Uislamu kuna uongo na ukweli sio hoja yangu Mkuu, sina haja ya kuingilia hayo mm. Mi nko naitafuta tu kweli iniweke huru na kimsingi nimeshaipata. Wala haiko ktk dini zenu hizi, ila nabii Issa aka Yesu au Masiya, kanuni zake kama zilivyoainishwa na Bible ni bora sana. Nazikubali,binadamu wote tungezishi maisha duniani yangekuwa na maana saana.
Mwingine ni Buddha,, huyu na Yesu tofauti zao utazitafuta kwa tochi mkuu. Unapata logic ya mengi ktk falsafa zao. Niko naendelea na Quran, ila hadi nilipofikia Muhammad alikuwa mtu mwema kwa ndugu zake tu...... Ana mafundisho tata mengi sana, labda bado sijamjua sana, na hapa duniani hana wafuasi kwa siku hizi.
Kama ulifuatilia post zote kwa makini, kuna post nilikwambia hata wanyama mawe na mimea pia wana chembe za ukristu. Ukristu ni yote yaliyo fundishwa na Kristu, na si vinginevyo. Si haya madhehebu haya tuyaonayo. Ingawa hata huko atakaye yashika mafundisho vyema, atakuwa mzuri. Mungu ni UPENDO, dini ni UPENDO, kanuni kuu ni UPENDO, sheria kuu ni UPENDO,,,, ili kufikia hapa, mtendee jirani yako vile upendavyo wewe kutendewa. Jirani hapa si mkristu mwenzako au mtanzania, au binadamu au mammals mwenzako, bali ni chochote chenye KUTHIRIKA na matendo yako.
Mfano we ni dereva, uko barabarani unadrive, mbwa anakatisha. Yesu anakwambia umtendee huyo mbwa kama vile we ungependa kutendewa. Kanuni ni fupi saaaana, badilishaneni viatu tu, we vaa vya mbwa na mbwa mpe vyako, then jiulize ungependa binadamu akufanyiaje we mbwa ukiwa unakatisha barabara? Jibu lako ndo ukipaswacho kumtendea mbwa.
Huu ndo ukristu, ndo Ukweli wa maisha na ndo maana ya kuishi na dhima ya kuishi. Mungu alitaka maisha yawe hivyo, maisha ya viumbe yanategemeana, binadamu anategemea mimea, anamtegemea hata nzi na mbu ktk kuishi kwake. Viumbe vyote ni bora, UPENDO kwa vyote.
Tatzo hapa, kanuni za kiislamu. Jinsi mtu anavyoubobea ndivyo uso wake unavyopoteza nuru ya UPENDO. Wenye akili hujiuliza kwanini? Majibu ya maswali hayo ndo yamefikisha hapa ktk mjadala huu wa leo tangu asubuhi.