Je, Adhabu Shule ya Msingi ni Child abuse?

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
295180_360278660712790_608140936_n.jpg
 
hii imetulia, kimsingi adhabu ni njia mojawapo ya kumfanya mwanafunzi au mtoto kutambua makosa yake na kujirekebisha. Ila adhabu iliyo bora ni kumpa mtoto/mwanafunzi adhabu ya kufanya chochote kwa mikono yake au akili yake, mf.kulima, kupalilia bustani, kufagia, kufyeka uwanja, kudeki darasa nk badala ya kuchapa (hii ni njia ya kikoloni zaidi) adhabu nilizotaja na zingine zinazofana na hizo ni nzuri kwani humjenga mtoto vizuri na pia humsaidia kujifunza jambo ambalo humsaidia ktk maisha ya baadae. Mf.mimi nimesoma sekondari na shule niliyosoma hakukuwa na kuchapwa, ni adhabu za kufanya kazi mbalimbali tu. Hii ilinijenga sana kisaikolojia na kujiamini zaidi ktk mambo ninayoyafanya. Hivyo changamoto kwa walimu na wazazi ni kuchagua adhabu ya kumpa mtoto kulingana na kosa lenyewe. Na sio kuchapa fimbo. Pia kutokumpa mtoto adhabu kama upuuzi wanaotuletea wazungu ni kujenga taifa lenye kiburi, lisilo na utii, lisilo sikivu, na lililo jaa jeuri. Wazazi na walimu msitake wazungu na mashirika yanayoingia kwa kigezo cha kutetea haki ya watoto kupandikiza dhana hii kwani hawana nia nzuri. Mtoto hawezi kuachwa tu akakua hivi hivi bila kuwa shaped. Tukumbuke mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Nawasilisha.
 
Hizo adahabu zinakiuka misingi ya kibinaadamu wala hazina ulazima hata chembe.

Kuadhibiwa hakumfanyi mtoto kuwa na nidhamu na kutoadhibiwa hakumfanyi mtoto kupotoka
 
hii imetulia, kimsingi adhabu ni njia mojawapo ya kumfanya mwanafunzi au mtoto kutambua makosa yake na kujirekebisha. Ila adhabu iliyo bora ni kumpa mtoto/mwanafunzi adhabu ya kufanya chochote kwa mikono yake au akili yake, mf.kulima, kupalilia bustani, kufagia, kufyeka uwanja, kudeki darasa nk badala ya kuchapa (hii ni njia ya kikoloni zaidi) adhabu nilizotaja na zingine zinazofana na hizo ni nzuri kwani humjenga mtoto vizuri na pia humsaidia kujifunza jambo ambalo humsaidia ktk maisha ya baadae. Mf.mimi nimesoma sekondari na shule niliyosoma hakukuwa na kuchapwa, ni adhabu za kufanya kazi mbalimbali tu. Hii ilinijenga sana kisaikolojia na kujiamini zaidi ktk mambo ninayoyafanya. Hivyo changamoto kwa walimu na wazazi ni kuchagua adhabu ya kumpa mtoto kulingana na kosa lenyewe. Na sio kuchapa fimbo. Pia kutokumpa mtoto adhabu kama upuuzi wanaotuletea wazungu ni kujenga taifa lenye kiburi, lisilo na utii, lisilo sikivu, na lililo jaa jeuri. Wazazi na walimu msitake wazungu na mashirika yanayoingia kwa kigezo cha kutetea haki ya watoto kupandikiza dhana hii kwani hawana nia nzuri. Mtoto hawezi kuachwa tu akakua hivi hivi bila kuwa shaped. Tukumbuke mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Nawasilisha.

Mkuu kwa hili nitaomba kupingana na wewe,kumpa mtoto adhabu kama kulima, kuchota maji,kufyeka uwanja au kutengeneza bustani binafsi sikubaliani nazo kwani kisaikolojia mtoto atakua akijua kwamba shughuli hizo ambazo ni sehemu ya maisha kuwa ni adhabu na wala usishangae siku utakayowapeleka watoto kutengeneza bustani ya shule kisha wakakuuliza kwani mwalimu tumekosa nini?Kwa kawaida adhabu inatakiwa kuwa motisha hasi itakayomfanya mtoto ajirekebishe makosa aliyoyafanya..
 
Hi nimesha wahi kuifanya wakati ninasoma darasa la 4 shule ya msingi miaka 40 iliyopita hahahah umenikumbusha mbali. Mbuzi Mzee
Heheee hii inanifanyaga nimkumbuke jamaa yangu tukiwa A-Level ye alipitisha mikono kinyume lol ikawa haifikii masikio halafu mwalimu akawa anamchapa kuwa anafanya makusudi wakati jamaa kagangamaa sana
 
Back
Top Bottom