Jawabu kwa Lord Denning: Mikataba mithili ya IGA inayotaja gharama halisi za miradi ipo hapa Tanzania

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1690700410390.png

Picha ya antena za Vodacom, Tigo, Airtel na TTCL zikiwa zimesimikwa kwenye mnara wa Helios baada ya makampuni haya kusaini mkataba wa upangishaji na Helios

I. Utangulizi

Makubaliano ya Kiserikali kati ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari za Tanzania yanaongozwa na Sheria za Kimataifa, Katiba ya Taifa la Tanzania, Sheria za Kitaifa zilizotungwa na Bunge la Tanzania, na mikataba mbalimbali inayoongozwa na sheria hizi.

Mikataba muhimu ni pamoja na mkataba wa IGA, mkataba wa HGA, mikataba ya wakandarasi, mikataba ya mikopo ya mabenki, na kadhalika, kama mchoro ufuatao unavyoonyesha:

1690826887153.png

Mchoro: Uhusiano kati ya Tanzania, Dubai, Kampuni zitakazotekeza miradi, na mikataba husika

Katika mazingira haya, kuna mtu, Lord Denning, ameuliza swali lifuatalo: Je, kuna mkataba wa IGA ambao uliwahi kusainiwa kati ya pande bili wnye kutaja gharama halisi za miradi kama vile bei ya huduma na kodi ya pango?

Jawabu kwa swali hili ni "ndiyo," na ufafanuzi ufuatao ni kwa ajili ya kuthibitisha hilo.

II. IGA na HGA ni mikataba mtambuka (framework contracts)

Mikataba ya IGA na HGA ni mikataba mtambuka, yaani "framework contracts." Kimsingi, mkataba mtambuka unaweza kuwa na sura mbili.

Kwanza, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi unafahamika, kiasi kwamba ikishasainiwa HGA hakuna haja ya mikataba mingine.

Mfano mzuri ni ule mradi wa bomba la mafuta linalounganisha Tanzania na Uganda, yaani mradi wa EACOP.

Pili, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi haufahamiki kikamilifu, kiasi kwamba, kushasainiwa kwa HGA hakuondoi haja ya mikataba mingine. Mchoro ufuatao unatoa picha kubwa kuhusu aina hii ya mikataba mtambuka:

1690821715629.png

Na tatu, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unatambuka miradi tofauti inayotekelezwa ndani ya nchi ile ile moja, lakini miradi hiyo inatekelezwa kwa nyakati tofauti, katika maeneo tofauti na watekelezaji tofauti, lakini pasipo ulazimma wa kubadilisha sheria za nchi husika, kiasi kwamba kusainiwa kwa "Framework Contract" pamoja na "Project Contracts" kunaondoa mahitaji ya mikataba mingine, na hivyo kuondoa sababu ya uwepo wa IGA na HGA. Mchoro ufuatao unafafanua zaidi.

1690821438357.png

Kwa kifupi, tunaweza kusanifu hoja ifuatayo juu ya uhusiano uliopo kati ya "mkataba mtambuka," unaoitwa IGA" na "mkataba wa HGA"

Mosi, mkataba mtambuka (framework contract) ni mkabata wa jumla kati ya pande mbili, mfano, kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Uganda; kati ya serikali ya Tanzania na taasisi ya kimataifa isiyo nchi kama vile Benki ya Dunia; au kati ya kampuni ya usafirishaji na kampuni ya mafuta.

Pili, mkataba mtambuka (framework contract) kati ya serikali na serikali, unaitwa "Intergovernmental agreement (IGA)" au "Heads of States Agreement (HSA)" au "Bilateral International Treaty (BIT)."

Tatu, na kwa hiyo, kimuundo, IGA, HGA na BIT zinafanana kwa sababu zote zinao muundo wa mkataba mtambuka (framework contract).

