January Makamba: Gridi Nzima ya Taifa kufumuliwa kwa Trilioni 1

January Makamba: Gridi Nzima ya Taifa kufumuliwa kwa Trilioni 1

Habari ndugu!

Waziri wa Nishati na Madini January Makamba amesema Serikali unatarajia kuanza mradi mkubwa wa kusuka na kufumua Gridi ya Taifa.

Mradi huo utakaojulikana kama Gridi Imara unatarajia kutumia shilingi Tilioni Moja na unatarajia kusainiwa February 15,2023 Ukiwa na lengo la kukomesha kukatika katika Kwa Umeme Nchini.

My Take,ngoja tuone kama kero ya kukatika katika Kwa umeme itaisha.👇


Hakuna lolote wajanja tu wamekuja na mpango wa kuiba hela za umma kibao. Kunakua na mpango wa repair and maintanance tu sio complete overhaul. Hata nchi tajiri ukichunguza hawajawahi kua mpango kama huo. Huu ni ubadhrifu tu. Jamaa ulaji iko kwenye damu.
 
Makamba ni mzuri katika upigaji kwa kuanzisha madudu madudu yasiyoeleweka.

Why mfumue grid? Kwanini msifanye Preventive maintanance ambayo ni cheap?
 
Isije kuwa team nzima inatafuta fedha ya 2025 election campaign!!!. Jamaa akawa ametoa wazo kama hili na likapita kwa kura nyingi mno.
 
Habari ndugu!

Waziri wa Nishati na Madini January Makamba amesema Serikali unatarajia kuanza mradi mkubwa wa kusuka na kufumua Gridi ya Taifa.

Mradi huo utakaojulikana kama Gridi Imara unatarajia kutumia shilingi Tilioni Moja na unatarajia kusainiwa February 15,2023 Ukiwa na lengo la kukomesha kukatika katika Kwa Umeme Nchini.

My Take,ngoja tuone kama kero ya kukatika katika Kwa umeme itaisha.👇


Walishapiga kwenye kinachoitwa ukarabati wa njia za kusambaza umeme na wakaahidi hautakatika katika tukasema sawa kwa sababu wakati wa kalemani mitambo haijawahi kuzimwa.

Sasa amekuja na project ya ufumuaji wa grid nzima na kuisuka upya hamadi 2025 election hii hapa! Basically hii Ni plan ya kupiga mpunga Mana hiyo estimation ilifanyika lini na kwa budgeti ipi hatujui!

Msisahau kuna lile likampuni la kihindi linapiga pesa kwa kwenda mbele!
Twafwa
 
Tatizo la umeme tz siyo kiwango Cha umeme kinachozalishwa Bali miundombinu ya kuufikisha umeme kwa mlaji
Daaah, unaweza ukasema mtu analishwa maneno.

Tatizo lilikuwa UCHAKAVU wa mitambo, ikaja UKAME, wamehamia kwenye GRIDI sasa, na wewe unaongezea MIUNDOMBINU sio? Hii yote ni miaka 2 tu tangu muwepo ofisi kubwa!

Mkiendelea hivi, itatulazimu tumtengaze Magu kuwa MWENYE HERI, kila kitu kilimtii kama ndio hivyo.
 
Wangejitahidi haswa kwenye ubora wa umeme. Umeme bora ni ule ambao una power factor ya 1.
Kwa sasa sidhani kama huu umeme unafika hata power factor ya 0.8!
Hili litawezekana hasa kwa kupunguza idadi ya nyumba zinazohudumiwa na transfomer moja au kwa kuweka transfomer kubwa zaidi kwenye mitaa.
Mkuu, umeongea kitaalamu kidogo, ila hiyo Power factor ya 1 inapatikanaje? Nipe ilmu hii.

Gridi inaweza kuwa na PF 1? Inaruhusika kiumeme? Inawezekana? Wafanyaje?
 
Kaka unawezaje kupata Power Factor ya 1 ? Labda Commercially ila Practically ni ngumu. Sababu hapa unaongelea Transmission line Kuna losses kutokana na Impedances na other factors

Labda uwe na Real Power pekee with no reactive power au uwe na Pure Resistive loads jambo ambalo haliwezekani practically.
Inawezekana. Hizi transfomer za miji mikubwa kama Dar inatakiwa wafunge zote za 500KVA. Hutu tudogo tudogo wafunge huko kwenye REA vijijini.
 
Mkuu, umeongea kitaalamu kidogo, ila hiyo Power factor ya 1 inapatikanaje? Nipe ilmu hii.

Gridi inaweza kuwa na PF 1? Inaruhusika kiumeme? Inawezekana? Wafanyaje?
Kule kwenye mitambo ya uzalishaji kama kwenye bwawa la Nyerere wafunge mashine za maana. Sio hizi za mchina...
 
Kule kwenye mitambo ya uzalishaji kama kwenye bwawa la Nyerere wafunge mashine za maana. Sio hizi za mchina...
Nimeona kuna mtaalamu amejaribu kuelezea kuwa PF ya 1 haiwezi kuwepo kutokana na transmission lines na walaji wa mwisho.

Hii ya mashine za maana, inakuaje kuaje pia?
 
Habari ndugu!

Waziri wa Nishati na Madini January Makamba amesema Serikali unatarajia kuanza mradi mkubwa wa kusuka na kufumua Gridi ya Taifa.

Mradi huo utakaojulikana kama Gridi Imara unatarajia kutumia shilingi Tilioni Moja na unatarajia kusainiwa February 15,2023 Ukiwa na lengo la kukomesha kukatika katika Kwa Umeme Nchini.

My Take,ngoja tuone kama kero ya kukatika katika Kwa umeme itaisha.👇


Na hata ingekuwa kweli, baada ya ukarabati (usukaji mpya) huo, hatua inayofuatia ingekuwa kubinafsisha hiyo gridi.
Haya ndiyo wanayojivunia sana hawa wapigaji.
 
Mjiandae kwa mgao mkali wa umeme.

Hiyo estimation imefanywa lini na imefanywa na kampuni gani?
Estimations imefanywa na Kipara Engineering National Grid Reform Electrification Company Limited -a subsidiary company of Taifa Gas Distribution Company Limited!

Rejea maelekezo ya Queen of Msoga Kingdom and Dukess of Zanzibar kwamba itumike Single sourcing kupata wakandarasi!
 
Back
Top Bottom