Kagera Kuingia Gridi ya Taifa: Umeme wa Uhakika

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
580
Reaction score
546
📍Ngara, Kagera

▪️Serikali yaanza utekelezaji wa mradi wa umeme kuunganisha Mkoa wa Kagera kwenye Gridi ya Taifa

▪️Waziri Ndejembi aweka jiwe la msingi la njia ya kusafirisha umeme Kyaka - Benaco

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka pamoja na kituo cha kupoza umeme cha Benaco, ambao utaunganisha Mkoa wa Kagera kwenye Gridi ya Taifa, hatua itakayomaliza changamoto ya kukatika kwa umeme katika wilaya za mkoa huo.

Waziri Ndejembi ameweka jiwe la msingi la leo tarehe 9 Mei 2026 wilayani Ngara mkoani Kagera, ambapo amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuukamilisha ndani ya miezi 24 kama mkataba unavyoelekeza.

“Tunachotarajia ni kuona ndani ya miezi 24 Mkoa wa Kagera umeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na changamoto za umeme zilizowasolishwa na Mhe. Mbunge wa Ngara ziwe historia kwa wananchi hawa,” amesema Ndejembi.

Akizungumza na wananchi, Waziri Ndejembi amesema kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Benaco hadi Kyaka unalenga kuunganisha Mkoa wa Kagera kwenye Gridi ya Taifa na kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika wakati wote.

Ameeleza kuwa Mkoa wa Kagera kwa muda mrefu umekuwa ukitegemea umeme kutoka nchi jirani, hivyo kupitia mradi huo Mkoa wa Kagera utaunganishwa moja kwa moja na Gridi ya Taifa, hatua itakayoongeza uhakika wa nishati na kuimarisha shughuli za kiuchumi na kijamii.

Aidha, Waziri Ndejembi amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati na kueleza kuwa Wizara itaendelea kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika wakati wote.

Katika hatua nyingine, amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja inapatikana transfoma yenye uwezo mkubwa pamoja na kuendelea kufanya marekebisho katika njia za kusafirishia umeme ili kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Ngara wanapata umeme wa uhakika katika kipindi wanachosubiri mradi huo ukamilike.

“Wananchi wa Ngara wanataka kupata umeme wa uhakika ambao haukatikikatiki, sasa nikuagize Mkurugenzi wa TANESCO na timu yako kuhakikisha tunapata transfoma mpya mara moja yenye uwezo mkubwa ya kuhakikisha tunapata umeme katika Wilaya ya Ngara, nakupatia mwezi mmoja,” amesema Ndejembi.

Ameongeza kuwa mradi huo unatarajiwa kuongeza ajira, kuhamasisha uwekezaji na kukuza shughuli za kilimo, uvuvi, ufugaji pamoja na uendelezaji wa viwanda katika ukanda wa ziwa, kwani ni fursa muhimu kwa wananchi wa Kagera na mikoa jirani.

Waziri Ndejembi ameziagiza TANESCO na mkandarasi kutoa fursa za kazi kwa wananchi wa maeneo yanakotekelezwa mradi katika wilaya za Ngara, Karagwe na Missenyi ili waweze kuwa sehemu ya mradi huo na kujiinua kiuchumi na kibiashara.
20260509_174522.jpg
 
Waziri Ndejembi ameziagiza TANESCO na mkandarasi kutoa fursa za kazi kwa wananchi wa maeneo yanakotekelezwa mradi katika wilaya za Ngara, Karagwe na Missenyi ili waweze kuwa sehemu ya mradi huo na kujiinua kiuchumi na kibiashara.View attachment 3586124
well done serikali sikivu ya ccm CHINI YA DR.SAMIA SULUHU HASSAN,

ni hatua kubwa na muhimu sana kwa ustawi wa maisha ya wana ngara, Kagera
 
Una andika ukiwa wapi? Unaifahamu Ngara?

Unafahamu kuwa umeme katika wilaya hiyo hukatika mara 20 kwa siku?
Unafahamu Ntara kunazalishwa umeme kutokana na maporomoko ya Rusumo?

Unafahamu kuwa umeme unaozalishwa hugawanywa kati ya Rwanda,Burundi na Tanzania?
Unafahamu kuwa umeme huo unaotosheleza mkoa wa kagera na kubaki, husafirishwa hadi Nyakanazi, na kupelekwa kunakoitwa kwenye gridi ya taifa?
Eti leo.mnafanya nini? Tusaidie kuelewa sisi tulioishia darasa la 4c kwamba mliweza vipi kusafirisha umeme kutoka Ngara kwenda Kwenye grid ya taifa na sasa mnaurejesha kwa grid! Hatuwaelewi.
 
Mkuu pole sana , huyo ni kidampa mmoja tu hapo Lumumba ulichomuuliza kwanza ni kimo kirefu kwa uelewa wake.

Hao wana kagroup kao huko kiongozi wao ni Kihongosi na Msigwa wanapewa vitu wanacopy wanakuja kujaza server halafu wanapeleka screeshot wanapewa buku 7 yao.

Hivyo ulichomuuliza hawezi kukisoma , kukielewa wala kukijibu.

Ni muda sasa watanzania wauone uchawa kama miongoni mwa maadui wa taifa ndio itakua njia ya kuukomesha.
 
Back
Top Bottom