Nne, kuna mkataba mtambuka (framework contract) kati ya kapuni ya Vodacom inayotoa huduma za simu and kampuni ya HELIOS inayojenga na kukodisha minara ya masafa,

Na tano, tukipata mkataba mtambuka (framework contract) kati ya Vodacom na Helios, tunakuwa tumepata mfano hai wenye kuonyesha muundo wa mkataba wa IGA, unavyopaswa kuwa.

III. Mkataba kati ya Helios na Vodaco ni mifano hai wa mikataba mtambuka isiyohitaji IGA wala HGA

Hapa nchini, kuna mifano mingi ya "mikataba mtambuka" ya aina hii ya pili. Mikataba hii inaonyesha gharama halisi za miradi husika, hata kabla mikataba ya miradi husika kusainiwa. Mifano mizuri hapa Tanzania ni kama ifuatavyo:
  1. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na kampuni ya Vodacom,
  2. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Tigo,
  3. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Airtel,
  4. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya TTCL.
  5. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Halotel.
Makampuni ya Halotel, Vodacom, Tigo, Airtel, na TTCL hutoa huduma za mawasiliano ya simu.

Lakini makapuni haya hayana mitaji ya kutosha kwa ajili ya kujenga minara nchi nzima.

MInara ya kurusha mawimbi ya sauti (signal relay stations) huhitajika kwa ajili ya kusimika antena za kupokea na kurusha upya mawimbi ya sauti kutoka kwa mpigaji hadi kwa mpokeaji.

Lakini, Helios ni kampuni ya Uingereza yenye mtaji wa kujenga na kukodisha minara kwa makapuni mbalimbali.

Helios wanamiliki minara zaidi ya 1000, katika Afrika mashariki na Kati. Hivyo, haya makampuni yetu yanakodisha nafasi kwenye minara ya Helios ili yaweze kuweka antena zao kwenye minara hiyo, na kuwahudumia wateja wake.

Kampuni inapoanza kukodisha nafasi kwenye minara ya Helios inakuwa haijui kwa uhakika inahitaji minara mingapi na iliyo wapi.

Kwa hiyo, busara ni kukodisha minara ya Helios kwa awamu, kulingana na wateja wanavyopatikana na wanakopatikana.

Hivyo, mchakato wa kuingia mkataba kati ya kampuni ya Helios na kampuni kama vile Vodacom inachukua hatua nne. Yaani:
  1. Kusainiwa kwa mkataba mtambuka mmoja (framework contract) wenye kutaja taarifa chache za jumla, zitakazoweka singi wa mikataba ya saiti moja moja katika siku za usoni.
  2. Kampuni yenye mahitaji kuiandikia Helios ikiomba huduma ya kukodishwa mnara kwenye site mpya.
  3. Kusainiwa kwa mikataba ya saiti maalum (site cocntract), na hivyo kuongeza idadi ya minara ya Helios iliyokodishwa kwa kampuni pale tu mahitaji ya kampuni yanapoongezeka kwa sababu wateja wapya wamepatikana.
  4. Helios kuandaa mnara kwenye saiti kulingana na mahitaji, na hatimaye kampuni kukabidhiwa saiti hiyo.
Kwa ujumla, mikataba mtambuka kati ya Kampuni ya Helios na makampuni yaliyotajwa hapo juu, inafanana katika muundo na maudhui.

