January Makamba, hizi picha unamaanisha nini? Makubwa!

January Makamba, hizi picha unamaanisha nini? Makubwa!

Kitendo cha January Makamba kupost picha twitter ambazo zina maana tata kimeibua minong'ono kuwa mbunge huyo wa Bumbuli amepigwa chini kwenye baraza la mawaziri.

Hivyo atabaki mbunge tu kama wabunge wengine.

Endapo itakuwa ni kweli basi hii moja ya mambo ambayo wananchi hawakutegemea kabisa huku wachache waliamini angeweza kuwa waziri mkuu na wengi wakiamini angeweza kuwa waziri na si naibu waziri.

Ukawa tulieni mbona mnaweweseka.........
 
January, Mwigulu, Kigwangala na Nape hawa watu ni malimbukeni wa siasa!
 
Picha zenyewe ndio hizo.... wekeni tafsiri zake


Nakama picha zenyewe ndo hizi? Kwa hakika ni mshangao mkubwa kwa mtu kama yeye kuweka picha hizi.Nahofia kuzi fafa nua kwani kuna mtu katukanwa kwa habari picha na ametajwa jina lake kwa habari picha ya mwisho.kama mwenye acount hiyo ange ifuta haraka.Dadisi kwa makini picha ya mwisho yule mtu alivyo kaa ni mtililiko wa herufi kuanzia mikono imetambulisha herufi mpaka mkia na hadi migu herufi ya mwisho ame ishia herufi l .
 
Nami nitachukua kadi ya ccm Magufuli akipiga chini Mawaziri waliokuwa awamu iliyopita maana walikuwa sehemu ya uozo
 
yaani ngazi alizotumia kushukia ama atakazotumia kupandia,anazing'oa na kuzichoma moto ,moja baada ya nyingineJE ATAPANDAJE KUTOKA HUMO AKIMALIZA KUZIOTEA MOTO(i mean atakapomaliza kuzitumia zikaisha atatokaje?)

Hapo inaweza ikamaanisha iyo ngazi ngazi alimwekea mtu apande, kadri huyo mtu alivokua anapanda hatua moja alikua akiharibu ngazi moja ili kumzuia yule wa chini asiweze kufika,mwisho jamaa wa juu katoka ndo maana unaona zile staircase za mwisho wa ngazi zipo, maanake wa juu katoka lakini wa jamaa chini kashindwa kutoka maana aliyetangulia kamwaribia ngazi..
Kwa great thinkers ukilinganisha hali ya sasa na hiyo picha unaweza ukahisi kitu, japo si lazima kila tunachohisi kiwe sahihi..kiukweli tunafaham January Ni mtu anayehitaji sana urais mwaka 2025 panapo majaliwa na namna njia ya kutokea Ni lazima utokee kwenye cabinet na wote tunakumbuka January amepambana sana kwenye uchaguzi huu kuhakikisha magufuli anashinda, kwenye campaign yeye ndo alikua Ni msemaji wa chama, kutokuepo kwake kwenye cabinet kama itakua hivyo, Ni jambo ambalo litafuta ndoto zake za urais 2025, ndo maana unaona kwenye picha amekaa kimya chini Kwani hakuna namna ya kufika juu na aliyemwekea ngazi apande ameharibu ngazi ili yeye asipande..
Hiyo Ni tafsiri yangu, inaweza isiwe sahihi pia.
 
Nakama picha zenyewe ndo hizi? Kwa hakika ni mshango mkubwa kwa mtu kama yeye kuweka picha hizi.Nahofia kuzi fafa nua kwani kuna mtu katukanwa kwa habari picha na ametajwa jina lake kwa habari picha ya mwisho.kama mwenye acount hiyo ange ifuta haraka.


Huo ufafanuzi ni kwa kiwango cha uwezo wako! Naona tayari kama ni mtihani umekwisha feli!
 
hivi january awe waziri kwa lipi hasa alilolifanya ?



Hakuwa anajua hata majukumu ya Wizara yake, moja ya mifano: tukumbuke alienda kushughuliia matatizo ya wakulima Songea wakati yeye anatakiwa kushughulikia mawasiliano
 
Mtu anapost picha za kijinga eti naye awali alikuwa anataka kuteuliwa kuwa Rais.
 
Naomba kujuzwa Baraza la mawaziri linapaswa litangazwe lini baadae ya Rais mteule kula kiapo? Atakapo amua yeye binafsi Au kuna muda maalum kwa Mujibu wa katiba ya JMT?
 
Niliishasema na narudia tena, kati ya wabunge ambao nina uhakika hawatauonja uwaziri safari hii ni January Makamba na Harrison Mwakyembe. Piga Ua hakuna atakayeupata. Wakiupata uwaziri naomba wadau wa jf mnichagulie hatua ya kujichukulia.
 
Nadhani wanamsingizia January. Ni account fake hii. Vinginevyo haya matusi makubwa kwa mkuu.
 
Dah ...hizi picha wakuu nikama ile michoro ya kina picaso na unaambiwa inathamani kubwa kweli.... millions of dollars....ukiitazama hiyo michoro na hizi picha kwa sisi low class huwezi pata big picture....yani nikama mzungu anavyocheza sebene in slow motion na hujui moves zake zinaenda na beat au rythim ipi...
 
magufuli akimtosa huyu kijana nitachukua kadi ya ccm ,huyu na mwigulu wabaki kwenye chama lumumba serekali haitaki watu wenye madoa mengi

Mimi naona hata Lumumba hawafai. Hawa jamaa hasahasa January Makamba ni wapigaji tu. Wakati wa blaablaa katika uongozi umepita. Wapigwe chini tu
 
Tuache utani, hapo January Makamba alikuwa anatuma ujumbe mzito kwa hali inayoendelea kwa sasa hapa nchini kuonyesha Makamba hakubaliani nayo, nadhani kuna wakubwa wamemtuma kufanya hivyo, Binafsi nimeelewa hivi.
1/Makufuli alitengenezwa tu kushika urais, ila waliomtengeneza wanamshangaa kujifinya mjuzi.
2/Makufuli ameanza kusahau alipotokea...
3/Makufuli hata afanye nini ili kujibadili sura lakini bado ni mfungwa...
4/Makufuli anajimaliza mwenyewe....
Saluti rafiki. Na ndiyo hapo watofautishe kuwa hii nchi siyo ya mtandao ni ya wananchi. Dr Magufuli ndiye atakaye tuumbia nchi mpya.
 
Hivi kwa mfano January Makamba angekuwa Rais wa Tanzania, hivi sasa watanzania tungekuwa tunatroti kivipi na hao TRA na TPA.
 
Back
Top Bottom