Afrika Kusini: Sanamu ya Desmond Tutu iliyofunikwa kilemba cha Wapalestina yazinduliwa

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,615
Afrika Kusini kaishikia bango Israel. Ngoja tuone kama Israel itarudi nyuma.

Habari kamili;

Sanamu ya marehemu Askofu Mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu iliyofunikwa kilemba cha Wapalestina imezinduliwa mjini Cape Town kuashiria uungaji mkono wake kwa Palestina.

Wakfu wa Desmond na Leah Tutu Legacy ulisema kuwa sanamu hiyo itaonyeshwa kwa muda hadi shambulio la bomu mjini Gaza litakapositishwa.

Israel inasema inajaribu kuiondoa Hamas, ambayo ilianzisha mashambulizi dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba, na kuua watu 1,300 na kuwashikilia wengine 240 huko Gaza kama mateka.

Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas mjini Gaza inasema zaidi ya watu 23,350 - wengi wao wakiwa wanawake na watoto - wameuawa na Israel katika vita hivyo.

Askofu Mkuu Tutu alikuwa mkosoaji mkubwa wa sera za Israel dhidi ya Wapalestina ambazo alizifananisha na vitendo vya mamlaka ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Chama tawala cha ANC pia kwa muda mrefu kimekuwa kikiunga mkono hoja ya Palestina.

Israel leo(Ijumaa) imekuwa ikijitetea katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki mjini The Hague dhidi ya shutuma za Afrika Kusini kwamba inatekeleza mauaji ya kimbari huko Gaza

Ilisema Afrika Kusini imepotosha ukweli na kwamba ilikuwa imewasilisha "maelezo yanayopingana na ukweli" kuhusu mzozo wa Israel na Palestina.

Chanzo: BBC Sawahili


55f1d3ed-a822-4c3f-9225-cc0041ba82bc.jpg
 
Back
Top Bottom