Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.
Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.
Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.
Akitangaza kujivua uanachama amesema,
Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.
Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.
VIDEO: