January Makamba naamini amepata cha kujifunza

January Makamba naamini amepata cha kujifunza

Japo siipendi CCM ila ndio ukweli wenyewe, watu wepesi sana kusahau kuwa siasa ni mipango,Makamba hakuwa na uwezo wa kuwa PM kwa sasa hata kwenye mawazo yangu binafsi hakuwa kwenye list.

sasa huyu kasim,si bora makamba
 
Tunakunywa POMBE, tukigombana tunafanya SULUHU tunategemea MAJAALIWA ya Mola baada ya hapo tunaenda JOB

..hivi vijimisemo vingine vya kipuuzi sana..!
Yani ukishakunywa "pombe" unategemea "majaliwa" ya mola ndio uende kazini?!
Hiyo kazi itafanyika kweli?!
Nimeamini kuna watoto wengi sana humu...
 
hivi kweli mnadhani mh. January yusufu makamba hakujua nafadi hii 2015 si yake.? Kwa weredi na uanasiasa wake wazi anaonekana ni mwenye kujitambua kuliko sisi tunaoshangilia tusivovijua, jaji mkuu anatoka tanga, hii ilitosha kukuonyesha wazi january alitqmbua yeye siye ktk nafasi hiyo ya juu ya nchi inayozalishwa na mfumo na si kura za wananchi, tambueni dhamiri yake ya urais ingaliweza kuvuka nguvu ya mfumo kama mwalimu alivyowahi kuhudumu na chief justice nyalali.

January yusufu makamba amejipambanua kwa uaminifu,weredi na utayari wa kuhudumu ndani ya nchi na nje ya nchi kwa nafasi yoyote, amefanikiwa kukivuka kivuli cha mzee yusufu makamba, anasimama kwa miguu yake, anajisimamia jambo ambalo sisi wenzake wengi kwa rika alilomo bado tunasumbuka nalo.

Nilidhani vijana wenzangu ambao 5yrs to come tutakuwa wa makamo kidogo tujivunie huyu msambaa kwani kwa maoni yangu ametuwakilisha vyema sana tena akituondolea mauzauza ya ngeleja,maige ,masha vijana kama siye walishindwa kuhudumu accordingly.

Alipo jqnuary panahitaji mbolea yetu kumlinda,kumkuza,kumuombea ili apevuke akiwa imara na muadilifu tena na tena...

Congrats january yusufu makamba, karibu malinyi ...tuijenge tanzania

Ujumbe huu kwa hisani ya wapi? Lumumba, Bumbuli au Msoga?
 
umemaliza au unatafuta maneno ya kumalizia? hujitambui wewe mpuuzi mkubwa na kibaraka wa makamba....watu kama wewe ndio mnaowalamba watoto wa vigogo miknd ili wawatemee makombo ya rasilimali za nchi wanazotafuna. utaishia hivyo hivyo na ukibarka wako

Kujitambua kuna kamilika kwa kujua ukomo wa uwezo wako ktk kufikiri,kuamua na kushauri, mimi sisukumwi na maslahi binafsi na kwa dhati huyu kijana mwenzetu si mtu wa kupenda cheap popularity ama wapambe, tukubali kutokubaliana kuwa ktk rika yangu wapo vijana walopewa nafasi on both sides CCM /UKAWA ambao mimi naona hawakuitendea haki fursa hiyo na wapo walotenda vema...CCM January is the best...UKAWA Mnyika is the best lakini wapo waliozitumia fursa hizi hovyo hapo wapo kina Maige, Ngeleja, nampia UKAWA/Upinzani wapo kina Machali,Zitto

Tutambue karama na uwezo wa kujihifadhi wa January Yusufu Makamba na JohnJohn Mnyika...ni ngumu kuwakuta hawa vijana wenzetu kwenye fish business ama matamko ya hovyohovyp hata wanaposimama kujenga hoja hawasukumwi na umimi ama uchampioni bali Utanzania wao.

Ni heri unitukane tu lakini nakataa kubeza karama na vipawa vilivyomo kwa January Yusufu Makamba eti kisa nitaonekana najikomba! Tusiwe wanafiki kwenye genuine issues. in him you can see a leader, angelikuwa anatokea kule Malinyi kwetu ningelimuunga mkono bila hofu.
 
ujumbe huu kwa hisani ya wapi? Lumumba, bumbuli au msoga?

kwa hisani ya unyoofu wa moyo wangu binafsi, utu wema na kufikiri nje ya chuki.

Tukubali kama binadamu tena kijana ana mapungufu yake ambayo ni asili ya mwanadamu yeyote. Nimesema hivo kwani sina ushahidi nayo lakini ninafarijika nionapo mazuri yake mengi hadharani na namna anavoiendea jamii kwa uaminifu, nidhamu na kujiamini.

