Je, rufaa hukatwa wakati unatumikia adhabu au kabla ya kutumikia adhabu?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,040
Najaribu kujiuliza japo sio Mwanasheria Je RUFAA yoyote hukatwa baada ya kuanza kutumikia Adhabu uliyopewa au kabla ya kutumikia Adhabu? WABUNGE

Halima Mdee na Genge Lake Wamepewa adhabu ya kufukuzwa uanachama na Kamati kuu ya Chama chao Adhabu hiyo huenda sambamba na kuvuliwa Ubunge mara moja pindi Taarifa ya Kuvuliwa Uanachama inapofika Bungeni kwa SPIKA kwa Mujibu wa Katiba ya Nchi inayosema Mbunge hupoteza Sifa ya kuwa Mbunge akifukuzwa na Chama chake.Ili waonekane wameanza kutumikia Adhabu Bunge lilipaswa mara moja kuwavua Ubunge kwa Mujibu wa KATIBA ya Nchi.

Baada ya Kuvuliwa Ubunge Kama walikuwa na NIA ya kukata RUFAA ndio WANGEKATA.Kwa Maajabu ya NCHI hii na BUNGE LAKE ,Halima na Genge Lake licha ya Kufukuzwa Uanachama na Bunge kupewa Taarifa lakini hakuna Utekelezaji wowote wa kuwavua Ubunge Kama KATIBA inavyoelekeza . Binafsi naweza kufananisha Tukio hili na kuwa WAMEKATA RUFAA kabla ya kutumikia ADHABU Je wanakata RUFAA ya NINI wakati hawana Adhabu yoyote wanayoitumikia? Kama ni UBUNGE bado wanaendelea nao.

Naomba Wanasheria mtupe elimu ya Rufaa hukatwaa wakati gani je wakati unatumikia ADHABU au Kabla ya kuanza Kutumikia Adhabu kwamba ukishindwa RUFAA ndio utumikie Adhabu uliyopewa.Kwa Halima na Genge Lake ni Wazi Wamekata Rufaa kabla ya kutumikia Adhabu na endapo watashindwa Rufaa ndio Waitumikie Adhabu yao ya KUFUKUZWA UANACHAMA .
 
Kinachofanyika sasa ni kubuy muda ili msimu huu upite wakamilishe ubunge wao. Ila ikija kuthibitika hata hapo baadaye kuwa ubunge wao haukuwa halal, vipi maamuzi yaliyopitishwa na bunge wangali hao wakiwa bungeni, yatakuwa na uhalali gani kisheria.
Kama ilivyokuwa kwa maamuzi ya kesi, ushiriki wa wajumbe wa kamati kuu kwenye baraza kuu kumebatilisha maamuzi ya baraza kuu... je ushiriki wa wabunge Batali (kama itathibitishwa hata baada ya miaka 6) hakutabatilisha maamuzi yote ya bunge kipindi wakiwapo bungeni??
Hapa kwa mimi ndio ninapoona kwa nini kuna nguvu kubwa inatumika kuwalinda.
 
Raia na vyombo vya dola wanatakiwa kuheshimu na kulinda sheria na katiba kwa wivu mkubwa na gharama yoyote ile. Hii ina maana ya kuwashughulikia viongozi wanaovunja au kuidharau katiba.

Viongozi wa serikali, bunge na mahakama hawako juu ya sheria na katiba ambayo ni sheria mama.

Hata hivyo, kwa sababu ya kukosekana kwa wananchi imara wanaoweza kusimamia, kutetea katiba na kuwadhibiti viongozi, uvunjifu wa katiba huonekana ni jambo la kawaida.
 
Kuna Mzee aliwahi kumsema
Kichwa Cha Mwendawazimu Huwa kiatumiwa na Vinyozi kujifundishia kunyo

Kweli Sasa nimeamini
Hili Bunge ni mfano halisi wa kichwa Cha Mwenda Wazimu

Ilianza enzihizo ila nakumbuka kinyozi Mwanafunzi mmoja Rip Mzee Six alifanikiwa kunyoa fasheni ya Kiduku ambayo ilikubalika na Taifa lilimpa Maua yake
 
Tanzania hakuna mahakama Wala majaji,bali kundi kubwa la vilaza na pumbumbu.

Nilipo anza kuwa mfuatiliaji mzuri wa shughuli za kimahakama,niligundua mambo ya kijinga katika field ya sheria ambayo hata mtu mpumbavu hawezi fanya upumbavu kama uliopo kwenye field hiyo.
 
Mimi ni mwanasheria wa kijiweni. Ninavyofahamu kuwa wanachama 19 waliofukuzwa na CHADEMA kisheria lazima watoke Bungeni kwanza. Kama ni rufaa wakate wakiwa nje ya Bunge. Kama wakishinda rufaa yao basi itabidi warudi Bungeni na walipwe marupurupu yote kama sheria inavyotamka. Nitoe mfano, Kama ukiwa na kesi na kashindwa kesi na ukafungwa kama utakata rufaa basi rufaa hiyo utaikata ukiwa bado uko Magereza mpaka hapo rufaa yako itakaposikilizwa na uamuzi kutolewa kama umeshinda kesi utatoka au kama hukushinda kesi utaendelea na kifungo. Hii ya akina Halima ni kituko cha mwaka.
 
Back
Top Bottom