Kwa ushahidi huu Trump alikuwa sahihi aliposema Afrika inatakiwa kutawaliwa upya

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,863
Miaka 60 Baada ya Ukoloni wa Waafrika tumeendelea kulaumu Wazungu kwa umaskini na migogoro yetu, huku sisi wenyewe hakuna cha maana tunafanya kujikwamua na hali hii.

View: https://twitter.com/africaupdates/status/1719966249482891718?t=hTpdjN24uzeWV8BoTCW2vg&s=19
Just imagine Wazungu waliyoweka mipaka ya Afrika wameiondoa na kuamua kufanya biashara baina yao huku wakitega mitego yao ya kuendelea kuzoa Mali Afrika.

Screenshot 2023-11-03 093127.png

Waafrika tulivyo mbumbumbu tumeamua kushirikiana na wakoloni kuiba Mali zetu wenyewe ila hatutaki kushirikiana wenyewe kwa wenyewe kujenga uchumi wa nchi zetu!

Angalia hii hapa;
- Hakuna miundombinu ya kuunganisha Afrika na Afrika ila tunajenga reli na Bandari kuimarisha kusomba Mali zetu kwenda nje!

View: https://twitter.com/africaupdates/status/1717567065975054762?t=ZcT2erV7rNYlBKUiJMD91A&s=19

- Tumeweka vikwazo vya kufanya biashara baina yetu ila tunafurahia kuwaona Wazungu walitoka kwao kuja Afrika tena kwa Biashara za kawaida kabisa kama kuuza viatu, kuwinda, nk, ambazo tungeweza kufanya wenyewe.

- Ukitaka kusafiri Nchi ya Afrika ni kama unataka kwenda kwenye mwezi, ni complications na costly sana.

View: https://twitter.com/africaupdates/status/1720253510896308558?t=zxu20NsNacsbPp0I7uAvrw&s=19

My Take
Sijajua mtu mweusi anakwama wapi hasa kwenye kujitambua.

Mfano, leo hii ukiangalia takwimu hata za Utalii hapa Tanzania unakuta Waafrika ni wengi, karibu nusu licha ya ugumu wa kusafiri na mavisa na gharama za juu zilizopo. Sasa je, ukiondoa visa unadhani Utalii utainuka kiasi gani?

Waafrika tuache upumbavu, kama tutarihusu free movements watu wawe na IDs tu, sio tu tutakuza Biashara bali hata migogoro na watu wanaokukimbia Nchi zao kwenda Ulaya vitakoma.

Afrika ndio Bara lenye Mali na potential kuliko Bara lolote hapa Duniani ila shida hatuna akili, na wengi wa viongozi ya Afrika ni kama mazombie tu wasiojitambua.

Waafrika wanatakiwa kuelewa kwamba uhusiano na Wazungu ni wa kinyonyaji na sio vinginevyo kulingana na walivyo set toka ukoloni.

Hakuna siku umaskini utaisha bila kubadili hili na ili kubadili lazima Waafrika tuwe na ushirikiano wa kibiashara sio wa kufanya mikutano ya AU Addis Ababa.

Hongera sana Kagame na Ruto Kwa kubaini kinachokwamisha Maendelea ya Africa.

View: https://twitter.com/FactsOnRwanda/status/1720092860828233805?t=3KYFiz9JPKLTGzNPdB9pPQ&s=19

View: https://twitter.com/africaupdates/status/1720253982218625061?t=l7DTEvnXYQpcOzl8q-HPjg&s=19
 
bila ya Kanisa na huo unaoita ukoloni hali ingekuwq mbaya zaidi, kabla ya Ukristu watu wetu hata hawakujua nchi ni nini, hakukuwa na City yoyote kwa maana ya city kama tujuavyo leo kuna Arusha, Dar au Iringa, hivyo siyo kweli kwamba tunarudi nyuma, ukweli ni kwamba tumepiga hatua kubwa sana mbele thanks to chritianity of course, labda tip tu usijilinganishe na watu ambao hamlingani, angalia ulipokuwa na ulipo hapo ndipo pa kulinganisha …
 