KImsingi, kila "mkataba mtambuka" kati ya Helio na kampuni yoyote hapo juu, una sehemu zifuatazo:
  1. Maelezo ya msingi kuhusu makubaliano: Sehemu hii inaongelea wahusika katika mkataba, malengo ya wahusika, na mwongozo wa jumla kuhusu mahusiano ya siku za usoni.
  2. Kiammbatanisho cha kwanza ("schedule 1"): Kinaongelea "configuration", yaani aina ya huduma ambazo Helios anapaswa kuhakikisha zinapatikana kwenye kila saiti. Mfano:-- kuna sharti kwamba, kama mnara unaotaka kukidishwa uko sehemu ambako hakuna umeme wa gridi ya Taifa, basi Helios aweke jenereta; -- kuna sharti kwamba, kampuni itapewa ukubwa wa eneo la meta moja ya mmraba kwa ajili ya kusimika antena yake; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba tambuka; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba mahsusi utakaosainiwa katika siku za usoni; -- na kadhalika.
  3. Kiambatanisho cha pili ("schedule 2"): Kinaongelea kodi ya pango inayotajwa kwa kutumia kizio cha "TZS/site/month". Gharama hizi ziko katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yenye umeme wa gridi ya Taifa (bei nafuu). Na Kundi la pili ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yasiyo na umeme wa gridi ya Taifa (bei kubwa).
  4. Kiambatanisho cha tatu ("schedule 3"): Kinaongelea muundo na maudhui ya mkataba utakaosainiwa kwa ajili ya kukidisha saiti moja tu, yaani kukodisha mnara mmoja pekee. Kwa hiyo, kama kampuni ya Vodacom itakodisha minara 100, kutasainiwa mikataba mahsusi 100.
  5. Kiambatanisho cha nne ("schedule 4"): Kinaongelea utaratibu wa kuongeza mnara mpya, yaani jinsi kampuni yenye mahitaji itakavyowasiliana na Helios na kuonyesha huduma ya mnara mpya ianze kutolewa lini.
  6. Kiambatanisho cha tano ("schedule 5"): Kinaongelea utaratibu wa kukabidhiana huduma kwenye saiti.
  7. Kiambatanisho cha sita ("schedule 6"): Kinaongelea protokali ya kutumia saiti, maana kwenye mnara mmoja kuna wakodishaji wengi. Yaani, unakuta kuna antena za Tigo, Airtel, Vodacom, na kadhalika.
IV. Hakuna haja ya IGA kati ya Tanzania na Dubai

Baada ya kusema hayo hapo juu sasa nafanya majumuisho muhimu kwa kuzingatia hoja yafuatayo:

Njia mojawapo ya kusanifu hoja, ni kuanzia kwenye ufanano wa vitu viwili (argument by analogy). Njia hii huzalisha hoja yenye muundo wa kimantiki ufuatao:
  1. Kitu X na kitu Y vinafanana kwa sababu kila kimoja kinazo sifa kadhaa zinazounda seti Z.
  2. Kitu X pia kinaonekana kuwa na sifa nyingine P.
  3. Kwa hiyo, kitu Y pia kinapaswa kuwa na sifa hiyo P.
Kwa kutumia mantiki hiyo hapo juu, sasa tunaweza kumjibu Lord Denning kikamilifu kama ifuatavyo:

Mosi, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza na kammpuni ya DPW kutoka Dubai zinafanana katika sifa zifuatazo:
  • zote ni Kampuni za wawekezaji wa Kigeni;
  • zote zinaotaka mazingira yenye utulivu wa kisheria na kisiasa kwa ajili ya uwekezaji ili wafanikiwe kuwekeza, kuvuna na kuhamisha faida kutoka nchini Tanzania;
  • zote zinahitaji kimilikishwa ardhi kwa ajili ya kuitumia kama saiti ya miradi yake;
  • na zote zinajenga saiti zinazoitwa minara, kuziboresha na kisha kukodisha nafasi yenye eneo maaluma kwa muda fulani kwa makampuni kadhaa. Kwa upande mmoja, HELIOS wanasimika minara na kuikodisha kwa makampuni yanayosafirisha mawimbi ya simu hapa Tanzania. Kwa upande mwingine, DPW wanajenga saiti zinazoitwa bandari, kuziboresha na kuvikodisha kwa watu wanaosafirisha mizigo kwa kutumia meli.
Pili, Kampuni ya HELIOS kutoka Uingereza inayo sifa ya ziada kwa sasa, yaani uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutumia "mkabata mtambuka" (framework agreement) ambao ni mwavuli wa "mikataba ya miradi mingi," kila saiti ya mnara ikiwa na mkataba wake (project site agreements), lakini pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Uingereza wala kuhitaji mkataba wa HGA kati ya Helios na serikali ya Tanzania.

