Mgambo wa maadili wa Sharia wavamia lodge kutandika watu wakati wa Eid nchini Nigeria

Mgambo wa maadili wa Sharia wavamia lodge kutandika watu wakati wa Eid nchini Nigeria

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
60,816
Reaction score
100,481
Mgambo wa maadili wa Sharia katika Jimbo la Katsina, Nigeria wakiwa na viboko na marungu wamevamia lodge mojawapo jimboni humo na kuanza kutandika wateja.

Majimbo 12 kati ya 36 ya Nigeria yana utawala wa Sharia wa Kiislamu ambapo huwa na mgambo waitwao Hisba kuhakisha Sheria ya Kiislamu inafuatwa na waumini wa dini ya Kiislamu, huwa wanaweza kupita kwenye bar, lodges na hotel kutekeleza sharia za kuzuia uzinzi na unywaji pombe, pia huweza kuwaadabisha wanawake kwenye suala la mavazi na huakikisha waumini wanafunga wakati wa Ramadhani.

Huwa najiuliza kwenye utawala wa Sharia katika taifa la mchanganyiko kama Nigeria sasa wasimamizi wa sharia huwa wanatofautishaje kati ya Waislamu na Wakristo?!
Mfano wakikutwa lodge muislamu na mkristo wanazini sharia itatimizwaje hapo? Au akikutwa mtu anamuuzia kitimoto au pombe muislamu sharia itatekelezwaje hapo?!
Screenshot_20260322-165034~2.jpg
Screenshot_20260322-165233~3.jpg
 
changamoto sana hapo nigeria
Nigeria ilitakiwa itawaliwe kijeshi na madikteta wasiondekeza dini kama China au igawanywe ziwe nchi mbili Kaskazini na Kusini kila upande ushike hamsini zake.
 
Nigeria ilitakiwa itawaliwe kijeshi na madikteta wasiondekeza dini kama China au igawanywe ziwe nchi mbili Kaskazini na Kusini kila upande ushike hamsini zake.
Kabila la wa Hausa ndio tatizo Nigeria
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Nigeria ilitakiwa itawaliwe kijeshi na madikteta wasiondekeza dini kama China au igawanywe ziwe nchi mbili Kaskazini na Kusini kila upande ushike hamsini zake.
next week nitajaribu kufuatili hilo jambo nilielewe sema hizi nchi zingine mambo ya dini wangekuja hata hapa bongo kujifunza mi naona tunaenda vizuri sana hapa
 
Back
Top Bottom