ukristo ndio njia ya wazungu kuingilia Afrika kuja kuinyonya

na bora wasitutawale kwani wataleta ushoga kupitia hayo makanisa yenu
 
Sikubaliani na wewe
 
ukristo ndio njia ya wazungu kuingilia Afrika kuja kuinyonya

na bora wasitutawale kwani wataleta ushoga kupitia hayo makanisa yenu
Mashehe wangapi wamefumaniwa live misikitini na je kesi ngapi tunazisikia za mashoga kama siyo pwani huko? Bara kusikia ubasha, usenge ni baada ya miingiliano ama sivyo tungebaki hivyo tulivyokuwa kabla ya wakoloni kuja, tusingeusikia usenge kamwe. Waarabu ndo chanzo cha usenge. Uliza wasichana wanaoenda kufanya kazi oman, saudi na kwingineko wanafwanyweje na matajiri wao. Siyo wote but most of them.
 
ukristo ndio njia ya wazungu kuingilia Afrika kuja kuinyonya

na bora wasitutawale kwani wataleta ushoga kupitia hayo makanisa yenu

angalau hata unajua kuandika leo hii na grammar nzuri tu isitoshe wazungu wametawala Dunia nzima siyo afrika tu, hata China, India, Singapore, Vietnam walitawaliwa pia sasa iweje anyonywe mwafrika tu?
 
bila ya Kanisa na huo unaoita ukoloni hali ingekuwq mbaya zaidi, kabla ya Ukristu watu wetu hata hawakujua nchi ni nini, hakukuwa na City yoyote kwa maana ya city kama tujuavyo leo kuna Arusha, Dar au Iringa, hivyo siyo kweli kwamba tunarudi nyuma, ukweli ni kwamba tumepiga hatua kubwa sana mbele thanks to chritianity of course, labda tip tu usijilinganishe na watu ambao hamlingani, angalia ulipokuwa na ulipo hapo ndipo pa kulinganisha …
Ukkristo umeleta wizi na ushoga tu,'na mauaji,

Isitoshe dini iyo inakwapua ngawira toka kwa masikini na kuwatia ufukara
 
Africa haiwezi kuwa kitu kimoja hili ni bara la Giza , ELIMU ndicho tumekikosa tena yenye tija si ili mradi kwenda shule kama viongozi wetu wanavyofuatisha.
Trump naye debe tupu atuache na ujuha wetu tushazoea wenyewe maisha haya.
 
Ukkristo umeleta wizi na ushoga tu,'na mauaji,

Isitoshe dini iyo inakwapua ngawira toka kwa masikini na kuwatia ufukara

Labda uko sahihi lkn pia ulipaswa useme kabla ya ukristu hali ilikuwaje hapa kwetu kwani uislamu ulikuwepo kwa karibia miaka 800, kulikuwa na maendeleo yoyote ya waafrika ? mfano vitu vya msingi kama
Shule, maji safi ya kunywa, dawa hospitalini, vifo vya mama na watoto hali ilikuwaje?
 
Wewi ni mpumbavu mkubwa,Kwa hiyo hizo ripoti zinazosema intra Africa trade ni only 15% ni Ccm inatwala Afrika?

Nachokwambia unachokiona Tanzania Iko hivyo all over Afrika sababu ujinga kama ulioelezwa hapo Juu.
Sawa. On our part, hapa Tanzania wanaofanya tuonekane wajinga ni ccm.
 
Tazama "ujinga" huu. Uzi imenzishwa bila ya kuwa na elements zozote za udini; sasa anagalia upumbavu wa waafrika katika uchangiaji wa maada hii.. mara ooh waarabu wafiraji, mara ooh wazungu wameleta ushoga kanisani etc.. yaani Africa kuna ng'ombe nyingi sana za miguu miwili..
 
Back
Top Bottom