Tatu, kwa hiyo, Kampuni ya DPW kutoka Dubai inapaswa kuwa na uwezo wa kuendesha biashara zake kwa kutummia "mkabata mtambuka" (framework agreement) pamoja na "mikataba ya miradi mahsusi" (project site agreements), pasipo kuhitaji mkataba wa IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai wala mkataba wa HGA kati ya DPW na serikali ya Tanzania.

Nne, kuipa kampuni ya DPW unafuu unaotokana na mikataba ya IGA na HGA na kuzinyima unafuu huo kampuni baki za wawekezaji wa kigeni ni ubaguzi usio na sababu za msingi dhidi ya baadhi ya wawekezaji wa kigeni.

Na tano, kwa hiyo, kwa ajili ya kutenda haki sawa kwa wawekezaji wote wa kigeni, Tanzania inapaswa kuepuka mikataba ya IGA na HGA.

V. Hitimisho na mapendekezo

Mkataba mtambuka (framework contract) kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba kati ya nchi na nchi (IGA). Na mkataba wa saiti kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba wa ngazi ya miradi kati ya nchi mwenyeji na mwekezaji wa kigeni (HGA).

Kwa hiyo, inawezekana, na ni lazima, kutaja gharama za mradi kama vvile kodi ya pango na pia ukomo wa muda kwenye IGA.

Na kama ambavyo Helios na makampuni ya simu yanasaini "Framework Agreements" na baadaye "Project Site Agreements," vivyo hivyo DPW na TPA wanaweza na wanapaswa kusaini nyaraka za aina hii.

Hakuhitajiki IGA wala HGA kamwe ili kuiwezesha DPW au kampuni yoyote iwayo kuwekeza katika bandari za Tanzania!

Mama Amon Desk
"Summbawanga Town"
Sumbawanga.
30 Julai 2023.
 
... kama ambavyo Helios na makampuni ya simu yanasaini "Framework Agreements" na baadaye "Project Site Agreements," vivyo hivyo DPW na TPA wanaweza na wanapaswa kusaini nyaraka za aina hii.

Hakuhitajiki IGA wala HGA kamwe ili kuiwezesha DPW au kampuni yoyote iwayo kuwekeza katika bandari za Tanzania!

Mama Amon Desk
"Summbawanga Town" ...

Mama Amon kiasi umepotoka kulinganisha mkataba tambuka wa kampuni kwa kampuni na wa nchi kwa nchi. Hata vile ufafanuzi wako umetoa picha halisi ya tofauti ya mkataba tambuka (IGA )na wa utekelezaji (HGA) kimataifa.

Nakubaliana nawe kuwa TPA na DP World, kwa kuwa tayari wamesaini MoU, waingie kwenye mikataba ya utekelezaji (HGAs) ambayo italindwa na sheria za nchi husika kupitia IGA yenye vifungu vyenye "nipe-nikupe", kulinda maslahi ya Mataifa yote.

Pamoja na pendekezo langu hilo, hoja yangu kuu Serikali iweke na kutekeleza mikakati ya kuwezesha makampuni ya ndani ya kuwekeza na wageni watumike tu kiubia kuongeza ufanisi na tija. Kuendelea kutegemea mataifa ya kigeni, kwa maendeleo, ni kudumisha ukoloni-mamboleo
 
Nakubaliana nawe kuwa TPA na DP World, kwa kuwa tayari wamesaini MoU, waingie kwenye mikataba ya utekelezaji (HGAs) ambayo italindwa na sheria za nchi husika kupitia IGA yenye vifungu vyenye "nipe-nikupe", kulinda maslahi ya Mataifa yote.

Pendekezo hili hapana! Uthabiti wa sheria zetu za PPP, Ardhi, Kodi, n.k. zinatosheleza mahitaji ya wawekezaji wa kimataifa.

Hazihitaji kuongezewa nguvu yoyote kutokana na IGA au HGA. DPW na TPA wasaini Fraework Contract, halafu Project Contracts zitafuata kadiri mahitaji yatakavyojitokeza.

