Je, haya mazoea ya miaka mingi ya kuogea sabuni za kufulia ni sahihi kweli? Kama si sahihi, yana madhara gani kwa afya za watanzania hapo baadae?

Uwe unawaza nje ya box bs we jamaa....miaka yote tunaogea,nani ameshalalamikia madhara ya kiafya!?
 
Tangu 2012 nimekuwa nikiogea sabuni ya jamaa na sijawahi kupata madhara, kwangu mm ni sabuni bora kabisa kufulia na kuogea
 
Sabuni hizi wanazoziita za kuogea yaani za kishua madaktari wengi wanasema si nzur mana zina kemikali nyingi sana ila tunashauriwa tutumie hizi jamaa, mshindi na n.k kwa kuwa hazina kemikali nyingi tena mpk watoto wachanga wanashauri watumie hizo wakati wa kuoga kwanza hizo sabuni za kuogea zinachavua kali sana mda mwingine mpk kuleta mafua
point ila hizi za kuogea kemikali yenyewe ni iliyopo kwenye DETOL, sasa kama wewe unatumi detal kwanini uogope sabuni za kuogea?
 
Nilichugundua SABUNI KIGOMA au MAGADI ni sabuni nzuri kunyolea ndevu ni mwaka wa kumi sasa saloon hawanipati kwa jero jero za kunyoa ndevu na vipele havinitoki hata kidogo.
THE FUTURE IS IN YOUR HANDS, DISCOVER YOUR POTENTIAL.
LAUNDRY SOAP BARS ZIMENIOKOA NA MENGI.
 
Mimi miaka kibao naziogea hadi leo nimeoga na hizo hizo na kati ya watu wanaojivunia ngozi zao na mimi ni mmoja wao. Kama kuna madhara tuelezane wadau tuelewe mapema.
Hazina shida basi ushamba na ulimbukeni, watu walisha kuwa Barinwash na matangazo ya biashara
 
Hazina shida basi ushamba na ulimbukeni, watu walisha kuwa Barinwash na matangazo ya biashara
Kabisa na nina fikir maisha ni namna ulivyojizoesha mwenyewe.
Kuna namna wengine hawawezi kuishi vile unavyoishi wewe.
Mim nimejizoesha simple life style na kiukwel nayafurahia sana haya maisha hata hospital sikumbuki nilini nilikwenda.
 
Yanil leo ndiyo nimefahamu kuwa kuna watu wanaogea sabuni za kufulia
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Je, haya mazoea ya miaka mingi ya watu kuogea sabuni za kufulia ni sahihi kweli? Kama si sahihi, yana madhara gani kwa afya za watanzania hapo baadae?

View attachment 1648029

Nimeamua kuandika haya kwa maana kwamba, tangia nianze kutazama TV sasa ni mwaka karibia wa 20 na sijawahi kuona hizi sabubi za kufulia kama vile mbuni, jamaa, kodrai pamoja na mshindi zikitangazwa kama ni sabuni za kuogea. Matangazo ya sabuni hizi yamekuwa yakiwaonesha akina mama wakiwa wanafua tu nguo hususan zile za watoto wadogo.

Sijawahi kuona tangazo likionesha mtu anaoga kwa kutumia sabuni za kufulia nguo jambo ambalo linamaanisha kwamba ndani ya sabuni hizi kuna kemikali maalum (detergents) kwa ajili ya kutoa uchafu katika nguo tu na sio kwa ajili ya mwili wa mwanadamu. Sasa huu utaratibu wa kuogea sabuni za kufulia, hususan za vipande ulitokea wapi?

Kwa miaka ya nyuma kidogo, kama sikosei basi ni mwaka 2017 au 2018 nilikuwa nikisikia kupitia matangazo ya redio pamoja na television khusiana na tangazo linalohimiza watu kutotumia dawa hovyo pasipo kupata ushauri wa daktari.

Katika tangazo lile walikuwa wanasisitiza kwamba sio kila homa ni malaria ikiwa na maana kwamba serikali ilikwisha gundua kuwapo na mazoea mabaya ya watanzania kupenda kujinunulia dawa kiholela pasipo kuthibitisha kama anaumwa ama la.

View attachment 1648036

Yaaani homa tu ikimshika mtu hata kama ni homa inayotokana na mafua, basi mtu anakimbilia dukani kununua dawa mseto kisha anameza. Mimi ninafikiri hili la watu kupenda kuoga kwa sabuni maalum kwa ajili ya kufulia limeshamiri sana maeneo waishio watu wa kipato cha chini (uswahilini) na serikali inapaswa kutazama hili kwa jicho la pili.

OMBI LANGU: Wizara ya afya inapaswa kukemea kupitia matangazo ya kwenye media (Radio, Television, online platforms) watu kuogea sabuni za kufulia kama ambavyo walikuwa wanakemea matumizi holela ya dawa (sio kila homa ni malaria) pasipo kupata ushauri wa daktari.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Zimetukuza hizo,mbona safi tu hatujawahi pata madhara
 
Ila sabuni ya unga ya Omo inawasha hatari, ila kila mtu na ngozi yake
Jamani inatumika tu hakuna madhara maana malighafi wanazotumia Ni za kawaida KABISA.MFANO
CAUSTIC SODA.
CHUN I YA MAWE.
MAFUTA YA MAWESE KWA HIYO HAKUNA TABU KAMA MCHANGANYIKO HUO UMEFUATA VIGEZO NA MASHARTI YA VIWANDA KWA KUPITIA SHIRIKA LETU PENDWA LA SIDO NA TMDA
 
Back
Top Bottom