HERY HERNHO
Member
- Mar 4, 2022
- 70
- 313
Urusi imechukua kiti cha urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa licha ya Ukraine kuwataka wanachama kuzuia hatua hiyo.
Kila baraza la wajumbe 15 huchukua nafasi ya urais kwa mwezi mmoja, kwa utaratibu wa kupokezana.
Mara ya mwisho Urusi ilikuwa na nafasi ya urais ilikuwa Februari 2022, na ndio ilianzisha uvamizi kamili wa Ukraine.
Ina maana kuwa Baraza la Usalama linaongozwa na nchi ambayo rais wake yuko chini ya hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa madai ya uhalifu wa kivita.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - ambayo si taasisi ya Umoja wa Mataifa - ilitoa hati ya Vladimir Putin mwezi uliopita.
Licha ya malalamiko ya Ukraine, Marekani ilisema haiwezi kuizuia Urusi kuwa mwanachama wa kudumu wa baraza kutwaa kiti cha urais.
Wajumbe wengine wa kudumu wa baraza hilo ni Uingereza, Marekani, Ufaransa na China.
Jukumu hilo mara nyingi ni la kiutaratibu, lakini balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzia, aliliambia shirika la habari la Urusi Tass kwamba alipanga kusimamia mijadala kadhaa, ukiwemo wa udhibiti wa silaha.
Alisema atajadili "utaratibu mpya wa ulimwengu" ambao, alisema, unakuja.chanzo bbc swahili