Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,114
- 34,957
Mkuu Mbuzi Mzee hii sasa kali kupitazote itakuwa huko ushenzini india huko hahahahahahh
Last edited by a moderator:
Mkuu Mbuzi Mzee hii sasa kali kupitazote itakuwa huko ushenzini india huko hahahahahahh
Mkuu kwa hili nitaomba kupingana na wewe,kumpa mtoto adhabu kama kulima, kuchota maji,kufyeka uwanja au kutengeneza bustani binafsi sikubaliani nazo kwani kisaikolojia mtoto atakua akijua kwamba shughuli hizo ambazo ni sehemu ya maisha kuwa ni adhabu na wala usishangae siku utakayowapeleka watoto kutengeneza bustani ya shule kisha wakakuuliza kwani mwalimu tumekosa nini?Kwa kawaida adhabu inatakiwa kuwa motisha hasi itakayomfanya mtoto ajirekebishe makosa aliyoyafanya..
Mimi natofautiana na wewe kwa hoja zifuatazo: kwanza hujanipa mbadala wa adhabu nyingine kama hizi hazimfai mtoto. Pia, mtoto anapopewa adhabu, kwa mtazamo wangu mimi, ni kuwa unamwita, unamworodhoshea makosa yake na kumwambia kuwa hilo ni kosa na anastahili adhabu. hivyo atakuwa anafahamu ni kwa nini anafanya adhabu hiyo. ofcourse si kila wakati kwani hakuna aliye mkamilifu, mara nyingine inafaa kumuonya kwa maneno tu, na kama atakuwa hasikii basi hapo ndipo adhabu inabidi kutolewa. Hii ni tofauti na kazi kama kazi. kwani kama wewe ni mzazi mzuri ambaye unakaa vizuri na familia yako, ni lazima utakuwa unawafundisha watoto maana na umuhimu wa kufanya kazi yoyote ile haijalishi ni ipi. na pia ni lazima umfundishe mtoto kukosa maana yake nini, na ni kwa nini ni muhimu na wajibu wa mzazi kumuonya mtoto pindi anapokosa. Mimi sikupingi ukija na hoja mbadala lakini natoa angalizo tu kuwa kama familia yako mtoto atakuwa anafanya kosa alafu unamwacha tu bila kutoa adhabu, wewe kama mzazi utakuwa unafanya kosa sana, na utakuwa unapingana na maagizo ya Mungu. Ila yote ya yote, watoto wanapaswa kupewa maonyo ya mdomo mara kwa mara na adhabu zisiwe nyingi na za mara kwa mara. Hii itawajenga vizuri. Mkubwa mimi naongelea experience, nimekulia ktk familia ya namna hiyo na hadi nimekuwa mkubwa sikuwahi kuwa na mawazo hasi kwa wazazi wangu na walimu kutokana aina ya adhabu walizonipa (nawashukuru sana na nawakumbuka sana kwa hili kwani wali shape future yangu). Pia nina mifano ya familia ambazo watoto walikuwa wakikosa hawapewi adhabu yoyote-kifupi tunasema walidekezwa. ndugu yangu nikikuonesha familia hizo kwa sasa utaelewa ninachosema hapa. sikulazimishi ukubali ninachosema lakini ukweli utabaki kuwa ukweli daima.
nakaribisha mada zaidi kwani hii mada tamu sana.
Asante sana mkubwa kwa uchambuzi wako na pia namshukuru mwalimu kwa kunipongeza hapo.Nikijaribu kusoma haya uliyoyaorodhesha hapo sipingani na hata moja.Kwani ni kweli kabisa kuwa sijatoa adhabu mbadala.Na vilevile tumetofautiana kidogo kwani mimi nimetoa mtizamo wangu kama mwalimu na wewe umebase zaidi katika familia.Kimsingi adhabu ziko nyingi sana na hakuna mtoto yeyote yule mtukutu ambaye anastahili kuachwa bila maonyo yanayofuatiwa na adhabu.Adhabu za kifamilia zinatofautiana kwa kiasi kikubwa na adhabu za shuleni,kwa mfano hakuna adhabu inayomuumiza mtoto kama kumnyima kile kitu anachokipenda(mf.wakati wenzake wanaenda mapumzikoni wewe unambakiza darasani na kuhakikisha anakosa muda wa kucheza japo kwa wiki nzima)au kumfanyisha kitu ambacho hakipendi(mf.kama hapendi kazi za darasani basi unampa karatasi hata kumi za kuandika kwa kurudia makosa yake mpaka amalize)Ila kwa upande wa familia umejaribu kuelezea vizuri lakini nitabakia katika msimamo wangu uleule kuwa shughuli za kawaida katika maisha ya mwanadamu zisitumike kama adhabu kwani hiyo itakuwa ni motisha hasi kwa mtoto.Shughuli kama hizo zinaweza kutolewa pale tu ambapo mazingira ya mtoto hayatampeleka kutegemea shughuli hizo katika maisha yake ya kila siku,kwa mfani mtoto aliyekulia mjini wewe kama baba utakapomuadhibu kwa kumpeleka shambani kwako na kumpatia kipande hiyo itakuwa ni stahili yake na si mtoto wa kule kwetu Maswa.Yeye ukimpa adhabu kama hiyo moja kwa moja utakuwa umedhavurugia utaratibu kwani hiyo ndio shughuli atakayoitegemea maishani mwake na atakua akiiona kama ni adhabu.Karibu tuendelee.
hii imetulia, kimsingi adhabu ni njia mojawapo ya kumfanya mwanafunzi au mtoto kutambua makosa yake na kujirekebisha. Ila adhabu iliyo bora ni kumpa mtoto/mwanafunzi adhabu ya kufanya chochote kwa mikono yake au akili yake, mf.kulima, kupalilia bustani, kufagia, kufyeka uwanja, kudeki darasa nk badala ya kuchapa (hii ni njia ya kikoloni zaidi) adhabu nilizotaja na zingine zinazofana na hizo ni nzuri kwani humjenga mtoto vizuri na pia humsaidia kujifunza jambo ambalo humsaidia ktk maisha ya baadae. Mf.mimi nimesoma sekondari na shule niliyosoma hakukuwa na kuchapwa, ni adhabu za kufanya kazi mbalimbali tu. Hii ilinijenga sana kisaikolojia na kujiamini zaidi ktk mambo ninayoyafanya. Hivyo changamoto kwa walimu na wazazi ni kuchagua adhabu ya kumpa mtoto kulingana na kosa lenyewe. Na sio kuchapa fimbo. Pia kutokumpa mtoto adhabu kama upuuzi wanaotuletea wazungu ni kujenga taifa lenye kiburi, lisilo na utii, lisilo sikivu, na lililo jaa jeuri. Wazazi na walimu msitake wazungu na mashirika yanayoingia kwa kigezo cha kutetea haki ya watoto kupandikiza dhana hii kwani hawana nia nzuri. Mtoto hawezi kuachwa tu akakua hivi hivi bila kuwa shaped. Tukumbuke mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Nawasilisha.