January hana la kujutia ama kusononekea ktk hiki mtoa hoja unachotaka tuamini.
 
Naamini sasa ni chuki binafsi na tushaanza kuingiza wivu usiopenda maendeleo. Ndio Binadamu tulivyo. Nashukuru kwa kuruhusu nami kutoa maoni na ushauri wangu kwenu.

Asanteni.
 
Ile wizara kwa mara ya kwana imepata sura ya uzalishaji na usimamizi...ujio wake kumsaidia Mbarawa kumeipa sura mpya TCRA...TTCL...Vietel...kasi ya Mkongo wa Taifa lakini imeisukuma serikali ktk kuingia ktk TEHAMA....

Kama Naibu Waziri ameweza kusimama imara ktk Bunge na kuipa Wizara hii uungwaji mkono usio mashaka.

Machache haya yatosha kuonyesha ni Kijana anayesimamia anachohubiri kwa matendo....

Niliaga ktk hili ila imenipasa kukujibu ingawaje sasa nahisi unahoji kwa dharau na makusudi yasiyojenga...

Hewala ndg yangu, Mnyonge mnyongeni ila haki yake ujitahidi aipate....Januari siyo wa hovyohovyoo hivo

Siku njema.
 
Acha majungu ww....Makamba ni president in the making....mliwekewa front kwenye kampeni kama strategy ya kuvutia vijana na pia mumzoee kwenye mambo makubwa ya kichama....ataingia kwa cc ya ccm, atapewa muda wa kukomaa na kuiva and finally mtaletewa kama mgombea urais...

kishaandaliwa uwaziri wa mambo ya nje na miaka kumi ijayo ndo atakuja kuwa mgombea wa uraisi!!! kila kitu kwenye siasa kimeshapangwa kabla....

Tutamkata sababu tume huru na katiba mpya zitakuwepo.
 
Huyo dogo ni mjinga sana kwanza ndo alikuwa kiongozi wa kuchakachua kura za UKAWA akitegemea kupewa huo wadhifa,kingine kichwa chake hakiko sawa anaugonjwa wa kujikomba komba,nitashangaa sana akipewa hata uwaziri itakuwa ni aibu kwa magufuli
 
umemaliza au unatafuta maneno ya kumalizia? hujitambui wewe mpuuzi mkubwa na kibaraka wa makamba....watu kama wewe ndio mnaowalamba watoto wa vigogo miknd ili wawatemee makombo ya rasilimali za nchi wanazotafuna. utaishia hivyo hivyo na ukibarka wako

Kujitambua kuna kamilika kwa kujua ukomo wa uwezo wako ktk kufikiri,kuamua na kushauri, mimi sisukumwi na maslahi binafsi na kwa dhati huyu kijana mwenzetu si mtu wa kupenda cheap popularity ama wapambe, tukubali kutokubaliana kuwa ktk rika yangu wapo vijana walopewa nafasi on both sides CCM /UKAWA ambao mimi naona hawakuitendea haki fursa hiyo na wapo walotenda vema...CCM January is the best...UKAWA Mnyika is the best lakini wapo waliozitumia fursa hizi hovyo hapo wapo kina Maige, Ngeleja, nampia UKAWA/Upinzani wapo kina Machali,Zitto

Tutambue karama na uwezo wa kujihifadhi wa January Yusufu Makamba na JohnJohn Mnyika...ni ngumu kuwakuta hawa vijana wenzetu kwenye fish business ama matamko ya hovyohovyp hata wanaposimama kujenga hoja hawasukumwi na umimi ama uchampioni bali Utanzania wao.

Ni heri unitukane tu lakini nakataa kubeza karama na vipawa vilivyomo kwa January Yusufu Makamba eti kisa nitaonekana najikomba! Tusiwe wanafiki kwenye genuine issues. in him you can see a leader, angelikuwa anatokea kule Malinyi kwetu ningelimuunga mkono bila hofu.

eti umesema makamba hana wapambe? kwani wewe ni mpambe wa nani? hv huyo january makamba unayejikomba kwake kila siku kaifanyia nini nchi hii?
 
Last edited by a moderator:
acha mawazo mgando,haka kama hajawa waziri mkuu at least atapata cheo kingine na kitengo stahiki,tuache uchama sasa na itikadi zisizo na msingi kwa taifsa letu
 
Watu bhana professional kwa kuchonganisha..mleta mada atakuwa mtaani kwao maarufu kwa kuvunja ndoa za watu
 
Back
Top Bottom