Naombeni kusadiwa kujua kuhusu majini. Nina imani watu wengi huwa tunatishwa sana..
Nina maswali naombeni kupewa msaada..
[emoji117] Nani aliwaumba majini?
[emoji117] Majini wameumbwaje na kwanini waliumbwa kwa kazi gani?
[emoji117] Kwanini hawaonekani nguvu gani au wao wapo ulimwengu gani hasa hadi tunashindwa kuwaona?
[emoji117]Je, vitabu vya dini vinasemaje kuhusu hawa viumbe ni sehemu gan majini watajwa na je mitume wa Mungu wamewahi kuwatumia hawa kwa kazi gani na kwanini?
[emoji117] Kwanini wanaonekana kuwa na nguvu zaid kuliko binadamu, mbinu ipi sahihi ya kuwadhibiti hao viumbe?
[emoji117] Je, maumbile yao halisi ni yapi na utawezaje kuwatambua?
[emoji117] Je, Mungu wanayemwamini ni huyu tunayemwamini sisi na huko watahesabiwa vipi haki siku ya mwisho na adhabu yao itakuwaje kwenye moto wa milele (nasikia wapo kama moto sina uhakika).
[emoji117] Je, wanaliana vip mimba zao hukaa muda gan na huishii miaka mingap tokea azaliwe yaani jin Mzee yupoje.
[emoji117] Mfumo wao wa utawala upoje na je kuna adhabu za kuwapatia endapo wanasumbua binadamu?
[emoji117] Je, wanaweza kuzaa na binadamu na mtoto akizaliwa huwaje?
Yaan dah yapo mengi maswali!
Naona wengi badala ya kukupa majibu wamehamia ktk malumbano ya kidini.
In shaa Allah nitajitahidi kukujibu walau kwa uchache Kama ifuatavyo : Swali lako la kwanza ni:
1)NANI ALIYE WAUMBA MAJINI?
Jibu: majini wameumbwa na Mwenyezi Mungu. Uthibitisho ni Qur 51:56 Allah aliposema:
"Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu mimi "
Pia 7:54 Qur an
" .... Fahamuni : kuumba (ni kwake tu Mwenyezi Mungu) na amri zote ni zake (Mwenyezi Mungu), ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote".
Pia Qur 30:26 inasema
"Na vyote vilivyopo mbinguni na ardhini humtii yeye.
Bila shaka huu ni ushahidi tosha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye ALIYE WAUMBA MAJINI NA VITU VYOTE UVIONAVYO ULIMWENGUNI.
2)
umeuliza WAMEUMBWAJE?
Jibu: wameumbwa kwa Moto. Ushahidi: quran 7:12
".....Akasema (iblisi) : mimi ni bora kuliko yeye, (mimi) umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo. "
Pia Qur 55:15
" Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto ".
Kwa hiyo MAJINI waliumbwa kwa moto.
3)
KWA NINI HAWAONEKANI
Jibu:
Ameitwa Jinni kwa sababu ya kutoonekana kwake na watu, hii ni kwa sababu kila kisichoonekana kwa jicho la binadamu ktk lugha ya kiarabu jina lake (hutoholewa) hutokana na herufi hizi (JIYM) na (NUUN).
Kwa mfano :bustani huitwa 'janna' kwa sababu ya kuzungukwa kwake na majani kila upande pasiweze kuonekana ndani.
Mfano wa pili. :Elimu ya uzazi huitwa 'Ilmul ajinna' kwa sababu ya kutoonekana kwake kile kilichokuwemo tumboni mwa mzazi.
Na majinni nao wamepewa hilo jina kwa sababu ya kutoonekana kwao kwa macho ya binadamu.
Ukichunguza hayo maneno 'JANNA' 'AJINNA ' na' JINNI' yana herufi ya JIYM na NUUN ndani yake.
4)
WANATAJWA WAPI KTK VITABU VYA DINI?
Jibu: Hawa majini wametajwa ktk Qur an na ktk biblia. Ktk Qur an wametajwa sehem tofaut tofaut na pia ipo sura inyowaelezea kwa kirefu, sura ya 72.
Pia ktk biblia wametajwa katika maeneo tofauti tofauti.
Mfano 1wafalme 13:17 walihusishwa na ujenzi wa nyumba ya nabii suleyman.
Pia ktk yuda 1:6-na 2kornto 11:14-15 biblia inawatambua majini km malaika waovu.
Ila ikumbukwe kuwa malaika waliumbwa kwa nuru na majinni kwa moto
Yuda 1:9 imemtaja kwa jina la "IBLIS" Kama alivyo tajwa ktk quran. Yuda 1:9 "lakini malaika mkuu alipo shindana na ibilisi na kuhojiana naye...."
Pia ufunuo 20:10 inasema ibilisi mwenye kuwadanganya watu atatupwa kwenye shimo la moto.
Hata ukisoma quran 6:128 inasema hao majini waovu na wafuasi wao wa kibinadamu wataingia Motoni.
(5)
NAMNA YA KUWADHIBITI
Jibu: kuwadhibiti kwake ni kwa kuisoma quran. Ukiisoma ayatul kursiy asubuh basi unajilinda nao tangu hiyo asubuh mpaka jioni yake.
Na pia Ukiisoma tena kwa hiyo jioni basi utajilinda dhidi yao mpaka asubuh yake.
kwa kifupi pendelea kuisoma hii ayatul kursiy In shaa Allah Mwenyezi Mungu atakuepusha nao.
(6)
MAUMBILE YAO HALISI
Jibu: Mtume (swalla Allahu 'Alayhi wa sallam) amesema:
"majini wako namna tatu, namna moja wana mabawa wanaruka na (namna) nyingine majoka na ng' e na hawapendi kuashiria mahala pamoja na hupenda kuhama".
Atw-twabraaniy na Al-haakim na Al-Bugharary.
(7)
WANAAMINI MUNGU GANI?
Jibu: miongoni mwao wapo walio silimu na walio Baki kwenye ukafiri ambao ndio huwapotosha binamu ili waende nao Motoni siku ya mwisho .
Quran 72:14 "nasi wapo miongoni mwetu walio silimu, na wamo miongoni mwetu walio kengeuka. Walio silimu hao ndio Walio tafuta uongofu
Kwa hiyo ktk wao majini wapo miongoni mwao walio silimu na waka mwamini Mwenyezi Mungu huyu tunaye mwamini wanadamu. Nao wakitenda mema basi watalipwa Kama watakavyo lipwa wanadamu watendao mema. Na wale waovu nao watalipwa Kama ilivyo kwa wanadamu watendao waovu.
(8)
WATAADHIBIWA ADHABU GANI?
Jibu: Majini waovu wataadhibiwa adhabu ya moto. Uthibitisho ni quran
6:128 "Na ile siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya Majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi Katika wanadamu.
Na marafiki zao katika wanadamu waseme: Mola wetu! Tulinufaishana sisi na wao, na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea
Basi Mwenyezi Mungu atasema: moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako niwenye hekma na mwenye kujua.
Pia rejea Ufunuo 20:10
"Na Yule ibilisi mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti alimo Yule mnyama na Yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku Hata milele na milele "
(9)
JE WANAWEZA KUZAA NA BINADAMU
Jibu : Ndio quran 18:50 inaonyesha kuwa ana kizazi chake (generation) pia quran 17:64 yaonyesha kuwa anauwezo wa kuzaa na mwanadamu
Rejea visa vya majini mahaba
Utapata kuelewa zaidi Juu ya hili.
Yangu ni hayo, km kuna sehemu nimeenda wrong basi wataalam watanisahihisha