SoC02 Je, Donald Trump alikuwa sahihi kufananisha Afrika na tundu la choo?

Stories of Change - 2022 Competition

Pamella

New Member
Nov 22, 2013
1
1
Kauli tata ilitoka kinywani mwa aliyekuwa Raisi wa Marekani awamu iliyopita Bwana Donald Trump ambayo ilisababisha taharuki na tafrani miongoni mwa wengi wapenda haki na amani duniani hasa kutoka Afrika. Hakika kwa mtazamo na hisia za kawaida kauli hii imesheheni udhalilishaji, dharau, ubaguzi na yenye kukera sana.

Pamoja na kuwa kauli hii haina staha lakini hebu tujitathmini kidogo. Je hali ikoje hapa nyumbani? Nadhani elimu ya uzalendo inahitajika sana. Misingi ya upendo, utu, uadilifu, utii n.k imetikiswa sana. Wachumia tumbo wanatafuna hela za Miradi mchana kweupe bila aibu, Waziri anakagua mradi wa maji uliogharimu Tsh milioni 600 anaonyeshwa kidimbwi. Baadhi ya askari polisi ndio majambazi siku hizi. Baadhi ya raia wanaharibu miundombinu kwa kung'oa na kuiba. Kuna watumishi wa umma wamejaa jeuri na dharau. Baadhi ya wanasiasa ni wabinafsi

Uzalendo ni dhana muhimu sana katika kuleta maendeleo endelevu na ya kudumu katika nchi. Nchi zilizoendelea sana watu wake ni wazalendo sana.

Maana halisi ya uzalendo ni upendo wa dhati kwa nchi yako, raia wenzako, lugha, utamaduni, mali nk zilizopo nchini. Upendo huu unadhihirishwa kwa vitendo na maneno ikiwa ni pamoja na kuisemea mazuri nchi yako ugenini.

Matukio ya ajabu yamekuwa mengi sana siku hizi. Hivi karibuni imeripotiwa polisi walimkamata mwanamziki fulani akiwa mazoezini asubihi kwaajili ya afya yake akifata maagizo ya daktari wake kule Iringa. Alipowasihi kupewa fursa ya kutaarifu mkewe na jirani zake walimkatalia wakamsomba na kumpeleka kituoni kwa kisingizio kwamba anahusika katika kesi ya mauaji ambayo kiukweli hakuwa anaifahamu. Alipojitambulisha kwao eti walimuamuru awaimbie alipowatii wakamwachia huru wakiwa tayari wameshamdhalilisha.

Je huu ni uadilifu kweli? Yapo mengi mabaya kuzidi haya yanayokera.

Dhana hii ambayo nimeiweka kwenye kitabu nilichokipa jina la " UZALENDO KWANZA: TUJENGE TANZANIA PAMOJA" ni pana sana.

Kitabu hiki ni zawadi yangu kwa watanzania hasa vijana na watoto wetu pamoja na watu wa umri, elimu na taaluma zote. Nimeandika kwa ligja nyepesi sana. Hakiuzwi kitapatikana bure hivi karibuni. Hii ni njia yangu ya kuonyesha uzalendo kwa vitendo kwa kutoa elimu hii bure ili tusibaki kudhalilika na tujenge Tanzania yetu.

Tembelea kiungo (link) hii hapa ili kuweza kupata maelezo yangu zaidi kuhusu dhana hii ya uzalendo


Nawapenda sana. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake wote.

IMG_20220427_113435_707.jpg
 
Back
Top Bottom