Hakuna sababu ya IGA wala HGA, isipokuwa kama hatuelewi maana na umuhimu wa state sovereignty, hasa baada ya historia chungu ya European extrcative colonialism iliyotanguliwa na Arab settler colonialism.
 
Mama Amon kiasi umepotoka kulinganisha mkataba tambuka wa kampuni kwa kampuni na wa nchi kwa nchi. Hata vile ufafanuzi wako umetoa picha halisi ya tofauti ya mkataba tambuka (IGA )na wa utekelezaji (HGA) kimataifa.

Katika aya hii umetoa tamko lisilo na utetezi. Napata shida kulijibu. Kwa nini unafikiri nimepotoka? Nijibu baada ya kusoma nukuu ifuatayo:

IGA na HGA ni mikataba mtambuka (framework ontracts)

Mikataba ya IGA na HGA ni mikataba mtambuka, yaani "framework contracts." Kimsingi, mkataba mtambuka unaweza kuwa na sura mbili.

Kwanza, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi unafahamika, kiasi kwamba ikishasainiwa HGA hakuna haja ya mikataba mingine.

Mfano mzuri ni ule mradi wa bomba la mafuta linalounganisha Tanzania na Uganda, yaani radi wa EACOP.

Pili, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi haufahamiki kikamilifu, kiasi kwamba, kushasainiwa kwa HGA hakuondoi haja ya mikataba mingine.

Mchoro ufuatao unatoa picha kubwa kuhusu aina hii ya mikataba mtambuka:

1690671381597.png

Na tatu, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unatambuka miradi tofauti inayotekelezwa ndani ya nchi ile ile moja, lakini miradi hiyo inatekelezwa kwa nyakati tofauti, katika maeneo tofauti na watekelezaji tofauti, lakini pasipo ulaiza wa kubadilisha sheria za nchi husika, kiasi kwamba kusainiwa kwa "Framework Contract" pamoja na "Project Contracts" kunaondoa mahitaji ya mikataba mingine, na hivyo kuondoa sababu ya uwepo wa IGA na HGA.
 
We
View attachment 2702526
Picha ya antena za Vodacom, Tigo, Airtel na TTCL zikiwa zimesimikwa kwenye mnara wa Helios baada ya makampuni haya kusaini mkataba wa upangishaji na Helios

Kuna mtu, Lord Denning, ameuliza swali lifuatalo: Je, kuna mkataba mithili ya IGA iliyosainiwa kati ya Tanzania na Dubai unaotaja gharama halisi za miradi kama vile bei ya huduma na kodi ya pango?

Jawabu kwa swali hili ni "ndiyo," na ufafanuzi ufuatao ni kwa ajili ya kuthibitisha hilo.

IGA na HGA ni mikataba mtambuka (framework ontracts)

Mikataba ya IGA na HGA ni mikataba mtambuka, yaani "framework contracts." Kimsingi, mkataba mtambuka unaweza kuwa na sura mbili.

Kwanza, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi unafahamika, kiasi kwamba ikishasainiwa HGA hakuna haja ya mikataba mingine.

Mfano mzuri ni ule mradi wa bomba la mafuta linalounganisha Tanzania na Uganda, yaani radi wa EACOP.

Pili, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unahusu mradi unaotambuka nchi nyingi katika utekelezwaji wake na utekelezwaji wake unahitaji maamuzi ya kiserikali na kibunge kwa kufanya mabadiliko ya sheria kadhaa katika nchi zote husika, ambapo wigo wa mradi haufahamiki kikamilifu, kiasi kwamba, kushasainiwa kwa HGA hakuondoi haja ya mikataba mingine.

