za kufulia, hususan za vipande ulitokea wapi?

Kwa miaka ya nyuma kidogo, kama sikosei basi ni mwaka 2017 au 2018 nilikuwa nikisikia kupitia matangazo ya redio pamoja na television khusiana na tangazo linalohimiza watu kutotumia dawa hovyo pasipo kupata ushauri wa daktari.

Katika tangazo lile walikuwa wanasisitiza kwamba sio kila homa ni malaria ikiwa na maana kwamba serikali ilikwisha gundua kuwapo na mazoea mabaya ya watanzania kupenda kujinunulia dawa kiholela pasipo kuthibitisha kama anaumwa ama la.

images (14).jpg

Yaaani homa tu ikimshika mtu hata kama ni homa inayotokana na mafua, basi mtu anakimbilia dukani kununua dawa mseto kisha anameza. Mimi ninafikiri hili la watu kupenda kuoga kwa sabuni maalum kwa ajili ya kufulia limeshamiri sana maeneo waishio watu wa kipato cha chini (uswahilini) na serikali inapaswa kutazama hili kwa jicho la pili.

OMBI LANGU: Wizara ya afya inapaswa kukemea kupitia matangazo ya kwenye media (Radio, Television, online platforms) watu kuogea sabuni za kufulia kama ambavyo walikuwa wanakemea matumizi holela ya dawa (sio kila homa ni malaria) pasipo kupata ushauri wa daktari.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
9,272
2,000
Maisha yetu ya shagala bagala ndio yanatusaidia hata yakija magonjwa mazito miili yetu inayaona mepesi.

Mtu anayekunywa maji ya special kila siku ukija kumpa maji ya bomba, chemchemi au ya mvua lazima augue.

Lakini mtu anayekunywa maji ya chemchemi mara nyingi unaweza kumlisha kinyesi na asidhurike.

Ndugu zangu msipende kuishi kizungu sana au kufuata taratibu zote za mashirika ya afya sababu hii itapelekea kinga za miili yetu kulemaa na mwisho tuje tuishi kama kuku wa kisasa

Yani msipende kinga zenu zakae kimazoeazoea! Kula chochote kinacholiwa na mwanadamu, kinywa chochote kinachonyweka na mwanadamu na wakati mwingine garagara kwenye tope kuua bacteria wabaya 😊

Sasa wewe jifanye una sabuni yako ya kuogea, una maji yako spesho ya kunywa, una vyakula vyako spesho nk, uone vile kikija kimbunga vile kitakusomba.

Simaanishi tuishi kama vichaa ila ukiwatazama vichaa utajifunza mengi sana
 
renamaizo

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
1,298
2,000
Tatizo ni mfumo wetu wa maisha watu wanachukulia vitu simplesimple tu unakuta unaenda kwenye nyumba ndoo zq kutumia hazijapangwa mtu anafulia ndoo io io anatumia kuogea huu sipend hii tabia na kuna wengine unakuta ndoo io io inatumika adi choon tena afadhal ww umesema mshindi kuna wengine wanaogea mpaka OMO

Tena sisi tunaokaa maeneo ya jiran na uswahilin ni balaa mtu unaoga sabun unatundika kwenye dirisha dogo la juu bafun watu wanaiba mpaka sabun nilichoka kwa kwel yaan sasa hv nikimaliza kuoga sabun naenda kuweka room

Yaan uku uswazi ni hatar tupu
 
jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
9,365
2,000
Maisha yetu ya shagala bagala ndio yanatusaidia hata yakija magonjwa mazito miili yetu inayaona mepesi.

Mtu anayekunywa maji ya special kila siku ukija kumpa maji ya bomba, chemchemi au ya mvua lazima augue.
Lakini mtu anayekunywa maji ya chemchemi mara nyingi unaweza kumlisha kinyesi na asidhurike.

Ndugu zangu msipende kuishi kizungu sana au kufuata taratibu zote za mashirika ya afya sababu hii itapelekea kinga za miili yetu kulemaa na mwisho tuje tuishi kama kuku wa kisasa

Yani msipende kinga zenu zakae kimazoeazoea! Kula chochote kinacholiwa na mwanadamu, kinywa chochote kinachonyweka na mwanadamu na wakati mwingine garagara kwenye tope kuua bacteria wabaya 😊

Sasa wewe jifanye una sabuni yako ya kuogea, una maji yako spesho ya kunywa, una vyakula vyako spesho nk, uone vile kikija kimbunga vile kitakusomba.

Simaanishi tuishi kama vichaa ila ukiwatazama vichaa utajifunza mengi sana
unashauri watu wasifuate maisha ya kizungu:-

1. Maisha ya kizungu ni kuogea "sabuni za kuogea" na ya kiafrika ni "kuogea sabuni za kufulia. ELIMU ELIMU ELIMU.

2. Maisha ya kiafrika ni "kunywa maji ya kisima yenye bakteria" na "maisha ya kizungu ni kunywa maji ya chupa yaliyopita purification method na kuondoa kalshamu iliyozidi ambayo inalegeza mifupa, inaleta matege kama watu wa Arusha-, inaozesha meno kwa kuwa na kalshamu nyingi?'

OMG, Tanzania tunahitaji elimu sana
 
Tuishi maisha ya kawaida ili tuweze kwenda sambamba na nature
 
Battor

JF-Expert Member
Mar 21, 2019
406
1,000
Mimi miaka kibao naziogea hadi leo nimeoga na hizo hizo na kati ya watu wanaojivunia ngozi zao na mimi ni mmoja wao. Kama kuna madhara tuelezane wadau tuelewe mapema.
 
jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
9,365
2,000
Tuishi maisha ya kawaida ili tuweze kwenda sambamba na nature
Maisha ya kawaida yanategemea mtu na mtu.

Kuna kiongozi anashangaa Meneja TRA kulipwa 15 milioni wakati kipindi cha kikwete walikuwa wanalipwa 45 milion.

Mbunge analipwa 11 milioni kwa mwezi na Daktari bingwa analipwa 2.5 milion kwa mwezi, yupi hapo aishi maisha ya kawaida?
 
Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
9,272
2,000
Maisha ya kawaida yanategemea mtu na mtu.

Kuna kiongozi anashangaa Meneja TRA kulipwa 15 milioni wakati kipindi cha kikwete walikuwa wanalipwa 45 milion.

Mbunge analipwa 11 milioni kwa mwezi na Daktari bingwa analipwa 2.5 milion kwa mwezi, yupi hapo aishi maisha ya kawaida?
Siongelei kipato cha mtu naongelea kuhusu afya zetu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom