January Makamba mtia nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM leo amesababisha wanachi kutoa machozi katika Wilayani ya Misenye mkoani Kagera, January yuko kwenye harakati ya kutafuta wadhamini.
January ambaye amevunja record ya kupata wadhamini wengi kuliko mgombea yeyote aliyefika katika ardhi ya Kagera, aliufanya umati kububujikwa na machozi pale alipomkumbuka Bibi yake kipenzi aliyefariki mwaka 2010, Machi
Akiongea kwa kuwakumbusha mambo aliyoyafanya akiwa na umri wea miaka tisa akiwa analelewa na Bibi yake kijijini pale, alisema Tulikuwa tunaishi wawili tu, Bibi amefariki hakuniacha Mbunge wala Waziri
..(akanyamaza kidogo) , amenifundisha mengi jinsi ya kula, nidhamu, heshima na mambo mengi, nafikiri huko aliko anafurahi
Aidha katika hotuba yake ambayo wanachi walikuwa makini kuisikiliza alibainisha mambo kadhaa lakini kubwa ikiwa kero ya fedha kiduchu wanayopata wakulima wa miwa wa Wilaya ya Misenye na ukosefu wa maji safi na salama