Mchoro ufuatao unatoa picha kubwa kuhusu aina hii ya mikataba mtambuka:

View attachment 2702564

Na tatu, mkataba mtambuka unaweza kuwa mtambuka kwa sababu unatambuka miradi tofauti inayotekelezwa ndani ya nchi ile ile moja, lakini miradi hiyo inatekelezwa kwa nyakati tofauti, katika maeneo tofauti na watekelezaji tofauti, lakini pasipo ulaiza wa kubadilisha sheria za nchi husika, kiasi kwamba kusainiwa kwa "Framework Contract" pamoja na "Project Contracts" kunaondoa mahitaji ya mikataba mingine, na hivyo kuondoa sababu ya uwepo wa IGA na HGA.

Mifano ya Mikataba mtambuka isiyohitaji IGA wala HGA

Hapa nchini, kuna mifano mingi ya "mikataba mtambuka" ya aina hii ya pili. Mikataba hii inaonyesha gharama halisi za miradi husika, hata kabla mikataba ya miradi husika kusainiwa. Mifano mizuri hapa Tanzania ni kama ifuatavyo:
  1. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na kampuni ya Vodacom,
  2. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Tigo,
  3. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Airtel,
  4. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya TTCL.
  5. Kuna "mkataba mtambuka" (framework contract) kati ya kampuni ya HELIOS na na kampuni ya Halotel.
Makampuni ya Halotel, Vodacom, Tigo, Airtel, na TTCL hutoa huduma za mawasiliano ya simu.

Lakini makapuni haya hayana mitaji ya kutosha kwa ajili ya kujenga minara nchi nzima.

MInara ya kurusha mawimbi ya sauti (signal relay stations) huhitajika kwa ajili ya kusimika antena za kupokea na kurusha upya mawimbi ya sauti kutoka kwa mpigaji hadi kwa mpokeaji.

Lakini, Helios ni kampuni ya Uingereza yenye mtaji wa kujenga na kukodisha minara kwa makapuni mbalimbali.

Helios wanamiliki minara zaidi ya 1000, katika Afrika mashariki na Kati. Hivyo, haya makampuni yetu yanakodisha nafasi kwenye minara ya Helios ili yaweze kuweka antena zao kwenye minara hiyo, na kuwahudumia wateja wake.

Kampuni inapoanza kukodisha nafasi kwenye minara ya Helios inakuwa haijui kwa uhakika inahitaji minara mingapi na iliyo wapi.

Kwa hiyo, busara ni kukodisha minara ya Helios kwa awamu, kulingana na wateja wanavyopatikana na wanakopatikana.

Hivyo, mchakato wa kuingia mkataba kati ya kampuni ya Helios na kampuni kama vile Vodacom inachukua hatua nne. Yaani:
  1. Kusainiwa kwa mkataba mtambuka mmoja (framework contract) wenye kutaja taarifa chache za jumla, zitakazoweka singi wa mikataba ya saiti moja moja katika siku za usoni.
  2. Kampuni yenye mahitaji kuiandikia Helios ikiomba huduma ya kukodishwa mnara kwenye site mpya.
  3. Kusainiwa kwa mikataba ya saiti maalum (site cocntract), na hivyo kuongeza idadi ya minara ya Helios iliyokodishwa kwa kampuni pale tu mahitaji ya kampuni yanapoongezeka kwa sababu wateja wapya wamepatikana.
  4. Helios kuandaa mnara kwenye saiti kulingana na mahitaji, na hatimaye kampuni kukabidhiwa saiti hiyo.
Kwa ujumla, mikataba mtambuka kati ya Kampuni ya Helios na makampuni yaliyotajwa hapo juu, inafanana katika muundo na maudhui.

