Je, Dunia ilianzia Mashariki ya Kati?

Je, Dunia ilianzia Mashariki ya Kati?

Ni muda mrefu tangu thread hii mkongwe Mshana Jr uanzishe.
Nikiwa huko Ulayae, nilipita pita sana katika makumbusho yao, hasa kwenye maktaba zao, nyingi kati allo ya hizo zipo restricted. Kwa kuwa nilisha kuwa raia wao kwa kuoa na kufanya kazi nchi kadhaa zao, hasa za kiutafiti, hivyo zuio halikunihusu sana. Nilijisomea mambo mengi ya kale. Wazungu waliyafatilia kwa undani sana tena very seriously tangu karne ya 12. Kunako karne za 16 hadi 19, au hadi Leo, bado wanafuatilia mambo huko MASHARIKI YA KATI, yaani nchi za IRAQI na IRAN kwa upekee, ingawa na zingine zipo. Kwa jina la ujumla the " MESOPOTAMIA". Huko ndiko kulikoanzia ustaarabu wote, I e, sayansi, maendeleo n.k. Hivyo hata dini zote hapa DUNIANI, msingi wake ni huko. Na chanzo cha asili ya kutokea kwa dunia yetu, kimeelezewa huko. Ni kweli, binadamu alifanyiwa " GENETIC ENGINEERING" hapa pande ya hii AFRIKA!
Haya yamefunuliwa kiasi katika kitabu cha " mtafiri wa mambo kale na mwandishi wa vitabu" katika moja ya vitabu vyake, hasa cha "The 12th Planet".
Ipo kama hadithi, lakini mengi ni facts.
Naomba tukisome na tuelewe between the lines. Wazungu sii wajinga kutumia trillions of money kuchimbua chini ili wapate kuona mambo kale kule MESOPOTAMIA.
Wamepata mengi, even the shuttle rockets/ships, engines, farming, botanicals things, etc.
Naomba tukisome na tuelewe between the lines. Wazungu sii wajinga kutumia trillions of money kuchimbua chini ili wapate kuona mambo kale kule MESOPOTAMIA.
Wamepata mengi, even the shuttle rockets/ships, engines, farming, botanicals things, etc💪🏿✔.
 
Ambaye ni Adam? Lilith? Eva? Au huyu wa Olduvai gorge? Je nafasi ya Babylon na Eden nk nk zinakaa wapi kwenye hili? Je Unazungumzia kwa muktadha wa historic world au pre-historic ?
Eden ni story ya kutungwa tu wa Wayahudi katika myths zao. Babylon ni jiji la kale zaidi duniani na mwanzo wa ustaarabu wa kale duniani wenye ushahidi mwingi wa kihistoria.
 
Eden ni story ya kutungwa tu wa Wayahudi katika myths zao. Babylon ni jiji la kale zaidi duniani na mwanzo wa ustaarabu wa kale duniani wenye ushahidi mwingi wa kihistoria.
waumini wa kidini wa kiasili na kihafidhina wanashikilia kuwa Edeni ilikuwa eneo halisi la kijiografia na kihistoria, wakitolea mfano maelezo ya Kitabu cha Mwanzo yanayotaja mito halisi ya Tigris na Eufrate, huku wakiamini kuwa kukana historia ya eneo hilo kunaharibu msingi mzima wa anguko la mwanadamu na hitaji la ukombozi.
 
waumini wa kidini wa kiasili na kihafidhina wanashikilia kuwa Edeni ilikuwa eneo halisi la kijiografia na kihistoria, wakitolea mfano maelezo ya Kitabu cha Mwanzo yanayotaja mito halisi ya Tigris na Eufrate, huku wakiamini kuwa kukana historia ya eneo hilo kunaharibu msingi mzima wa anguko la mwanadamu na hitaji la ukombozi.
Watu wanaweza kuamini chochote ila hakuna ushahidi wowote wa kihistoria wa uwepo wa bustani ya Eden, hiyo ni imani ya kwenye Biblia na Quran tu ambavyo sio vitabu vya Historia.
 
