#COVID19 Japan: Wachezaji wawili wa Afrika Kusini wapatikana na maambukizi ndani ya Kijiji cha Olimpiki

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Wachezaji wawili wa Afrika Kusini ambao wapo nchini Japan kushiriki mashindano ya Olimpiki wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona siku ya Jumamosi, wakitajwa kuwa washiriki wa kwanza wa mashindano hayo kupata maambukizi ya virusi vya corona wakiwa ndani ya Kijiji cha Olimpiki.

Washiriki wengine wawili, Kocha wa mchezo wa raga na mchambuzi wa video, wote raia wa Afrika Kusini wamepatikana pia na maambukizi ya virusi vya corona wakiwa nchini Japan, na kufanya idadi ya Waafrika Kusini walioambukizwa virusi hivyo kufikia wanne.

Mhudumu wa Afya wa msafara wa wachezaji wa mchezo wa raga amesema ameshangazwa na maambukizi kwani kigezo cha kuruhusiwa kutoka Afrika Kusini ni kutokuwa na maambukizi ya corona.

Mkuu wa Kamati ya Olimpiki amewahakikishia wananchi wa Japan kuwa uwezekano wa wao kupata maambukizi kutoka kwa washiriki wa mashindano ya Olimpiki ni ‘sifuri’ kutokana na tahadhari iliyowekwa.

Hata hivyo, bado kuna hali ya wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa visa vya maambukizi mapya katika mji wa Tokyo, kuzidi watu 1,000 kila siku kwa siku nne mfululizo.

Chanzo: SkySports
 
Covid 19 is myths trust me last year a crews of sailors in Navy 🚢🚢🚢 ship owned by France reportedly affected by COVID-19 without any conduct with mainland for 6months
 
Back
Top Bottom