KImsingi, kila "mkataba mtambuka" kati ya Helio na kampuni yoyote hapo juu, una sehemu zifuatazo:
  1. Maelezo ya msingi kuhusu makubaliano: Sehemu hii inaongelea wahusika katika mkataba, malengo ya wahusika, na mwongozo wa jumla kuhusu mahusiano ya siku za usoni.
  2. Kiammbatanisho cha kwanza ("schedule 1"): Kinaongelea "configuration", yaani aina ya huduma ambazo Helios anapaswa kuhakikisha zinapatikana kwenye kila saiti. Mfano:-- kuna sharti kwamba, kama mnara unaotaka kukidishwa uko sehemu ambako hakuna umeme wa gridi ya Taifa, basi Helios aweke jenereta; -- kuna sharti kwamba, kampuni itapewa ukubwa wa eneo la meta moja ya mmraba kwa ajili ya kusimika antena yake; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba tambuka; -- kuna kifungu kinataja ukomo wa muda wa mkataba mahsusi utakaosainiwa katika siku za usoni; -- na kadhalika.
  3. Kiambatanisho cha pili ("schedule 2"): Kinaongelea kodi ya pango inayotajwa kwa kutumia kizio cha "TZS/site/month". Gharama hizi ziko katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yenye umeme wa gridi ya Taifa (bei nafuu). Na Kundi la pili ni bei za kukodisha mnara ulioko kwenye maeneo yasiyo na umeme wa gridi ya Taifa (bei kubwa).
  4. Kiambatanisho cha tatu ("schedule 3"): Kinaongelea muundo na maudhui ya mkataba utakaosainiwa kwa ajili ya kukidisha saiti moja tu, yaani kukodisha mnara mmoja pekee. Kwa hiyo, kama kampuni ya Vodacom itakodisha minara 100, kutasainiwa mikataba mahsusi 100.
  5. Kiambatanisho cha nne ("schedule 4"): Kinaongelea utaratibu wa kuongeza mnara mpya, yaani jinsi kampuni yenye mahitaji itakavyowasiliana na Helios na kuonyesha huduma ya mnara mpya ianze kutolewa lini.
  6. Kiambatanisho cha tano ("schedule 5"): Kinaongelea utaratibu wa kukabidhiana huduma kwenye saiti.
  7. Kiambatanisho cha sita ("schedule 6"): Kinaongelea protokali ya kutumia saiti, maana kwenye mnara mmoja kuna wakodishaji wengi. Yaani, unakuta kuna antena za Tigo, Airtel, Vodacom, na kadhalika.
Hitimisho

Mkataba mtabuka (framework contract) kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba kati ya nchi na nchi (IGA). Na mkataba wa saiti kati ya Helios na makampuni ya simu ni kama mkataba wa ngazi ya miradi kati ya nchi mwenyeji na mwekezaji wa kigeni (HGA).

Kwa hiyo, inaweekana, na ni lazima, kutaja gharama za mradi kama vvile kodi ya pango na pia ukomo wa muda kwenye IGA. Timu ya Johari Hamza haikuwa na weledi katika mambo haya.

Na kama ambavyo Helios na makampuni ya simu yanasaini "Framework Agreements" na baadaye "Project Site Agreements," vivyo hivyo DPW na TPA wanaweza na wanapaswa kusaini nyaraka za aina hii.

Hakuhitajiki IGA wala HGA kamwe ili kuiwezesha DPW au kampuni yoyote iwayo kuwekeza katika bandari za Tanzania!

Mama Amon Desk
"Summbawanga Town"
Sumbawanga.
30 Julai 2023.
View attachment 2702527
Kwakuwa jambo lilipendekezwa na kukubaliwa na Baraza la mawaziri, likalitishwa na ofisi ya mwansheria mkuu wa serkali ,likapitishwa na Bunge Kisha CCM wakalipitisha pia Kama chama Basi kinachoendelea ni kelele tu.

USSR
 
Hatukubaliani na wazo lako. Kelele za wenye nchi sio "kelele tu." Ukoloni wa walowezi kwa mara ya pili hapana. Hoja yetu iko hivi:

The Dubai Investors want to implement the projects within a policy and legal framework whose objective is to create an environment for foreign investment that protects the companies against changes in national priorities, together with the changes in law that can result.

In order to achieve this, IGA and HGA requires the state to make an agreement with the investor that contains what are called "stabilization clauses."

An Intergovernmental Agreement (IGA) between the states through whose territories an identified project system is to be operated. It addresses horizontal issues concerning the pipeline infrastructure as a whole – cooperation, land rights, tax structures, issues relevant to the implementation of the project.