Watu wanaweza kuamini chochote ila hakuna ushahidi wowote wa kihistoria wa uwepo wa bustani ya Eden, hiyo ni imani ya kwenye Biblia na Quran tu ambavyo sio vitabu vya Historia.
Hebu thibitisha kwa facts kwamba ni simulizi za kufikirika ili tujengane kielimu na maarifa
 
Mashariki ya kati ndiko mambo ya dini yaliania huko,Jerusalem ni mji umetajwa katilka bibliia mara kibao.

Biblia ni kitabu kizuri ukikisoma kwa kuongozwa na roho matakatifu,utafahamu mengi wasiyoyajua wasomi.Kuonyesha kuwa mashariki ya kati ni muhimu kwa wakazi wa dunia hata Yesu alipoulizwa kwa dalili za mwisho wa dunia aliwaambai "iangalieni mashariki ya kati".

Kwa wale wafuatiliaji na wachunguzi wa mambo ya dini ukristo na uislam,kama unajua nini kinaendelea pale maeneo ulipo msikiti wa Al-aqsa kati ya wayahudi na wapalestina.Je jambo hilo litaishaje?Wayahudi wanatakiwa wajenge hekalu lao pale lakini kuna msikiti,hapo ndipo tunasema "mwacheni Mungu aitwe Mungu".Neno la Mungu ni lazima litimize kusudi lake.

Mshana jr na wengine wanaofahamu kuhusu mambo ya ulimwengu usioonekana naomba kuwauliza kuna mtu nilikuwa nadiscuss naye mambo mazito akaniambia katika kila mwezi kuna siku moja mwanadamu huwa hana ulinzi kabisa.Akasema siku hiyo unakuta mganga hatoki kwenye himaya yake anakuwa anategemea visaidizi fulani alivyoweka kwake.

Hili lina ukweli jameni?Mimi naamini Mungu (Jehova)anatulinda siku zote kama unamtegemea na unaenenda katika njia zake.
Hekalu ni nini kwani?
 
Naingia moja kwa moja bila kujali ujio wa mvua za El nino.
Katika pita pita zangu ndani kitabu cha "The 12th Planet" nimeongeza maarifa kathaa toka kwa watu wa kale wa "MASHARIKI ya KATI" , kumbe hata mambo haya ya unajim, wao, wa MASHARIKI ya KATI walishayapata tangu kale sana kwa kusona/kurithishwa na "Babu Zao" yaani "Wa - SUMERIAN"
Hawa ndiyo walifundishwa wa wale viumbe waliotua pale MASHARIKI ya KATI, wakaanza maisha, baadaye sana wakafanya"Genetic Engineering katika maabara zao na kutoa viumbe vilivyofanana na wao.
Basi, kwa mujibu wa The 12th Planet, hii ni sayari yao, nayo huzunguka JUA kwa mzunguko wa saa, wakati Sayari zote huzunguka kinyume cha saa.
Kumbe basi, Sayari yao inapokaribia kwenye"ORBITS" ya sayari zingine huweza kusababisha baadhi ya mabadikiko ya kama hali ya hewa n k. Hii hasa kwa dunia yetu.
Huenda hata hii El nino ikawa na dalili hizo, hasa mzunguko huu unapotukaribia - "PERIGEE " Bora unapokuwa mbali sana na Dunia yetu, yaani " APOGEE "
Wenzetu Wazungu wanalijua hili, ila hawataki kutuambia sisi.
Sayari hii/Nyota hii inapokaribia Dunia yetu, wakati wa juoni upande wa Magharibi, endapo una macho makali au kiona mbali, unaweza kuiona, wanasema, hung'aa sana, mwanga wa "Dark Red"
Kumbe sasa jibu kwa Mshana Jr, ni ndiyo, Mambo Yote Yalianzia MASHARIKI YA KATI.
NB: Naomba tulifuatilie hili kwa kufanya tafiti rahisi.
Kama to vile neno " EDEN" lina maana gani, I e, ardhi kavu, fuatilia neno hili, kwa kiingereza cha kale, kijerumani cha kale na mabila karibu yote ya MASHARIKI YA KATI. Sii neno hili tu, yapo mengi sana. Yalitokana na lugha ya Kwanza ya Ki - SUMERIAN, baadaye Ki - Kadiani, Ki - babiloni, Ki - Assyriani n k
 
Back
Top Bottom