Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,577
- 729,450
Nazungumzia dunia ya uhai? dunia inayoongelewa kwenye vitabu vyetu vya dini!
Tumekuwa na mada ihusuyo bustani ya Eden kimsingi binafsi imenisaidia kuongeza ufahamu.
Ni katika mada hiyo nimegundua kuwa historia ya dunia hasa kidini na kiimani inabebwa na mashariki ya kati na kwa sehemu Africa...inawezekana kabisa wazungu si wakazi wa dunia hii au walikuja baadae kabisa wakati maisha yakiendelea na inawezekana kabisa walitoka sayari nyingine.
Ukisoma habari za mnara wa babel( babylon tower) ukisoma habari za bustani ya eden ukisoma habari za Jerusalem na paradiso, habari za makabila 12 za Israel, mfalme suleiman na machimbo yake! Hifadhi kubwa ya urithi wa dunia na hata mafuta ghafi ni hapo middle East
Lakini pia inawezekana kabisa hata sodoma na gomora haikuwa mbali na hapo maana yake Ukiangalia hizo picha tu mwonekano wake utaona kabisa kama kuna watu walikula bhata basi ni hawa jamaa.
Mashariki ya kati ina role kubwa sana kwenye historia ya dunia yetu leo hii na ndio maana nikawaza kwa uwazi kabisa kuwa huenda ikawa ndio kitovu cha dunia ya uhai imani dini
starehe na hata dhambi
Hii kama ni kweli je hizi kabila nyingine zilitoka wapi? Je nazo ni uumbaji wa Mungu? Je kabla ya hawa wa middle East kuja wengine walikuwa wapi?wakifanya nini? Je hawa ndio wale wa mataifa waliotajwa kwenye Biblia takatifu?
Mniwie radhi kwa mapicha mengi mengi lengo lilikuwa ni kuleta ufafanuzi kwa haraka..picha hurahisisha mawasiliano. .na ndio maana hata baadhi ya picha hizi si halisi bali wajuzi walituchorea kile kilichosimuliwa na kuandikwa
Hizi ni picha na maelezo kidogo ya kile kilichofanyika Sodoma (sodom)na gomorah ilikuja kujulikana baadae au wazungu walikuja kuligeuza neno sodom kama ulawiti na ushoga...hii yote ni hapo hapo mashariki ya kati
Picha hizi za bustani zinazoning'inia za Babilon (hanging gardens of babylon) bado zinathibitisha watu wa mtaa huo walivyoharibika kwa starehe pengine kuliko kizazi kingine chochote na inawezekana kabisa hawa ndio makungwi wetu
Zilikuwepo pia bustani zenye manukato hapa guru wa mapenzi ndio walitoa darasa la mapenzi
Ukija kuangalia biashara na hata majanga mengine kama ya gharika ya wakati wa Nuhu na mengine yote ikiwemo vita na majanga ya kiasili mashariki ya kati kuna kitu cha ziada kuhusu uumbaji wa dunia hii