The Host Government Agreements (HGA) between individual states within whose territory the project system is to be realized and the project investor(s). It addresses vertical issues concerning the project activity within the territory of each state – governmental obligations, investor duties, relevant standards, liability, issues relevant to the implementation of the project in each specific territory.

The stabilization clauses under IGA and HGA demand that there be no changes in the state’s policies that would alter the terms for the project initially agreed, without the consent of the other contracting party.

Sometimes the intention is to avoid the risks of nationalization, or the effects of changes in tax rates.

In other cases, the intention is much wider because the host government is required to undertake, for at least 66 and possibly 99 years, not to apply any fresh legislation or other measures if these will affect the profitability of the project.

This includes measures having their origin in international treaties to which the host government is a party and measures aimed at improvements in environmental and social protection, except for certain qualifications.

It is a framework that poses a clear and present threat to human rights and national sovereignty. We disagree.
 
I love this ! Detailed explanation
 
Pendekezo hili hapana! Uthabiti wa sheria zetu za PPP, Ardhi, Kodi, n.k. zinatosheleza mahitaji ya wawekezaji wa kimataifa.

Hazihitaji kuongezewa nguvu yoyote kutokana na IGA au HGA. DPW na TPA wasaini Fraework Contract, halafu Project Contracts zitafuata kadiri mahitaji yatakavyojitokeza.

Hakuna sababu ya IGA wala HGA, isipokuwa kama hatuelewi maana na umuhimu wa state sovereignty, hasa baada ya historia chungu ya European extrcative colonialism iliyotanguliwa na Arab settler colonialism.

Nakubaliana nawe kuwa tuna Sheria, Kanuni na Taratibu za uwekezaji ambazo makampuni ya nje hutumia. Nami nimekuwa nikiuliza, hadi sasa sijapata jibu Kwa nini DP World haipiti Kituo cha Uwekezaji (TIC) badala ya kutumia mgongo wa nchi yake, Dubai, kwa kutumia mkataba wa makubaliano (IGA) wenye vifungu batili?

Hoja yangu, unayoikataa, inazingatia ukweli kuwa, DP World inataka kuwa na uhakika wa usalama wa uwekezaji wake ambao unaaminishwa ni mkubwa sana (kiwango hakitajwi ila utatajwa kwenye mikataba ya utekelezaji - HGAs).
 
Sasa ndugu kama unajiuliza na haupati jibu, kwanini unahitimisha kuwa wanataka usalama wa kipekee!? Huu upekee ni kwa maslahi ya nani wakati kumbe sheria zetu (kupitia TIC) zina nguvu kuwapa usalama huo?
 
Hitimisho langu ni swali / mshangao
 
Hamna kitu hapo, Pumba tupu
unafananisha mkataba wa kukodisha kibanda cha mpesa na mikataba ya kuendesha nchi
Mleta mada amezunguka mbuyu baada amerudi pale pale, mwisho wa siku hakujibu swali lililoulizwa.
Muulizaji alitaka mfano wa IGA ambayo itakuwa na HGAs kisha ikataja gharama halisi ya uwekezaji.

Alipaswa amjibu IGA kati ya nchi x na y ilihitaji HGAs na ilitaja gharama halisi za uwekeza.

Ukalinganishe IGA na framework contracts baina ya kampuni na kampuni kweli??.
Mleta mada anakusudia kutuambia nini hapa??
 
IGA na HGA ni mikataba kati ya nchi na nchi na siyo baina ya makampuni, kama ulivyotaka tuelewe kwa mifano uliyotoa
Duu! Kama ambayo unajiuliza na haupati jibu kwanini DPW wawe na IGA na Tanzania na si kupitia TIC, ndivyo mleta bandiko kasema badala ya IGA na HGA, hawa jamaa; DPW na TPA wasaini Fraework Contract, halafu Project Contracts zitafuata kadiri mahitaji yatakavyojitokeza.
Naona unachojiuliza ndicho huyu mtu kajibu.
 
Back
Top Bottom