January Makamba naamini amepata cha kujifunza

January Makamba naamini amepata cha kujifunza

Binadamu ndivyo tulivyo, mtu akifanya kazi yake eti kajipendekeza, January ana malengo yake na wala siyo uwaziri mkuu,,, acha kuanzisha mada za kiumbea na zisizo na msingi kwa nchi yetu

Kwa hiyo yule anayefunga watu kamba za viatu ndio kazi yake?
 
Kigango cha BAKWATA kitafikiriwa baadae ... So far ratio za Uteuzi ziko 5 :1
Kwenye Maisha kimbelembele hakifai kabisa, kujikweza sana karibu na wakubwa sio tiketi ya kupata wadhifa wa juu.

Nampa pole January Makamba, asubirie Uwaziri tu lakini sio Uwaziri Mkuu.

Wahenga wasema, kukaa karibu na Mahakama sio kujua sheria.
 
Hata uwaziri hapati.Shombo ya Kikwete hatuitaki kabisa.Wanalipi jema waliloifanyia nchi yetu mpaka waendelee kuwepo.Inatosha,wapumzike tu wasubiri mengineyo.
Kwenye Maisha kimbelembele hakifai kabisa, kujikweza sana karibu na wakubwa sio tiketi ya kupata wadhifa wa juu.

Nampa pole January Makamba, asubirie Uwaziri tu lakini sio Uwaziri Mkuu.

Wahenga wasema, kukaa karibu na Mahakama sio kujua sheria.
 
uwiiii nina raha sana... ok acha ngoma iendeleeee....

Mwakembe pole, january pole... tunataka viongozi wapya sio wale wanaovaa viatu vya baba zao..... ngoja niendelee na maombi kwa namna hii mie mtoto wa muokota vyuma vyakavu naweza pata ubunge wa kuteulikwa...khaaaa..
 
magufuli tumuombee kwa Mungu anaweza kutuvusha hasipobadilika
 
Kwenye Maisha kimbelembele hakifai kabisa, kujikweza sana karibu na wakubwa sio tiketi ya kupata wadhifa wa juu.

Nampa pole January Makamba, asubirie Uwaziri tu lakini sio Uwaziri Mkuu.

Wahenga wasema, kukaa karibu na Mahakama sio kujua sheria.
Hiyo nayo ni tia maji tia maji maana David Chanyeghea ametinga mahakama kuu kupinga ubunge wake , tusubiri tuone .
 
Ila alikuwa na uwezo wa kuwa raisi?

Ile alitumia kama platform ya kufanya ajulikane tu "Kujitangaza" angalia hata ACT sasa hivi inajulikana nchi nzima japo ina mbunge mmoja tu, waliutumia uchaguzi vizuri kujitangaza na sidhani kama walikua na nia ya kushindana hasa kwa kila jimbo
 
akatwe sehemu zote tu hata uwaziri maana kidondadonda kilizidi aisee
 
huyu si ndio yule alifeli kwenye sosho ikaja ile ya 8mb?
 
kishaandaliwa uwaziri wa mambo ya nje na miaka kumi ijayo ndo atakuja kuwa mgombea wa uraisi!!! kila kitu kwenye siasa kimeshapangwa kabla....

hawezi kuwa raisi maana mkapa atakuwa kuzimu au atakuwa amesha poteza nguvu
 
Acha majungu ww....Makamba ni president in the making....mliwekewa front kwenye kampeni kama strategy ya kuvutia vijana na pia mumzoee kwenye mambo makubwa ya kichama....ataingia kwa cc ya ccm, atapewa muda wa kukomaa na kuiva and finally mtaletewa kama mgombea urais...

Rais wa wasafi au:what:
 
Hii thread nilianzisha wiki iliyopita lakini mods wakaitoa,

Natoa ushauri tu kwa mods muwe waungwana kwa kuheshimu mawazo ya wengine hata yasiyowapendeza, kuna yanayofundisha na mengine kujenga.

Wahenga walinena "nionyeshe rafiki zako nikuambie ulivyo"

Niliona aina ya utendajikazi wa rais Magufuli ni tofauti kabisa na ulivyokuwa utendaji wa Kikwete ndio maana nikasema hivyo kwa kujiamini.

Magufuli ni mchapakazi, hapendi unafiki wa kujipendekeza hana uswahiba na mtu kama alivyokuwa mtangulizi wake.

Natabiri tena hata safu ya mawaziri itashangaza wengi.
 
Kwenye Maisha kimbelembele hakifai kabisa, kujikweza sana karibu na wakubwa sio tiketi ya kupata wadhifa wa juu.

Nampa pole January Makamba, asubirie Uwaziri tu lakini sio Uwaziri Mkuu.

Wahenga wasema, kukaa karibu na Mahakama sio kujua sheria.

Alikuambia anataka uwaziri mkuu?
 
Back
Top Bottom