Je, Biblia ya ukweli/Halisi ni ipi?

Nimeisoma kwa kutulia, nimeona huo mkanganyiko wa vita ya kugombea kutambulika kwa chapisho fulani kati ya hayo mengi
Kimsingi sioni tatizo kwa muktadha wa kuwa dini na imani ni vitu vinavyoathiriwa na tamaduni, mila na desturi... Hivyo katika kueneza neno la Mungu kuna mahali kulipatikana upinzani wa kutaka kuongeza ama kupunguza kitu... Lakini bado msingi mkuu haujaathiriwa kabisa

Jr
 
Unataka kusema hii katiba inayotumika sasa Tz katika nchi yako imeandaliwa na kupitishwa na watu wanaojulikana na wananchi wamekubaliana nao?
 
Katiba inayotumika maadam ni msahafu wetu tuna uwezo wa kurekebisha mambo .Umeshasikia kamati ya kurekebisha biblia ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuuliza kama hii katiba inayotumika sasa imepitishwa na watu wanaojulikana na wananchi wamekubaliana nao? Hujajibu halafu unakimbilia kusema inawezekana kubadili baadhi ya mambo,wakati zoezi la katiba mpya tumeona kilichotokea.
 
Ni mila na desturi zipi zilizoharibiwa na zingesaidia vp katika kuleta maendeleo?
Hebu fafanua mkuu maana haya mambo huwa hamtoi ufafanuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna jamii yoyote katika ulimwengu isiyokuwa na mila na desturi zake. Kilichofanyika ni kuzivuruga ili tuzione hazina maana tukumbatie za kwao ili tufishwe kifikra. Na katika hilo walifanikiwa ndo maana wewe hapo ambaye ni zao la malengo yao unaendelea kuwatetea.
Tulikuwa na tiba zetu za asili ambazo zilisaidia sana kwenye afya. Wakajitahidi kuzififisha - lakini imekuja kugundulika kwamba hizo tiba zetu ndizo hizo sasa wanaboresha na kuturudishia kwa gharama kubwa sana.
1. Naamini unajua vyema kampuni ya DNLG wanatumia miti ipi kutengeneza dawa then wanapiga hela.
2. Naamini kama wewe ni mfuatiliaji unajua thamani ya mti wa mlonge ambao unaonekana ni mti wa kipekee kwenye tiba.
3. Kila kabila ilikuwa na namna yake ya kuabudu na kile walichokiabudu lilirudisha majibu tarajiwa. Niwe wazi katika hili ... huko mkoani Kagera ilikuwa mtu akikutenda ubaya ukamlilia Kaihula Nkuba - ilikuwa haipiti mwezi radi inashuka na kutoa tahadhari ili mtenda dhambi ajirudi.
Sijui kwenye makabila mengine lakini kote kulikuwa na utaratibu wa kuendesha ibada na kujiongoza ili jamii iendelee kustawi.
Ni mengi ambayo wamebeba na kufanyia kazi; utashangaa ukihitaji historia ya Karagwe unaipata Germany badala ya kuipata Karagwe penyewe. Leo hii ndo wanajitokeza wazungu wengine eti wanataka kuwekeza kwenye mambo ya makumbusho - hata huko kuna kitu wamelenga.
Kwa ujumla ukitaka kuiharibu jamii haribu historia yake, haribu mila na desturi zake - na katika hilo walifanikiwa
 
Hatuelewani , point ni watu wasiojulikana ila katiba watu wanajulikana ila ni upeo wa kufikiria katika kupokea hiyo katiba . Ni swala tu la umoja bila woga kudai katiba kulingana na maisha yetu . Angalia Kenya walivyofanya na wanaendelea kuichambua . Ila biblia ikisema rangi nyeusi ni nyeupe "ndio mzee" hakuna ubishi ! Hebu hoji kuhusu uumbaji wa Adam na Eva , utaitwa taahira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maneno ya Mungu na tafsiri ya maneno ya Mungu.
Maneno ya Mungu utayasikia kutoka ndani yako kwa sababu Mungu yuko ndani yako. Yule anayehubiriwa makanisani ni mungu wa deal. - toa ndugu toa - Mungu wa kweli anakuongoza kwenye kutambua mema na mabaya toka ndani yako. Hawa wanaotafsiri maneno ya Mungu ni deal tu. Ona walivyojimilikisha ardhi, mahekalu, vyuo n.k. kwa kivuli cha dini zao.
Hautakuja kuyajua hayo mpaka pale utakapokuwa umefunguka jicho la rohoni - jicho la tatu. Mnamchangia mchungaji / mtumishi wa mungu mahela wakati wahumini wanahangaika na maisha.
Imeandikwa Dini ya kweli ni hii - saidia wajane, maskini na yatima - mengine mbwembwe tu. Sio kwamba napinga dini ila kuna umuhimu wa kuchunguza kwa kina wanaosambaza hizo dini nyuma ya pazia wana nini?
 
