Friday, November 28, 2008
Language in this Blog
Watu kadhaa wamenitumia email kuuliza kwanini natumia Kiingereza kuandika kwenye blog hii wakati "lugha ya taifa" ni Kiswahili. Concept ya "lugha ya taifa" tunaweza kuijadili hadi asubuhi. Kwa kifupi, hapa ni ruksa kutumia Kiswahili au Kiingereza. Binafsi napenda kutumia Kiingereza kwasababu nadhani Kiswahili nakifahamu chote ila Kiingereza ni lugha ngeni kwangu kwahiyo napenda kuifanyia mazoezi zaidi lugha hii ngeni. And the only way to acquire proficiency kwenye lugha ni kuitumia mara kwa mara.
And my sense ni kwamba mtu yoyote ambaye ameweza ku-navigate the web mpaka akafika kwenye blog hii certainly atakuwa anaelewe lugha ya Kiingereza.
Posted by January Makamba at 5:10 PM 2 comments
Hilo ndio jibu alolotoa katika swali kuhusu utumiaji wa Kiingereza....
Kama msomi hatakiwi kusema anadhani ,anatakiwa kusema takwimu inaonyesha kuwa asilimia fulani ya walengwa wake wanaweza kusoma kingereza anachoandika.
Kama watanzania ndio walengwa wake je ni watanzania wangapi licha ya kujua kingereza wako competent enough kujadilia point zao nzuri ktk lugha hii ya kigeni.
Mimi nilichogundua ni kuwa kuna muda unapunguza kasi na ukali wa michango unapotumia lugha za kigeni ijapokuwa kuna kipindi baadhi ya misamiati ya lugha hii ya kigeni inaweka mkazo mzuri kwa mtu aneyefahamu.
Madai yake ya kutumia lugha hii ktk kujifunza zaidi kingereza kwa hiyo anataka kusema mission yake ktk kuanzisha blog hiyo ni kukuza kingereza chake.
Halafu kuna kitu kinatakiwa kutoka kwa watu kuwa kingereza si ndio ubora point ,ni lugha kama lugha zingine hata machizi waliozaliwa kwenye nchi zinazozungumza kingereza wanazungumza hiyo lugha ,hata mambumbu walifika grade school wanaweza kuandiaka nakuchangua kwenye hiyo blog .
Lack of self-esteem and defensive mechanism inawezekana kufanya kutumia lugha hivyo.