Kwani hadithi ya Yesu ilikuwaje?kwani Yesu hakutolewa kafara na MUNGU,Mungu anaweza kufanya chochote
1---Nani kakudanganya kwamba Mungu anaweza kufanya KITU CHOCHOTE hata cha kijinga ???
2--Nani kakudanganya kwamba Mungu anahitaji kutoa maisha ya Mtu (kafara) ili jambo fulani litimie??
3---Kama ni kafara je kwanini Mungu hakuwaambia mapema Yesu na Floyd kwamba angewatoa kafara kwa sababu fulani???
4---Mbona hao wote Yesu na Floyd walipokuwa wanatokewa hiyo unayoiita "kafara" walikuwa Wakilia kwa uchungu wa maumivu ya "kafara', Yesu alilia; Eloi Eloi lamasabachtan, na Floyd alilia; nashindwa kupumua.
5---Je ukiambiwa "kafara" hiyo unayoisifu ni ukatili dhidi ya binadamu utakataa??
6---Je, Kama ni kweli ni kafara kutoka kwa Mungu, watu wakisema Munguu ni katili watakuwa wamekosea ??? (Mungu hawezi kuwa katili aslan).
7---Je ungekuwa ni wewe, ungependa utolewe kafara kama huyo G, Floyd au Yesu???
8--- Je wale wanaotoa kafara kwa kuua watu kama Albino ili wapate dhahabu machimboni na utajiri wapo sahihi???
9--- Je watoto na ndugu na jamaa wa G. Floyd watakubaliana na wewe unaposema huyo mpendwa wao ni Mungu aliyemtoa kafara???
10---- Nabii Ibrahimu aliota anamchinja mwanaye wa pekee, na alipoamka asubuhi akataka kumchinja huyo mwanae kidhahiri lakini Mungu akamkataza na kumwambia achinje kondoo, kwa nini alimkataza na wakati huohuo, kwa mujibu wako, Yeye Mungu kamtoa kafara G. Floyd na Yesu "kafara" ??