Unazungumzia madawa yetu asili,unataka kusema kwa mfano wachina au wakorea hadi sasa wanatumia madawa na tiba zao za asili kwamba hawatumii tiba za kizungu kama tufanyavyo sisi waafrika?
 
Unazungumzia madawa yetu asili,unataka kusema kwa mfano wachina au wakorea hadi sasa wanatumia madawa na tiba zao za asili kwamba hawatumii tiba za kizungu kama tufanyavyo sisi waafrika?
Hapo umenipata - asilimia 75 ya wachina wanatumia madawa ya asili na wameboresha hadi wana viwanda vya kutengeneza madawa ya asili yasiyokuwa na chemicals;

Fuatilia Cuba waliokataa muingiliano na mataifa ya kufuata mlengo wa magharibi wana sifa zifuatazo:-
1. Vifo vya watoto na wajawazito viko chini sana kwa sababu wao hawaamini kwenye hizi chanzo zinazosambazwa kiholela.

2. Life span ya mcuba iko juu kwa sababu anatumia kile chenye manufaa kwa afya yake.

Njooo nchi za Afrika, Ebora, Ukimwi, Maralia, homa ya ini n.k yaani kumekuwa kama dampo la maradhi. Viongozi wetu wanakubali kila kitu pasipo kuuliza wataalam kama kina madhara au la!

Umeona kwenye tiba tu - hata nyimbo wasanii wetu wameishapoteza mwelekeo wa nyimbo za asili zao.
 
Haueleweki point yako hasa ni ipi? Ni kwamba biblia haijulikani imepatikana vp ama imetungwa na nani? Au kwamba biblia haifanyiwi maborekebisho?
 
Kwahiyo mkuu unataka kuniambia mimi nikienda china sehemu kubwa ya matibabu nitakayokutana nayo ni matibabu ya tiba za asili kuliko matibabu ya kizungu?
 
Mkuu mie nimezungumzia kuhusu maneno ya Mungu na tafsiri ya maneno ya Mungu,sasa hayo sadaka na wahubiri yanaingia vp kwa nilichokieleza?
 

Kuongeza ima kupunguza tbs hii hapa
sasa utuwekee Biblia Ambayo inaenda kinyume na maagizo hayo
Hata allah Ameitakasa Biblia Takatifu
sasa wewe usie jua kusomana kazi yako uongo na uzushi na kudhania


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nadhani hapo mwanzo niliweka rai kabisa huu uzi sio wa kidini na hakutakiwi kuwa na mijadala ya kukashifu dini za watu wala personal attacks otherwise uzi utahama kama mlivyoharibu ule uzi wa Book of Enoch

Hoja hapa ni Biblia gani ni sahihi kati ya vitabu 66,73 au 81?? Sasa hayo ya Quran hayajibu sababu hata hiyo Aya ya Quran haijasema hiyo Bible anayosema iko perfect ni ipi ya protestant?? RC au Tawahedo?? So bado haijajibu swali kabisa

Bottom line ni kwamba **** watu mnakuja na hoja kwamba Bible canon ilishushwa na Roho mtakatifu sasa nachojiuliza ina maana Roho mtakatifu anajipinga kiasi ashushe Canon tofauti kwa wakristo?? Na kama sio Je ina maana mmoja ndio yuko sahihi na wengine wamepotoka?? Na kama wengi wamepotoka nini hatma ya ukristo kama watu wamepotezwa miaka yote hii na hawajajikomboa??

Haya maswali ukiyajibu kisomi utakuwa umetusaidia ila ukiingiza udini hapa unakuwa hauna mchango wowote maana huwezi jua majibu yako yanaweza badili watu imani humu so jitahidi uwe positive kwenye mijadala yanayogusa imani yako.
 
Mkuu kwenye bible kuna mstari unasema hivi "kila neno lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho "
Kwa iyo wanaotumia vitabu vingi/ vichache wote wapo sawa.
....

Hawawezi kuwa sawa sababu wingi na uchache havifanani. Lazima kuna wengine watakuwa na ziada na wengine kinyume chake,tena ukizingatia suala nyeti la imani lenye kuangalia mustakabali wa waja na hatima yao. Hapa umakini wa dharura unatakiwa uchukue nafasi yake.
 
Hata allah Ameitakasa Biblia Takatifu

Hivi huwa unajisikiaje unapo andika uongo wa wazi ?

Kwanini unapenda kuizungumzia Qur'an wakati hujui chochote juu ya Qur'an ? Tazama ulichokiandika na kaisome tena hiyo aya ya 115 katika sura ya 6 (Al An'am). Utuonyeshe ni wapi imezungumzia ?

Umenukuu tena aya ya 24 katika sura ya 18 (Al Ahkaf). Jaribi kuwa mkweli hata kwa bahati mbaya. Aya zote zina zinaelezea utukufu wa Qur'an.

Sasa jaribu kujenga kielimu wala si kibubusa na kufanya ghishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…