mmh hapo unataka kunichekesha tu! siku hizi kiswahili watu watu hawawezi kukiongea kwa ufasaha.fuatilia utaona mtu msomi tu anasema husiniambie, husije, habali, bizaa, inshu yaani ni shida tupu.watangazaji wengi wa radio ni majanga wako half cooked.
Nimecheka sana...Mwingine anasema 'gharama za masomo' kuwa ni 'bei za masomo'; wengine 'suala' kwa maana ya 'issue' wanasema 'swala'; 'afadhali' wanasema 'afadhari' au 'hafadhali'. 'kwenda' wanasema 'kwendaga'